Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 032
M.  Jumamosi, 05 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Hajui Historia ya Nchi Yake!
(Imetafsiriwa)

Ni moja ya mambo ya ajabu, na ya kushangaza sana, kwamba waziri katika nchi ambayo ilikuwa kubwa kwa muda mrefu hajui historia ya nchi yake, kuelezea hisia zake za mshangao na hasira kwa madhihirisho ya kusherehekea kurushwa makombora dhidi ya umbile la Kiyahudi.

Serikali ya Ujerumani na mawaziri wake wamesahau jinsi walivyowatendea Mayahudi kabla ya Vita vya Pili vya Dunia; waliwazuia madaktari wao kuwatibu Aryans kufikia Septemba 1938. Mnamo Agosti 1938, mamlaka za Ujerumani zilitoa taarifa kwamba kufikia Januari 1, 1939, kila mwanamume na mwanamke Myahudi ambaye hakuwa na jina la Kiyahudi lazima aongeze jina 'Israel' au 'Sara' kwa majina yao, ili kuwatofautisha na watu wengine.

Serikali ya Ujerumani na mawaziri wake wamesahau muungano wao na Waislamu, walipotia saini makubaliano ya muungano na Khilafah Uthmani mnamo Agosti 2, 1914, pamoja na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi wa Ujerumani nayo.

Ingawa asilimia ya Mayahudi nchini Ujerumani ni chini ya mara ishirini ya asilimia ya Waislamu, sera ya Ujerumani inafuata njia ya dhulma dhidi ya Waislamu, ikitoa kauli za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, na kauli zinazounga mkono umbile la Kiyahudi lililonyakua ardhi ya Waislamu, Palestina!

Inaonekana kwamba waziri huyo aliyetajwa hapo juu anaongeza ujinga wa kisiasa kwenye ujinga wake wa kihistoria, kwani huenda asiwe anajua ukweli kuhusu utawala wa Iran na mzunguko wake pambizoni mwa Amerika, na hajui kuwa sio tishio kwa umbile la Kiyahudi. kama ilivyo kwa Ulaya, ikiwemo Ujerumani. Huenda asijue kuwa Amerika inatumia faili ya nyuklia ya Iran kama kisingizio dhidi ya Ulaya na makampuni yake.

Kauli za hivi punde za waziri huyo zinaelezea hofu kubwa iliyojaa nyoyoni mwa viongozi wa nchi za Magharibi baada ya Oktoba 7, 2023 na matukio yaliyofuata. Kwa vile umbile la Kiyahudi lilivyokabiliwa na tishio lililokuwepo, na lilibeba ujumbe kwa viongozi wa Magharibi kwamba utawala wenu duniani na katika nchi za Kiislamu si wa milele, na wakati wa utawala huu kukomeshwa umekaribia. Waziri huyo alionyesha hisia zake za ndani kuhusiana na kile alichokiona cha Waislamu kusherehekea kurushwa kwa makombora ya Iran - hata ikiwa ni matupu - kwenye umbile la Kiyahudi, basi ingekuwaje kama makombora haya yangekuwa ya kweli, na yamejaa milipuko ambayo husababisha uharibifu mkubwa kwa vifaa vya umbile la Kiyahudi?

Serikali ya Ujerumani na mawaziri wake walipaswa kufikiria kuhusu nchi yao; na kuona kwamba baada ya wao kuwa nchi kubwa, sasa wanaongozwa na Amerika, kama vile watawala vibaraka wa ulimwengu wanavyoongozwa na Amerika. Wakumbuke kwamba Marekani iliwaongoza kwenye vita dhidi ya Waislamu nchini Iraq mwaka 1991, na kuwaongoza kwenye vita dhidi ya Waislamu nchini Afghanistan mwaka 2001, kisha Marekani ikajitoa katika nchi zote mbili. Ilipojiondoa Afghanistan mnamo 2021, haikuwaarifu washirika wake mapema!

Leo, Ujerumani, kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Ndani, inaelezea kushangazwa na hasira yake. Tunamwambia yeye na serikali ya Ujerumani iliyo nyuma yake: Waislamu hawatasahau kauli hii ya Ujerumani, wala hawatasahau ushiriki wake katika kupigana na Waislamu zaidi ya mara moja - kama waziri huyo alivyosahau historia ya nchi yake - na Dola ya Khilafah iko karibu mno, Mwenyezi Mungu akipenda, kisha Waislamu watakujibisha kwa misimamo yako yote dhidi yao, ukandamizaji wako kwao katika nchi yako, na kauli zako za uadui dhidi yao. Kisha hutakuwa na wakati wa kuonyesha hasira au mshangao, na utajuta, lakini hakutakuwa na wakati wa majuto.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu