Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Baada ya Majanga na Damu ... Mkataba wa Riyadh kati ya Hadi na Baraza la Mpito, Uko wapi Uislamu na Vipengee vyake?!?!


Ni Mchezo Mchafu wa Kisiasa ambao Asili yake Umeingia ndani ya Damu ya Watu wa Yemen na Tawi lake ni Kugawanya-Madaraka.
(Imefasiriwa)

Mnamo Jumanne, 05/11/2019, Saleh Al-Khanbashi, akimuwakilisha Hadi, na Nasser Al-Kubaii, akiwakilisha serikali ya mpito, walisaini Mkataba wa Riyadh kumaliza mapigano kati ya vikosi vyao tangu tarehe 2/08/2019. Mkataba huo ni pamoja na kuunda serikali isiyozidi mawaziri 24 na wawe sawa kati ya majimbo ya kaskazini na kusini, na uteuzi wa Hadi wa magavana katika majimbo ya kusini. Pia, kuunganishwa kwa vikosi vya jeshi la serikali na baraza la mpito na kuambatanishwa kwa Wizara ya Ulinzi, pamoja na kupanga upya vikosi vya usalama chini ya uongozi wa Wizara ya Mambo ya ndani, na kurudi kwa vikosi vya jeshi waliohama kutoka nafasi zao ili kushiriki katika mapigano huko Aden, Mkoa wa Abyan na Shabwa, na kuundwa kwa kamati chini ya usimamizi wa Muungano wa Msaada wa Uhalalishaji unaoongozwa na Saudia ili kufuatilia utekelezaji wa makubaliano… Mkataba huo ulitiwa saini baada ya vita ambavyo watu kadhaa waliuawa na mamia walijeruhiwa, na hali bado ni mbaya. Kutiwa saini kwa Mkataba wa Riyadh kulihudhuriwa na Mtoto wa Mfalme wa utawala wa Najdi, Mohammed bin Salman, wakala wa Amerika, na Mohammed bin Zayed, mtiifu kwa Uingereza, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.

Makubaliano haya yanaonyesha ushawishi uliyotolewa na Amerika na wafuasi wake upande wa Falme za Kiarabu, ambazo zinawakilisha Uingereza, kuondoka Yemen, ili wafuasi wa Baraza Kuu la Harakati ya Mapinduzi, mrengo wa Baoum - harakati asili ya mrengo wa Amerika - na wale kama wao waweze kushindana na Hadi na Serikali ya Mpito na wafuasi wao juu ya utawala wa Yemen ya kusini. Kuondoka pia kwa vikosi vya UAE kutoka Yemen ya kusini itasaidia vikosi vya Riyadh kuwezesha kuwasili kwa harakati za Baoum na kuvutia mawakala wa Amerika kuwa sehemu ya utawala wa Yemen ya kusini, kwa sababu Hadi na serikali ya mpito ni mawakala wa Uingereza, na mapigano ambayo yalikua kati yao ni kugonga harakati za Amerika.

Hizb ut Tahrir ilisema katika Jibu la Swali la 13/8/2019 M: "Kulikuwa na Harakati ya Kusini (Al-Hirak) ambayo ilijitangaza rasmi kusini mwa Yemen mnamo 2007 ikiongozwa na mwanaharakati wa upinzaji Hassan Baoum anayehusishwa na Amerika na kuungwa mkono na Iran .... Uingereza iliogopa harakati zake, lakini uoga huu ulifikia kilele chake baada ya kifo cha Salih, ambapo ushawishi wa Uingereza ulipungua baada ya kufanikiwa kwa Mahouthi kupanua ushawishi wao kaskazini. Hivyo basi, ilianza kufikiria sana kuwa na nguvu kusini, kama kadi ya shinikizo ambayo ingeiwezesha iwepo katika utawala wa Yemen, ikiwa haiwezi, angalau kuwa sehemu ya utawala kusini ... Kwa hivyo, ilianza kufikiria sana juu ya kuzingatia ushawishi wake kusini, haswa kwani haikumtegemea kabisa Hadi kwa misingi kwamba Saudi Arabia imemdhibiti. Kwa hivyo, Uingereza ilivutiwa na jambo hili kupitia UAE kupenyeza harakati ya awali ya Kusini au kuipunguza kwa kuunda harakati mpya iongoze kwenye uwanja… na kisha ililenga kupitia UAE na wafuasi wake kupata harakati kusini sambamba na mrengo wa Baoum kuiondoa katika makusudio ya kusini; walipata kile walichokuwa wakitafuta katika Aidarous Al-Zubaidi ..) Mwisho. Leo, Amerika, kupitia bin Salman, anataka kugonga ushawishi wa Uingereza kwa kuleta vibaraka wa Amerika kusini madarakani na

kufanya Hadi na Serikali ya Mpito katika majadiliano na Mahouthi kama sehemu moja na sio pande mbili kama ilivyotarajia Uingereza.

Makubaliano haya yanathibitisha kwamba watawala wa nchi hii na watawala wa nchi za kikanda waliopo katika makubaliano haya ni watumwa wa Makaffiri Wamagharibi, hususan mkoloni wa zamani Uingereza, na Amerika anayetaka kudhibiti nchi hii yote, na kwamba wao (watawala) ni mashahidi wa uongo tu, na wanaoendesha ni Amerika na Uingereza. Makubaliano haya yalifanyika kulingana na mpangilio wa kirasilimali kwa kugawa masuala katika upendeleo ambao vifungu vya Uislamu havikuwa na sehemu.

Nchini Yemen, matumizi ya nguvu kufikia malengo ya kisiasa yamehalalishwa. Waingereza walitumia Baraza la Mpito, na Amerika haikuthubutu kusema neno, kwa sababu walitumia njia ile ile kuleta Mahouthi kudhibiti Sana’a, pamoja na mjumbe wake wa Umoja wa Mataifa Jamal bin Omar.

Tunafahamu kabisa kuwa watu wa Kaskazini na Kusini mwa Yemen wanatamani kuishi chini ya Uislamu, ambao wamenyimwa kwa muda mrefu, na kwa sababu ya watawala wanaotawala na kisichokuwa kile kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu hawakuvuna isipokuwa ugumu wa maisha, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt): 

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً] 

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki” [Ta-Ha: 124].

Sisi katika Hizb ut Tahrir hatupingi suluhisho litakalozuia umwajikaji wa damu baina ya watu wa Aqeeda moja. Tunajua kwa yakini Uislamu unahimiza kufanya suluhu baina ya watu na vikundi, lakini makubaliano haya hayatawatoa watu wa Yemen kutoka katika mateso yao makubwa maadamu viongozi hawa hawahukumu na kile kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu, na maadamu wanajihusisha na adui wa Ummah; Kafiri Mmagharibi na Umoja wa Mataifa, na maadamu Kafiri Mmagharibi anaingilia kati kila mzozo mdogo ama mkubwa ulioko juu ya nchi. Kwa hivyo, Yemen ikibakia hivi, hali itabaki ya mvutano wa vita hadi pale Mwenyezi Mungu atakapoidhinisha kusimamishwa kwa Dola ya Khilafah.

Hizb ut Tahrir inatoa wito kwa watu wa Iman na hekima wa Kaskazini na Kusini na Waislamu wote kufanya kazi na wao kusimamisha Khilafah ya Uongofu ya pili kupitia njia ya Utume ambayo Mwenyezi Mungu ameihahidi na bwana wetu Mtume Muhammad (saw) akapeana bishara njema ya kurudi kwa utawala wa Uislamu ili kuleta haki na kueneza wema, kwa maana leo ulimwengu mzima unakabiliwa na ukosefu wa haki kutoka kwa serikali za kisekula na utaokolewa tu na serikali ya Kiislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema katika Hadith iliyopokelewa na al-Numan bin Bashir, Mwenyezi Mungu amrehemu: 

«...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» 

“Kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume.”

H. 26 Rabi' I 1441
M. : Jumamosi, 23 Novemba 2019

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Yemen

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu