Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Barua kwa Raisi wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), jamaa zake na Maswahaba zake (ra).

Bw. Shavkat Mirziyoyev, katika hotuba yako kwa kikao cha 46 cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2021, ulisema katika taarifa yako: “Kama sehemu ya kutambulisha utaratibu wa kitaifa wa kuzuia mateso, tutaendelea kukandamiza vikali aina zote za mateso, unyama au udhalilishaji. Uhalifu kama huo hautakuwa na sheria ya mipaka. Tunakusudia kuidhinisha Itifaki ya Hiari ya Mkataba dhidi ya Mateso.” Na inajulikana kuwa serikali ya Uzbekistan imejiunga na makubaliano haya na kuahidi kuwalinda watu wa Uzbekistan kutokana na uhalifu wa mateso.

Katika mwaka huo huo, pia ulitia saini azimio jipya, “Katika Kuboresha Mfumo wa Kuzuia Mateso.” Kwa ajili hiyo, kozi za mafunzo zimekuwa zikiandaliwa katika uwanja wa kupambana na mateso, kwa wale wanaofanya uchunguzi wa haraka, uchunguzi wa awali, shughuli za uchunguzi na uchunguzi wa awali na kwa wafanyikazi wa taasisi kutekeleza adhabu. Mnamo Julai 19, 2023, kozi ya mafunzo ilifanyika katika jimbo la Tashkent juu ya mada, “Kuboresha ustadi wa kitaalamu wa wafanyikazi wa asasi za serikali kuhusiana na utayarishaji wa ripoti ya mara kwa mara ya sita ya Jamhuri ya Uzbekistan juu ya utekelezaji Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso na Unyanyasaji na Adhabu Nyengine za Kikatili, za Kinyama au za Kushusha hadhi.” Kwa mujibu wa huduma ya vyombo vya habari ya Mahakama Upeo ya Jamhuri ya Uzbekistan, leo Uzbekistan imeidhinisha hati zaidi ya themanini za kimataifa, katika uwanja wa haki za binadamu na uhuru. Katika suala hili, mikutano na semina nyingi zilifanyika na maamuzi yalichukuliwa ndani ya nchi.

Licha ya hatua na maamuzi yaliyochukuliwa ili kuhakikisha haki za binadamu na uhuru wa raia wa Uzbekistan, isipokuwa mnamo tarehe 4 Januari 2024, maafisa wa masuala ya ndani wakishirikiana na idara ya upelelezi usiku wa manane walivamia nyumba za baadhi ya ndugu zetu ambao wanaishi katika jiji la Tashkent ambao ni wanachama (Mashababu) wa Hizb ut Tahrir ambao walihukumiwa mwaka 1999-2000 na kuachiliwa huru baada ya miaka mingi ya kifungo cha takriban miaka 20. Idadi kadhaa ya wanachama (Mashababu) wa Hizb ut Tahrir walikamatwa kihalifu katika mazingira ya kutisha na maafisa waliojifunika nyuso wa Kikosi Maalumu. Mashababu hao walioletwa katika Wizara ya Mambo ya Ndani walipitia mateso makali. Wakati wa kesi ya vijana hawa 23, iliyoanza mnamo tarehe 9 Mei mwaka huu katika wilaya ya Sheikhan Tahur ya Tashkent, Mashababu hao walimsimulia hakimu jinsi walivyoteswa baada ya kukamatwa, ikiwemo:

1) Baada ya Mashababu kufikishwa kwenye Afisi ya Mambo ya Ndani, wanawekwa mifuko vichwani mwao na kuwawekea shinikizo kubwa kwa siku mbili, wakiwatesa kuanzia saa nane usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

2) Mashababu walilazimishwa kutia sahihi hati ya ungamo, iliyotayarishwa mapema na chombo cha uchunguzi, ili kutumia ungamo hili kama msingi wa mashtaka, kama ifuatavyo:

a) Iwapo mmoja wa wanachama (Shab) hakusaini ungamo, walitishia kumleta mke wake afisini humo na kumbaka...

b) Shab mwengine alitishiwa kuletwa mwanawe anayesoma nje ya nchi hadi Uzbekistan kupitia ubalozi.

c) Mtoto mwengine wa Shab aliletwa katika Afisi ya Mambo ya Ndani na kulazimishwa kutia saini hati ya kukiri akieleza kwamba mtoto wake angefungwa iwapo hatatia saini.

d) Katika sehemu nyingine, uchunguzi wa awali ulifanyika kwa mmoja wa ndugu zetu kabla ya uchunguzi, ambapo hata aliteswa na nguvu za umeme.

Inajulikana kuwa Katiba na sheria ya Uzbekistan inakataza vikali kukamatwa na kuwekwa kizuizini kiholela. Walakini, mamlaka za serikali bado zinaendelea na tabia hii. Hakukuwa na ushahidi wa kimada unaothibitisha hatia ya watu waliotajwa hapo juu waliokamatwa huko Tashkent. Hakukuwa na ushuhuda wa mwathirika dhidi yao. Walikamatwa bila haki! Ingawa Jamhuri ya Uzbekistan imeidhinisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Mateso, Mashababu waliteswa kikatili. Walilazimishwa kutoa ungamo na ushuhuda kwa kulazimishwa na maafisa wa uchunguzi. Vifungu vya 159 na 244 vya Sheria ya Jamhuri ya Uzbekistan, ambavyo vilitumiwa dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir wakati wa utawala wa zamani wa Karimov, vilibandikwa juu ya Mashababu hawa wote.

Na hapa tunauliza: Utawala huu unasubutuje kuwakamata na kuwatesa wale wanaosema “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu” na wakajitahidi kwa ajili kheri ya Uzbekistan na watu wake, na wakati huo huo kuwaruhusu wahalifu na watenda maovu kueneza ufisadi, uporaji na uharibifu katika nchi kwa uhuru na usahali kamili? unasubutuje? Na serikali iko wapi na kauli mbiu zake: “Uhuru wa fikra na imani,” “fikra dhidi ya fikra, dhumuni dhidi ya dhumuni..”?

Yaliyotokea na yanayoendelea Uzbekistan yanathibitisha kushindwa kifikra kwa utawala wa kisekula na kuendelea kwa watu wake wenye ushawishi mkubwa katika nyayo za muuaji Karimov... Vyenginevyo, kwa nini utawala huo unarudia kuwakamata na kuwatesa Mashababu wa Hizb ut Tahrir, ambao wametumia zaidi ya miaka ishirini ya maisha yao katika magereza ya Uzbekistan? Na kwa nini utawala unasema uongo na kuzua mashtaka yasiyo na msingi?!

Kumhukumu mtu kwa ajili tu ya fikra na imani sio jambo geni kwa watu wa Uzbekistan. Wamelizoea tangu utawala wa Karimov, jambo ambalo linaweza kumfanya mtu yeyote asiye na hatia kuwa na hatia. Lakini kinachoshangaza ni viongozi wa utawala wa sasa kuendelea kushikamana na njia ya utawala wa zamani, licha ya kudai kuwa hawafanani na utawala uliopita katika “sera za ukandamizaji na kunyamazisha sauti!”

Hapo chini, tunakupa orodha ya majina ya ndugu zetu wanaoshtakiwa katika wilaya ya Sheikhan Tahur ya Tashkent:

1) Yakubov Muradjan Nemtaovich

2) Afzalov Mahmut Dadabojevic

3) Alamov Isamuddin Jalalovich

4) Hekmatov Fakhruddin Sharafovich

5) Fazilbekov Dawaranbek Ulugbekovich

6) Akhonjanov Omid Abdurakhimovich

7) Mamurov Dilmurad Mukhtarovich

8) Tulaganov Mirzad Mirvoshidovich

9) Mirzi Akhmedov Mashrab Shamilevich

10) Gafurov Bakhtiyar Talatovich

11) Mirtalibov Abdurazak Abdovatahovich

12) Ashrafov Sadr al-Din Saladinovich

13) Ali Mammadov Aziz Agzamovich

14) Mirdib Akhmedov, Atabek Abdul Khalilovic

15) Rakhmetov Anwar Samadovich

16) Yuldashev Anorgan Sabitovich

17) Murat Tahirovic Nizamov

18) Kamalov Khairullah Abdul Ahdevich

19) Mahmudov Dilmurad Rahimovich

20) Abdullah Yev Zabihullah Khalilullah Yevitch

21) Abdurrahmanov Shaukat Abdurashidovich

22) Rahimov Ebadullah Rakhmonovich

23) Shamsev Alam Tulyaganovich

Hii ndiyo orodha ya watu wetu (Mashababu) ambao walikamatwa kwa dhulma katika maeneo ya Tashkent, Andijan, Hawqan, Karshi na Samarkand. Waliletwa Tashkent na wanachunguzwa:

1) Musa Yev Shukrallah Saadallah Yevitch

2) Salimov Dilshad

3) Tokhtasinov Abdul Hamid

4) Mammadov Mammadjan

5) Masalev Ravshan

6) Amanturdiyev Abdul Ghaffar

7) Timirov Torakul

8) Argachev Khurshid

9) Hemetov Atabek

10) Azizov Bakhtiar

11) Khakimov Bakhtiar

12) Yuldashev Kemal

13) Razquf Babur

14) Abdurrahmanov Anwar

15) Tagayev Shaukat

16) Arabov Ulugbek

Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu hatima ya wale waliotajwa, tukijua kuhusu mateso na shinikizo ambalo Mashababu wetu wanakabili wakati wa kesi zao.

Hizb ut Tahrir sio shirika la kigaidi, na chama hiki, ambacho kimekuwa kikifanya kazi katika nchi zaidi ya hamsini kwa zaidi ya miaka sabiini tangu kuanzishwa kwake, hakijarekodiwa au kuthibitishwa kufanya kitendo chochote cha vurugu au hujuma mahali popote... Ni zaidi ya miaka ishirini na tano sasa tangu mamlaka za Uzbekistan zitangaze vita vyao dhidi ya Hizb ut Tahrir. Licha ya jinai zote za kutisha, mauaji ya kutisha, mateso mabaya yenye kusababisha kifo, na vifungo vya miongo kadhaa vilivyofanywa na kundi la wahalifu ndani ya vyombo vya usalama vya Uzbekistan dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir, hakuna tukio hata moja la vurugu au hujuma ambayo imethibitishwa au kurekodiwa kuwa imefanywa na Mashababu wa Hizb dhidi ya serikali hii na wauaji wake!

Kujumuishwa kwa Hizb ut Tahrir kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi nchini Uzbekistan hakuna msingi kabisa, bali ni uhalifu na vitisho vikubwa. Kwa hiyo, tunazitaka mamlaka za kidini zenye hekima za Waislamu nchini Uzbekistan, kamati ya kidini, vyombo vya kutekeleza sheria, na asasi zengine rasmi kushinikiza kuondolewa kwa Hizb ut Tahrir kwenye orodha ya ugaidi!

Watu hao wasafi, wema, na wacha Mungu ambao sasa wanahukumiwa kwa dhulma na kwa ukali wamethibitisha kwamba walipunguza uhalifu katika maeneo ambayo walikuwepo. Walibeba ulinganizi kwa wahalifu na wezi wapotovu ambao hawakujali, na kwa neema ya Mwenyezi Mungu walijigeuza kuwa watu wema wenye tabia njema.

Wale wanaohukumiwa walitanguliza maslahi, na usalama wa Uzbekistan zaidi ya maslahi yao na usalama wa kibinafsi!

Wale wanaohukumiwa miongoni mwa watu wa imani hawana unafiki ndani yao; wanasema kweli bila ya kuogopa lawama ya yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Ni watu wa fikra na njia.

{وَمَنْ أَحْسَنُ  قَوْلاً مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحاً وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ}

 “Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?’” [Surah Al-Fussilat 41:33].

Kwa nini watu wema na wasafi wanalazimishwa kwenda uhamishoni, wakiiacha nchi yao na kuhamia ng’ambo ili kuepuka dhulma, vifungo, na mauaji?

Tunamwambia Bw. Shavkat Mirziyoyev: Mashababu wote wa Hizb ut Tahrir wanaozuiliwa katika magereza ya Uzbekistan, ambao kwa sasa wako katika kesi, wanaofanyiwa uchunguzi, au wanaoishi uhamishoni, ni Wauzbekistani. Mwenyezi Mungu amewapa haki kamili ya kutoa maoni yao kwa manufaa ya nchi hii... Zaidi ya hayo, ulipochukua urais, ulikula kiapo kwenye muundo huo wa kikatiba uliothibitisha haki ya kujieleza na kuabudu. Hivyo basi, utawala haujashikamana na amri ya Mwenyezi Mungu wala muundo huo wa kikatiba kiutendaji! Kwa hivyo, tunataka kutoka kwako:

1) Kuondolewa kwa kibandiko cha “shirika la kigaidi” kutoka kwa Hizb ut Tahrir.

2) Kuachiliwa mara moja kwa wafungwa wote kutoka kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir ambao wamezuiliwa kinyume cha sheria katika magereza ya Uzbekistan, ambao baadhi yao wamezuiliwa kwa miaka ishirini na tano.

3) Kwamba mashtaka mazito ya jinai dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir wanaohukumiwa huko Tashkent yafutwe, waachiliwe huru, na wale waliowatesa, kuwaua na kuwadhulumu wahukumiwe.

4) Kukomesha kufanya uchunguzi kwa Mashababu wetu waliokamatwa kwa dhulma na kwa vurugu.

5) Kukomesha mashtaka ya jinai ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir, kwa watu wanaotafutwa na kwa wale wanaoishi nje ya nchi.

#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД

#PleaFromUzbekistan

#صرخة_من_أوزبيكستان

H. 29 Dhu al-Hijjah 1445
M. : Ijumaa, 05 Julai 2024

Hizb-ut-Tahrir
Uzbekistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu