Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

﴾وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿

“Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini” [Aali ‘Imraan: 139]

Kipindi cha hivi majuzi kimeshuhudia mjumuiko wa mashambulizi mabaya ambayo yamepelekea kwa vifo vya raia, Waislamu na wasiokuwa Waislamu ikijumuisha wanawake na watoto wengi. Hata kama wengi wao katika Waislamu japo sio wote, wanapinga vitendo hivi kwa sababu vinakwenda kinyume na Dini yao na msimamo jumla wa Ulaya hususan ule wa Ufaransa ambao vyombo vyake vya habari na ndimi za wanasiasa wake katika kutumia msamiati “Ugaidi wa Kiislamu” ukiunasibisha na fikra za Jihad ndani ya Uislamu… Natija yake ni kuwa Uislamu umefungamanishwa na udhalimu, uhayawani na umwagaji damu ilhali jamii ya Waislamu kwa ujumla imelaumiwa na kutakiwa kuachana na Dini yao na kutangaza utiifu kwa usekula na misingi yake ya kimagharibi.

Dola za kikoloni zinakalia kwa mabavu baadhi ya ardhi za Waislamu na kudhibiti ardhi nyingine na zimo katika kuwaua Waislamu na kuwashambulia wasiokuwa na hatia pasina kujali wala kuzingatia kuhesabiwa au maadili ya utu… Na yaliyotokea ndani ya Iraq na Afghanistan pale ambapo mamia ya maelfu ya watu walipouliwa bado limo katika kumbukumbu zetu… kama zinavyopora rasilimali za Waislamu na kuharibu ardhi zao ili kuhifadhi ulafi wa maslahi ya kirasilimali… Uislamu umefanya kuwa ni lazima kwa Waislamu kulinda ardhi, matukufu na rasilimali zao na kuwafaradhishia wawapinge wakoloni. Licha ya hayo, Hukmu za Jihad ndani ya Uislamu – ziko kinyume na yanayofanywa na dola (zinazoitwa za ustaarabu) za kikoloni! – Unafanya kuwa uhadaifu ni Haram na umeharamisha kuua wasiokuwa wapiganaji au kuwashambulia wanawake na watoto pamoja na watu walio na mkataba… Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Nabii (saw):

«... وَلاَ تَغْدِرُوا، وَلاَ تَغُلُّوا، وَلاَ تُمَثِّلُوا، وَلاَ تَقْتُلُوا وَلِيدًا»“…Na musisaliti, na musipitilize, musikatekate na musiuwe mtoto” na kauli yake (saw): «... فَلَا تَقْتُلُوا ذُرِّيَّةً، وَلَا عَسِيفًا [أجيرا أو عاملا لا علاقة له بالحرب]»“… Musiue kizazi au ‘Aseef [Mkono ulio ajiriwa au mfanyikazi asiyehusika na vita]”. Ibn ‘Umar alisema: Mwanamke aliyeuliwa aligundilika miongoni mwa vita vya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) na hivyo basi Nabii akaharamisha kuuliwa kwa wanawake na watoto. Shafi’I alisema kuhusiana na Musta’min (aliyepewa usalama): “Lau watakuwa wamempa usalama basi usalama wao utaheshimiwa (utajumuisha): Usalama wake kwao wao, hawezi kuwaua na hawezi kuwasaliti” na Ibn Mawdood Hanafi alisema: “Na ikiwa Muislamu ataingia Dar ul-Harb (ardhi ya vita) akiwa na ulinzi/usalama hatakiwi kujihusisha na lolote lile dhidi ya damu zao au mali zao na ni kwa sababu inazingatiwa kufanya hivyo ni kuwasaliti nako kumeharamishwa.” Hizi ndizo hukmu za Uislamu kuhusiana na Al-Jihad na Al-Harb (vita) juu ya Musta’min… na zinakilisha hukmu kubwa na zilizo bora.

Wanasiasa wa Ulaya wanalijua hili kwa yakini na bado wanayapatiliza matukio tuliyo yataja ili kuunasibisha uhayawani na Uislamu na udhalimu kwa fikra ya Al-Jihad nako ni kuwaonyesha wale wanaolingania utekelezaji wa Uislamu ndani ya ardhi za Waislamu kuwa ni watu wanaopenda kumwaga damu magaidi… Napia ni sababu ili waweze kujiwekea pazia katika matendo yao ya kutisha ya kikoloni mbele ya watu wao na ili iwe ni kisingizio cha utekelezaji wa njama zao kwa misingi ya fikra ya kuubadilisha Uislamu kwa kubadilisha fahamu na hukmu  zake na kukijenga kizazi kipya kwa kile wanachokiita “Uislamu wa Ulaya.” Tunawapa onyo Waislamu juu ya mipango hii na tunatoa mwito kwao wajifakhiri na Dini yao na wajifunge kwa Shari’áh yao na kujifakhiri na fahamu zake zinazojumuisha fahamu ya Al-Jihad. Na lazima wajue kwamba mitihani itakavyokuwa mikali na matatizo yatakavyokuwa, mustakbali utakuwa ni kwa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt)

حَتَّىٰ إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ﴿

“Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya wakosefu.” [Yusuf: 110].


H. 20 Shawwal 1437
M. : Jumatatu, 25 Julai 2016

Hizb-ut-Tahrir
Ulaya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu