Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 12 Rabi' I 1446 | Na: H 1446 / 023 |
M. Jumapili, 15 Septemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Udungaji Visu Mgongoni mwa Umma Unaendelea kutoka kwa Watawala Vibaraka Ruwaibidha wa Waislamu!
(Imetafsiriwa)
Ufalme wa Al Saud unaregesha udungaji visu wake mgongoni mwa Umma wa Kiislamu kwa kushirikiana na watawala wa Ruwaibidha (watepetevu na wazembe) katika nchi za Kiislamu kupitia mbio zao za kuhalalisha mahusiano na umbile nyakuzi, licha ya jinai zote za mauaji ya halaiki na uhangaishaji Waislamu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaofanywa na umbile hilo katili. Balozi wa Saudia nchini Marekani, Reema bint Bandar Al Saud, alihudhuria Mkutano wa Kilele wa Mazungumzo wa Amerika na Mashariki ya Kati katika mji mkuu wa Marekani, Washington, katika halfa iliyosifiwa na magazeti ya umbile la Kiyahudi kama “isiyo na kifani”, kwani baadhi ya maafisa wakuu kutoka kwa umbile lao walishiriki katika halfa hiyo hiyo, na mabalozi wa Morocco na Bahrain nchini Marekani walishiriki katika mkutano huo uliotajwa. Tovuti rasmi ya Mkutano wa Kilele wa Mazungumzo ya Amerika na Mashariki ya Kati (MEAD) inasema kwamba “imesimama mstari wa mbele katika kukuza mazungumzo muhimu kati ya Marekani na Mashariki ya Kati. Mkutano wetu wa kila mwaka huwaleta pamoja viongozi kutoka kanda zote mbili ili kuimarisha ushirikiano na kuunda sera za siku zijazo.”
Hatua hizi kwa hakika zinatumikia mbio za vibaraka hawa kwa kile wanachokiita “mkataba wa uhalalishaji mahusiano”, kana kwamba ardhi ya Palestina na watu wake ni bidhaa ya bei nafuu ambayo Ruwaibidha wanafanya biashara kwayo katika vilabu vyao kwa bei rahisi, bali pasi na bei yoyote! Hivi ndivyo vyombo vya habari vya umbile hilo viliripoti kutoka kwa afisa mmoja mkuu, ambaye alitabiri uwezekano wa kuhitimisha makubaliano ya kuhalalisha mahusiano kati ya Saudi Arabia na umbile la Kiyahudi katika kipindi cha kati ya kuanza kwa uchaguzi wa Marekani mnamo Novemba na kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani mnamo Januari 20, huku akisisitiza kuwa hii “inahitaji kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, na ruwaza kuhusu kutatua kadhia ya Palestina.” Badala ya kuliondolea mbali umbile nyakuzi la Kiyahudi, inatoa amani na usalama; hivi ndivyo balozi wa Saudia alivyothibitisha katika taarifa yake ya awali wakati wa Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos, mnamo Januari 2024, ambapo alisema katika mahojiano yake na Becky Anderson, mtangazaji wa CNN: Saudi Arabia “inatambua kikamilifu haja ya ‘Israeli’ kujisikia salama, haiwezi kuwa kwa gharama ya watu wa Palestina.” Kauli hii yenyewe inathibitisha khiyana kubwa iliyofanywa na watawala wa Al Saud ambao wamejitolea kuwatumikia Mayahudi, na hata kuwapa uungwaji mkono wa kisiasa na kiuchumi ili kuendeleza dhulma na ukandamizaji wao dhidi ya Waislamu nchini Palestina.
Kwa kuzingatia kile ambacho Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken alichosema katika mkutano na waandishi wa habari nchini Haiti: kwamba “bado ana matumaini” kuhitimisha makubaliano ya uhalalishaji mahusiano kati ya umbile la Kiyahudi na Saudi Arabia kabla ya mwisho wa muhula wa Rais wa Marekani Joe Biden Januari 2025. Tunaelewa pale ambapo upepo huu wa sumu unatokea na tunajua nani anaendesha sera hii ya kifisadi. Marekani inadhamiria kutafuta kufikia makubaliano ambayo Saudi Arabia italitambua umbile la Kiyahudi (hadharani), kwa badali ya kuanzisha uhusiano imara wa usalama kati ya Riyadh na Washington, na kutoa usaidizi wa Marekani kwa mpango wa nyuklia wa raia wa Saudi ambao una uwezo wa kurutubisha urani. Amerika inaushikilia mateka utulivu wa ufalme wa Saud mikononi mwake, na gharama yake ni kuhalalisha mahusiano na umbile hilo, kama ilivyofanya hapo awali kwa Imarati, Bahrain, na Morocco, na njia inaandaliwa hivi karibuni kwa Sudan kutangaza uhalalishaji wake wa mahusiano haya vilevile.
Tukirudi kwa taarifa za balozi kuhusu eneo hilo pana, Binti Mfalme Reema bint Bandar alisema: “Lakini kadiri hii inavyoendelea, ni jambo lisiloepukika kwamba aidha umbile jeuri au kosa litatokea ambalo litaturudisha nyuma. Na sipendi kusema hivyo, lakini litaturudisha kwenye Zama za Kale. Ni eneo lenye moto na tete, eneo langu la dunia.” Anatambua kwamba endapo eneo hilo linaloungua litalipuka, litateketeza vyombo vyao na kumaliza mamlaka yao, na hili halitatokana na “umbo jeuri” kama anavyolielezea, bali ni kupitia dola thabiti inayoregesha mamlaka ya Ummah na ubwana ndani yake ni kwa ajili ya Sharia ya haki na imejengwa juu ya Aqida (itikadi) iliyopachikwa ya Ummah. Hii ni Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na sio kuregea kwenye Zama za Kale. Bali ni kuuamsha Ummah kutoka katika usingizi wake, ili uinuke kutoka katika kurudi nyuma kwake, ukukute vumbi la udhaifu, na ufanye jihad ya kuzikomboa ardhi na watu wake, kung'oa maumbile yote haya maovu na serikali zinazokula njama, na kumaliza dhulma, na kuwaondoa madhalimu. Haya ndiyo wanayoyahofia Wamagharibi, vibaraka wake na washirika wake katika eneo, kwa sababu Dola ya Khilafah haitakubali udhalilishaji na udunishaji ambao Magharibi imeufanya kupitia watawala wake Ruwaibidha ambao waliuza ardhi na heshima zao kwa badali ya viti vibovu vya utawala na mamlaka zilizopitwa na wakati.
Tunawatahadharisha vibaraka hawa kwa yale aliyoyasema Mola Mlezi Mtukufu katika Surat Al-Ma’idah:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]
“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma’idah 5:51].
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |