Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 20 Rabi' II 1446 | Na: H 1446 / 041 |
M. Jumatano, 23 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuanguka kwa Kile Kilichosalia cha Jani la Mtini Lililochakaa ambalo Hadhara ya Magharibi Inafikiri Inaficha Aibu Yake!
(Imetafsiriwa)
Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu katika ardhi za Palestina, Francesca Albanese alisema: “(Israel) inafanya mauaji ya kutisha ya halaiki mjini Gaza na kuwachinja Wapalestina kila siku kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi.” Albanese alieleza katika mahojiano na Al Jazeera kwamba (“mauaji ya halaiki ni uhalifu mkubwa unaopaswa kutushtua. Katika miezi kadhaa iliyopita, nimerudia katika mamia ya mahojiano kwamba mauaji ya halaiki yanayofanywa na (Israel) ni ya kutisha na ya mabaya, na sielewa kwa nini yaendelea mpaka sasa.” Aliuliza, “Itahitaji nini hadi kukomesha janga hili?” kabla ya kuthibitisha kwamba yale yanayotokea Gaza yamethibitisha mwisho wa mfumo wa dunia ulioundwa baada ya Vita Kuu vya II vya Dunia. Aliongeza, “Mfumo huu wa dunia unaonyesha sura yake halisi kama kundi la kikoloni la nchi za Magharibi zinazoendelea kuunga mkono (Israel) na kudai kuwa inajilinda, na sivyo (Israel) sasa inawachinja Wapalestina Gaza. Kile munachokiona ni watoto mjini Gaza wanauwawa barabarani, na watu kuchomwa kwenye mahema.” Albanese alihitimisha hotuba yake kwa kuthibitisha kwamba kinachotokea Gaza ni “mauaji ya halaiki kwa lengo la kudhibiti ardhi, na hivi ndivyo (Waisraeli) wenyewe wanavyosema”).
Katika muktadha huu, ripoti moja ilichapishwa katika Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 19, 2024, kuhusu “kufuatilia kupigwa marufuku kwa maandamano katika vyuo vikuu vya Marekani na vikwazo vilivyowekwa na nchi za Ulaya.” Demokrasia za Magharibi, yaani Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani na Ubelgiji zilituhumiwa katika Umoja wa Mataifa kwa kukandamiza vikali haki ya kuandamana kwa ajili ya kadhia ya Palestina, hasa mwanzoni mwa vita katika Ukanda wa Gaza. Ripoti hiyo ilizungumzia kuhusu “maandamano yaliyokandamizwa vikali katika vyuo vikuu nchini Marekani,” ikimaanisha kuingilia kati kwa polisi wa kutuliza ghasia jijini New York mwishoni mwa Aprili 2024 kuwafukuza wanaharakati kadhaa wanaounga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia. Ama kuhusu nchi za Ulaya, ripoti hiyo ilitaja haswa “Ujerumani, ambayo iliweka marufuku kamili ya maandamano ya Wapalestina mnamo Oktoba 2023, na tangu wakati huo imeweka vizuizi kwa maandamano kama hayo katika maeneo mbali mbali ya Ujerumani,” na kuongeza kuwa vizuizi hivi “havikuwekwa kamwe kwa maandamano yanayounga mkono (Israel), lakini daima kwa wale wanaounga mkono Wapalestina.” Iliongeza kuwa “Ufaransa ilijaribu kuchukua hatua sawa, lakini mahakama ilizikataa, na tathmini sasa inafanywa kwa msingi wa kesi kwa kesi,” ikibainisha kuwa “Ubelgiji na Canada zimepitisha misimamo sawa”.
Mfano wa kutokuamini kwa kiongozi wa ulimwengu wa Magharibi Amerika katika uhuru wa kujieleza, ambayo imekuwa ikiendesha vita nje ya nchi, ni wakati polisi wa Amerika walipowakamata zaidi ya waandamanaji 200 wanaounga mkono Palestina baada ya kupanga kuketi nje ya Soko la Hisa la New York mnamo Oktoba 15, 2024, kutaka kukomesha uungaji mkono wa Marekani kwa vita vya umbile la Kiyahudi dhidi ya Gaza. Waandamanaji waliimba kauli mbiu za kibinadamu kama vile “Iwacheni Gaza iishi” na “Komesheni ufadhili wa mauaji ya halaiki” mbele ya jengo maarufu la soko la hisa karibu na Wall Street huko Manhattan. Kinyume chake, kulikuwa na idadi ndogo ya waandamanaji wanaounga mkono umbile la Kiyahudi kwenye eneo hilo, ambao waliinua bendera yake, na hawakuchukuliwa hatua yoyote na polisi.
Hili ni ombi kutoka kwa mawakili na wanaharakati wa haki za binadamu kutoka kambi ya Magharibi, na huu ni ushahidi wa sauti na picha, unaothibitisha kwamba hadhara ya Magharibi na nchi zinazoegemezwa juu yake, hususan nchi zinazoongoza za ulimwengu wa Magharibi, Marekani, Ufaransa na Ujerumani, zinaanguka kwa kile kilichobakia cha jani la mtini ambacho nchi za Magharibi zilidhani kuwa zinaficha aibu yake, kwani hali ya nchi za Magharibi imefikia mahali ambapo haijaridhika na kulipa umbile la wale waliolaaniwa silaha za kuua watu na mawe, bali kwa kumkandamiza kila mwenye kukanusha ukatili huu, na huu ndio msumari wa mwisho uliopigiliwa kwenye jeneza la hadhara ya Magharibi, na kilichobakia pekee kwa watu duniani, ukiwemo Umma wa Kiislamu, ni kuizika maiti hii inayonuka, ili wanadamu wapumzike kutokana na maovu yake na wale wanaoiendesha.
Kazi ya kulizika zimwi hili ni wajibu kwa Umma wa Kiislamu, kwani ndio mmiliki wa hadhara badali iliyostaarabika ambayo inaweza kwa sifa zote kuuendeleza wanadamu kwa maadili ya kibinadamu ambayo Mwenyezi Mungu amewachagulia watu wote. Umma lazima uasisi chombo cha kisiasa ambacho kinawakilisha hadhara ya kimungu ya Kiislamu ambacho, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, itaiondoa batili na kuipa ushinda haki. Hivyo basi, watu wote wenye ikhlasi katika Ummah lazima wafanye kazi ya kusimamisha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume kwa kuyataka majeshi ya Waislamu kukata mikono ya Magharibi katika nchi zetu; tawala zilizopo humo, na kuinusuru Hizb ut Tahrir ili kuisimamisha, ili itimie kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) isemayo: «وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye” Imesimuliwa na Bukhari.
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |