Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  18 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445 / 30
M.  Jumatatu, 24 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mtazamo wa Serikali Tawala katika Uchimbaji Migodi Unaziimarisha Dola Adui (Muharib) na Kuwadhoofisha Waislamu wa Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Wizara ya Madini na Petroli ya Afghanistan imetangaza kuwa katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, zaidi ya dolari bilioni saba zimewekezwa katika sekta ya madini nchini Afghanistan. Katika mchakato huu, kando na makampuni ya ndani, makampuni kutoka Qatar, Uturuki, Urusi, Iran, China na Uingereza pia yamechukua dori kubwa. Huu unachukuliwa kuwa uwekezaji mkubwa zaidi katika uchimbaji madini katika historia ya Afghanistan.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inaona mambo nyeti yafuatayo kuhusu suala hili kuwa ni muhimu kuangaliwa:

Kwanza, migodi ya Afghanistan ni mali ya umma. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ»“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto.” Katika Hadith hii, neno “moto” linakusudiwa kuwa nishati, kawi na viambajengo vyake. Hivyo basi, Shariah imeruhusu watu wote katika jamii kufaidika na mali ya umma. Kwa mfano, Waislamu wote wana hisa katika mafuta ya Saudi Arabia, gesi ya Qatar, na migodi ya Afghanistan. Kwa hiyo, utawala wowote unaodhibiti migodi ya Umma wa Kiislamu unawajibika kuendelea na uchimbaji na utumiaji kwa kuzingatia kanuni za Shariah. Kanuni ya Shariah inaelekeza kwamba migodi isitumike kama chanzo cha mapato kwa bajeti ya kawaida na ya maendeleo ya serikali, isipokuwa kwa sehemu zinazohusu ustawi wa pamoja wa Waislamu. Zaidi ya hayo, hairuhusiwi kwa mtazamo wa Shariah kukabidhi migodi mikubwa na ya kimkakati kwa makampuni binafsi. Badala yake, dola ya Kiislamu inawajibika kwa uchimbaji wa migodi kwa niaba ya watu, na faida inayopatikana kutoka kwayo inapaswa kutumika kikamilifu kwa ustawi wa umma na huduma za umma. Hukmu hii inatumika kwa aina zote za mali ya umma, iwe inahusisha uchimbaji madini, utoaji, uboreshaji, uzalishaji, au ugawanyaji. Kwa hiyo, mchakato wa sasa wa kutoa kandarasi ya migodi mikubwa na ya kimkakati kwa makampuni binafsi ni utaratibu usio halali na uliojaa matokeo hatari kisiasa.

Pili, Afghanistan ni ardhi yenye utajiri wa maliasili tofauti tofauti za thamani. Hivi sasa, China, Urusi na Marekani sio tu zimekuwa zikimezea mate maliasili za Afghanistan bali pia zinajitahidi ima kuinyonya migodi hii kwa manufaa yao binafsi au kuwazuia wapinzani wao kuingia kwenye migodi ya kimkakati ya Afghanistan. Zaidi ya hayo, nchi hizi hutumia makampuni ya uchimbaji madini kama pazia ili kuendeleza malengo yao ya kisiasa na kijasusi. Kwa kuwa uchimbaji wa migodi ya Afghanistan unaweza kucheza dori kubwa katika mpito wa kawi duniani na mchakato wa uzalishaji wa vipuri vidogo, dola kubwa zinakodolea macho migodi ya kimkakati ya Afghanistan na mchakato wa kupata vitu adimu. Kupata mwanya wa ufikiaji haya kunaweza kulemeza mizani katika mchezo wa kimataifa wa siasa za kijiografia upande wa mojawapo wa dola hizo. Kwa hivyo, ni muhimu kwa watawala kusimamia migodi ya Afghanistan kwa njia ambayo haiimarishi uchumi na viwanda vya dola adui.

Tatu, mchakato wa sasa wa utafutaji, uchimbaji, usafishaji na kuzipiga mnada rasilimali za madini hauna utaratibu wa uwazi na mshikamano, na baadhi ya maafisa wenye ushawishi katika serikali inayotawala wana mchango mkubwa katika mikataba na unyonyaji. Kuendelea na mchakato huu kumeiweka Afghanistan kwenye “laana ya rasilimali,” na kuigeuza kuwa njia ya migogoro ya kisiasa na ushindani kati ya nchi za kigeni na vikundi vya ndani. “Laana ya rasilimali” ni hali ambapo badala ya ukuaji wa uchumi na utulivu, rasilimali za madini husababisha umaskini, taabu na vurugu. Ishara za mienendo hii hatari tayari zinaonekana. Hata kama serikali inayotawala itapata mabilioni ya dolari kutokana na uchimbaji madini, bado haitaweza kubadilika na kuwa dola tajiri na yenye natija lakini itabaki kuwa dola utumiaji fedha nyingi.

Nne, uzoefu wa nchi unaonyesha kuwa ubadhirifu wa rasilimali za madini hufungua njia ya kukosekana kwa utulivu.

Afghanistan inaweza tu kukwepa "laana ya rasilimalir" kupitia mfumo unaosimamia rasilimali za madini kwa msingi wa fikra na hukmu za Kiislamu, kama anavyosema Mwenyezi Mungu kuhusiana na umuhimu na matumizi ya rasilimali za madini:

[وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ]

“Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.” [Al-Hadid:25].

Kwa kutafakari aya hii tukufu, inadhihirika wazi kwamba kwa mtazamo wa Uislamu, rasilimali ya madini inapaswa kutumika kwa malengo mawili ya msingi. 1) kutumia madini kwa ajili ya uhamasishaji wa silaha kutoa Nusrah (utekelezaji na ulinganizi) wa Dini ya Mwenyezi Mungu na 2) kutumia madini kukidhi mahitaji na manufaa ya binadamu.

Kwa hiyo, jitihada zozote za kuchimba na kutumia madini ambazo hazijaegemezwa kwenye hukmu za Shariah, uchamungu, na utambuzi wa kina wa kisiasa hazitasaidia kupata ustawi wa watu bali zitakuwa ni njia ya kutokuwa na utulivu na ushawishi wa nchi zenye nguvu. Huku rasilimali za madini zikiwa ni neema ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameijaalia taifa; hivyo, rasilimali hizi zinapaswa kutumika ipasavyo na kihalali kwa manufaa ya watu, na muhimu zaidi, kuweka msingi wa dola ya kiviwanda yenye teknolojia ya juu ya kijeshi yenye lengo la kutabikisha kikamilifu Uislamu na kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa mataifa mengine kupitia njia ya Dawah na Jihad.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu