Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  19 Jumada II 1443 Na: Afg. 1443 H / 09
M.  Jumamosi, 22 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kushughulikia Matatizo ya Kiuchumi ya Afghanistan Haiwezekani Bila Utabikishaji wa Kina wa Uchumi wa Kiislamu!
(Imetafsiriwa)

Imarati ya Kiislamu ilifanya Kongamano la Kiuchumi la Afghanistan ambapo wawakilishi wa nchi 20 walihudhuria ana kwa ana huku wengine 40 wakijiunga mtandaoni. Kongamano hili lililenga kutathmini matatizo ya kiuchumi ya Afghanistan katika nyanja tofauti tofauti ili kupata masuluhisho mwafaka ya matatizo hayo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inakadiria nukta zifuatazo ya kuzingatiwa kuhusiana na uchumi wa Afghanistan:

Kwanza: Matatizo ya kisiasa na kiuchumi ya Afghanistan hayawezi kutatuliwa ndani ya mipaka yake ya sasa. Katika karne ya 19, Afghanistan ya kisasa iliundwa na dola kubwa kwa njia ambayo daima iweze kudhibitiwa na kuzitegemea dola hizi. Kwa kutia saini mikataba mbalimbali, wakoloni walisababisha Afghanistan kugeuka kuwa nchi isiyo na bahari, isiyo kufikia njia ya bahari. Kwa sababu hii, Afghanistan chini ya muundo wake wa sasa wa jiografia na utawala haiwezi kuwa huru kisiasa na kiuchumi. Afghanistan itakuwa dola yenye nguvu iwapo tu itaungana na Pakistan na Asia ya Kati. Kuunganisha ardhi za Kiislamu sio tu ni wajibu wa Kiislamu juu ya Waislamu bali pia kutawanufaisha Waislamu wa eneo hilo kijiografia.

Pili: Nidhamu ya kiuchumi ni sehemu muhimu ya mfumo wa Kiislamu. Nidhamu ya kichumi katika Uislamu sio Soko Huria, Ujamaa, mifumo mchanganyiko na mengine yafananayo na hayo, bali ni nidhamu ya kiuchumi tofauti na nidhamu nyengine ambao msingi wake ni imani ya Kiislamu na hukmu za Sharia. Misingi mikuu katika uchumi wa Kiislamu ni ushibishaji wa mahitaji ya kimsingi ya kila mwanadamu, kama vile: chakula, nguo, malazi na mgawanyo wa haki wa rasilimali. Pia ni wajibu wa Dola ya Kiislamu kutoa maisha ya utu kwa kila raia bila kujali ubaguzi wa rangi, kabila na dini. Kwa bahati mbaya, nidhamu ya kiuchumi ya Imarati ya Kiislamu bado ina utata kwani taratibu zake za sasa za kiuchumi zinafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na miundo ya serikali fisadi iliyotangulia. Wakati kusimamishwa kwa Dola halali ya Kiislamu na kutabikishwa kwa uchumi wa Kiislamu ikiwa ni mojawapo ya majukumu muhimu mno ya viongozi wa sasa wanaotawala.

Tatu: Kujenga uchumi imara kunahitaji Imarati hiyo ya Kiislamu kukata mikono ya mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, na Shirika la Biashara Duniani. Waislamu kamwe hawataona ustawi wa kweli katika kuwepo kwa mashirika haya ya kikoloni. Ingawa mashirika haya yanahalalisha uwepo wao chini ya kivuli cha misaada ya kibinadamu, hakika ni jukumu la serikali kupanga mambo ya watu na kutatua shida zao, sio za mashirika ya kimataifa. Uendeshaji wa mashirika ya kimataifa, kwa upande mmoja, unasababisha uhalali wa Imarati ya Kiislamu kutiliwa shaka [na kuifanya ionekane kuwa haina uwezo wa kutatua matatizo ya watu], na kwa upande mwingine, inapelekea kuundwa kwa muundo sambamba ndani ya serikali, kushughulikia mahitaji ya watu. Hata hivyo, ukweli ulio wazi ni kwamba taasisi hizi za kimataifa na/au mashirika ni silaha zenye nguvu na vile vile silaha laini za wakoloni wa Magharibi zinazowasaidia kutekeleza malengo yao ya kikoloni kupitia vile vinavyoonekana kuwa ni vifurushi vya msaada wa kibinadamu.

Nne: Uislamu unaharamisha dola ya Kiislamu kuwa tegemezi kisiasa na kiuchumi kwa nchi nyingine. Kwa hivyo, imejihami na sera za kujitegemea na za ustawi wa kiviwanda ili kushughulikia matatizo makuu ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje na utegemezi kwa wageni. Sera hii ya kiviwanda imeegemezwa kwenye Jihad na kuendeleza kupanua ulinganizi wa Uislamu. Bila shaka, ili kupata sera za kujitegemea na bidhaa za viwanda, kuna haja kubwa ya miundombinu ya elimu, mipango ya mafunzo ya kiufundi na fursa za utafiti. Kwa sasa, Afghanistan na eneo hili lina hifadhi nyingi za asili na nguvu kazi changa ambayo inasaidia kuwezesha sera ya viwanda. Sera kama hiyo pia itaokoa serikali hii kutoka kwa uchumi unaotegemea ushuru, ikiondoa mzigo wa shinikizo kutoka kwa watu masikini pia.

Tano: Sarafu katika Uislamu imeambatanishwa na kipimo cha dhahabu. Dola ya Kiislamu lazima ichapishe noti kulingana na utajiri wake halisi, ambao ni dhahabu na fedha. Sababu yake ni kwamba hukmu za Sharia za Uislamu zimebainisha dhahabu fedha pekee kuwa ndio kipimo pekee cha sarafu. Mwenyezi Mungu (swt) ameamua tu dhahabu na fedha itumike kama kiwango [Nisab] cha Zakat. Kwa sasa, sarafu ya Afghanistan imeambatanishwa na dolari ya Marekani. Hii sio tu imefanya uchumi wa Afghanistan kuwa tegemezi kwa Amerika na Magharibi, lakini pia imesababisha mfumko wa bei na kuyumba kwa sarafu ya Afghanistan.

Tunawahimiza kukamata nidhamu ya kiuchumi na sera zinazotokana na vyanzo vya Sharia, ambazo, kwa upande mmoja zitapelekea radhi za Mwenyezi Mungu (swt), na kwa upande mwingine, zitashughulikia matatizo ya kiuchumi yaliyopo.

 [وَعَسَى أَن تَكْرَهُواْ شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَعَسَى أَن تُحِبُّواْ شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ وَاللّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ]

“Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [Al-Baqara: 216].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu