Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 29 Sha'aban 1445 | Na: 027 / 1445 H |
M. Jumapili, 10 Machi 2024 |
Tangazo la Matokeo ya Kuuangalia Mwezi Mwandamo wa Ramadhan 1445 H
(Imetafsiriwa)
Bismillah Al-Rahman Al-Rahim wa Alhamdulillah Rabb Alameen na rehma na amani zimshukie mjumbe ambaye ni rehma kwa walimwengu wote bwana wetu Muhammad na jamaa na maswahaba zake wote.
Amepokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad kwamba alisema, “Nilimsikia Abu Hurairah (ra) akisema: kwamba Mtume (saw) amesema, au alisema: Abu Al-Qasim (saw) amesema: «صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فأَكْمِلُوا عِدَّةَ شعبانَ ثلاثين» “Fungeni kwa kuuona (mwezi mwandamo) na fungueni kwa kuuona. Lakini ikiwa (kutokana na kutanda kwa mawingu) muonekano wa mwezi utafichika kwenu, basi kamilisheni siku thalathini za Sha’aban.””
Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mkesha huu wa Jumatatu, muandamo wa mwezi mpya kwa mujibu wa matakwa ya Shariah unathibitishwa, na kwa hiyo kesho, Jumatatu ni siku ya kwanza ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1445 H.
Kwa mnasaba huu, nafikisha salamu na pongezi zangu za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wote wanaofanya kazi humo, kwa Amir wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, nikimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie na aharakishe ushindi kwetu na tamkini kupitia mikono yake.
Mwaka huu, Ramadhan inakuja huku ulimwengu ukishuhudia mapambano yanaoendelea kati ya utashi wa Umma wa Kiislamu wa kushikamana na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na utashi wa mkoloni wa Kafiri wa Kimagharibi kupandikiza umbile vamizi la Mayahudi kwenye Ardhi hiyo Iliyobarikiwa kama kiambatanisho. Mapambano hayo yameishughulisha dunia nzima, na hakuna mazungumzo ya kisiasa kwenye jukwaa lolote yanayopita bila swali kuulizwa kwa mmiliki wake: unaunga mkono upande gani? Mapambano hayo yamefichua masuala kadhaa ambayo ni lazima yakomeshwe ili kuelewa mahali ulipo Umma wa Kiislamu.
Imebainika kuwa mchakato wa uhalalishaji mahusiano umefeli tangu kuanzishwa kwake. Mazungumzo yote yaliyojaribiwa na vyombo vya habari vilivyofadhiliwa kuonyesha wazo kwamba Umma wa Kiislamu umeanza kuikubali fikra ya umbile la Kiyahudi haikuwa chochote ila uongo kutoka kwa watawala kwenda kwa watu. Watawala hawa si chochote ila ni mabaki duni yanayosibu kila jamii ya wanadamu. Watawala wetu wamewaendea tu wahaini ambao ni wa aina yao.
Imethibitika kwa Umma wa Kiislamu kwamba majeshi yana dori muhimu katika kutatua masuala yake. Baada ya Umma wa Kiislamu kujihusisha na Mambinduzi ya Kiarabu dhidi ya watawala bila ya kutilia maanani dori ya majeshi ipasavyo, leo unawaita, "Mko wapi enyi majeshi ya Kiislamu? Kwa nini hamjitayarishi kuinusuru Gaza?" Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hii inatangaza chemchemi mpya ya mapinduzi, lakini wakati huu ni "Chemchemi ya Mapinduzi ya Majeshi ya Kiislamu" ambapo majeshi ya Kiislamu yanatoka kwenye kambi zao na kunyoosha mikono yao kwa Umma wa Kiislamu kwa kuunusuru na kuinusuru Dini yake. Ama kuhusu watawala wasaliti, hatutawataja kwa urefu katika suala hili. Wananuka uvundo katika vita hivi katika hali amabyo hawajawahi kunuka hapo mbeleni na Ummah hauwavumilii tena, unangoja kwa hamu kujiondoa kutokana nao kwa fursa iliyo karibu zaidi.
Vile vile, Umma wa Kiislamu umehisi uzito wa njama ya kuzigawanya ardhi za Waislamu. Vijana wa Umma wa Kiislamu walijaribu kuandamana hadi Palestina kutoka nchi kadhaa, lakini mipaka iliyochorwa na Makubaliano ya Sykes-Picot iliwazuia kufika kwenye Ardhi Iliyobarikiwa. Wengi wametambua kwamba mipaka hii ilichorwa tu ili kutumika kama jela inayozuia Umma wa Kiislamu kuja kujisaidia wenyewe.
Ama watu wa Gaza Hashem, wanyonge wao, wakiwemo watoto, wanawake na wazee, wameonyesha mandhari ya subira na uthabiti katika kukabiliana na dhiki, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu zaidi kwa kiwango kilichoandikwa na mashujaa wao kupitia mandhari za ukakamavu na ujasiri, wakijitahidi kulifanya duni neno la walio kufuru. Hivyo, watu wa Ghaza wameondoa vumbi kutoka kwenye njia iliyonyooka inayotoka katika Uislamu, ikijumuisha Muumini wa Kiislamu anayetafuta yaliyo kwa Mwenyezi Mungu juu ya mambo yote ya kidunia, na mujahidina vijana ambao hawapepesi macho mpaka wawashinde maadui zao. Kati ya yule anayesema kwa furaha, "Kifaru kinawaka moto!" na mzee mtulivu na aliyeridhika anayebusu macho ya “nafsi ya nafsi,” watu wa Gaza wameupa moyo ulimwengu kwamba hakika Uislamu ni kitu adhimu.
Enyi Waislamu:
Hisia zinaamshwa, picha iko wazi, na mafikio yanajulikana; kuhamasishwa kwa majeshi, kuondolewa kwa watawala na kuvunjwa kwa mipaka. Msiache mihanga ya watu wa Gaza iende bure, msiache Mwezi Mtukufu upite bila kumaliza njama ya Sykes-Picot na kusimamisha tena Khilafah Rashida. Katika historia, Khilafah imekuwa njia ya kivitendo ya kuunganisha nguvu za Waislamu. Ni mfumo wa kisiasa ambao Umma wa Kiislamu ulifanya kazi ili kufikia maslahi yake na kuwashinda maadui zake. Siku zimethibiti kwenu kwamba mfumo wowote wa kisiasa usiokuwa wa Khilafah unaleta aibu, fedheha, hasara na udhalilifu tu kwa Waislamu. Ukombozi wa Palestina unahitaji ukombozi wa ardhi za Waislamu kutoka kwenye mipaka ya Sykes-Picot, na ni majeshi ya Waislamu pekee ndiyo yanayoweza kufanya hivyo, kwani wao ndio wenye uwezo wa kweli katika ardhi zetu, na ni watoto wenu, basi wahamasisheni na kuwashajiisha ili kusimamisha Khilafah kwa sifa.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
[وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَسَى اللهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُواْ وَاللهُ أَشَدُّ بَأْساً وَأَشَدُّ تَنكِيلاً]
“Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulio ya walio kufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu.”[An-Nisa:84].
Mkesha wa Jumatatu ndio tarehe mosi ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan wa mwaka 1445 H.
Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |