Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 10 Dhu al-Hijjah 1440 | Na: 1440 H / 042 |
M. Jumamosi, 10 Agosti 2019 |
Risala ya Kheri kutoka kwa Hizb ut Tahrir kwa Sikukuu ya Idd ul-Adha
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd
(Imetafsiriwa)
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Al-Rahman Al-Rahim… Sifa njema zote ni kwa Allah na rehema na amani zimshukie mtukufu zaidi wa Mitume ya Mwenyezi Mungu, aliye tumilizwa kama rehma kwa walimwengu wote, bwana wetu, bwana wa viumbe vyote na mtume wa mwisho Mtume Muhammad (saw) na kwa mababu zake, baba wa Mitume, Ibrahim na juu ya bwana wetu Ismail, Mtume aliye tolewa kama sadaka, na juu ya familia ya Muhammad (saw) na maswahaba zake wote.
Al-Bayhaqi amevua kutoka katika As-Sunan Al-Kubra kutoka kwa Saeed ibn Jubair kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume (saw) amesema:
«مَا الْعَمَلُ فِي أَيَّامٍ أَفْضَلُ مِنْهُ فِي عَشْرِ ذِي الْحِجَّةِ. قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ؟ قَالَ: وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ ثُمَّ لَا يَرْجِعُ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ» “Hakuna amali bora katika siku kushinda ile inayofanywa katika (siku kumi za mwanzo za Dhul Hijjah). Maswahaba wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume akasema: Hata Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake kisha kusirudi chochote katika hivyo.”
Idd ul-Adha iliyo barikiwa imewadia, siku ya kusherehekea kwa waumini kwa kukamilisha utiifu wao katika siku kumi hizi. Kwa hivyo pongezi kwa wale waliohiji katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu na pongezi kwa wale walio ongeza utiifu katika siku kumi hizi.
Katika sikukuu hii ya Idd ul-Adha iliyo barikiwa, Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Mwenyezi Mungu amuhifadhi, anawapa pongezi vijana na mabinti wote wa Ummah huu mtukufu wa Kiislamu kwa risala ifuatayo:
بسم الله الرحمن الرحيم
Sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na juu ya jamaa na maswahaba zake, na wale wanaomfuata, ama baada yao.
Kwa Ummah mtukufu wa Kiislamu, kwa mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, kwa wabebaji Da’wah watukufu, kwa waheshimiwa wanaozuru ukurasa wa Facebook,
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh, Mwenyezi Mungu aukubali utiifu wenu, na Mwenyezi Mungu aifanye Idd yenu ijae kheri na baraka. Mwenyezi Mungu aikubali Hajj ya waliohiji, na Mwenyezi Mungu aifanye iwe Hajj iliyo kubaliwa, na juhudi zilizo pokewa na dhambi zilizo samehewa. Pia namuomba Mwenyezi Mungu (swt) awape tawfiq wale ambao hawakuhiji mwaka huu wahiji mwakani kwa kheri juu ya kheri.
Kaka zangu na dada zangu waheshimiwa, tunamtukuza kwa Takbir na tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa neema ya Uislamu, na tunamtukuza na kumsifu Yeye (swt) kwa neema ya ubebaji da’wah hii pamoja na swafu za Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah. Tunamtukuza na kumsifu Yeye Subhanahu wa Ta’ala kwamba chama hiki kimesimama imara licha ya njama za wakoloni na vibaraka wao, watawala wa biladi za Waislamu, na licha ya khiyana za wanafiki, ambao nyoyo zao zinaugua na wazushi. Hakika, tunamtukuza Mwenyezi Mungu kwa Takbir: Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd.
Khilafah, ambayo Hizb ut Tahrir inaisaka, inawakesheza usiku kucha wakoloni makafiri, na kuwaogofya vibaraka wao watawala katika biladi za Waislamu, na kuwatia dhiki wanafiki na wenye chuki ambao nyoyo zao zinaugua, wanao wakimbilia makafiri kwa ajili ya hifadhi kutokana na kile wanachodai kitawasibu.
[فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَنْ تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَنْ يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِنْ عِنْدِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنْفُسِهِمْ نَادِمِينَ]“Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jengine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Ma’ida: 52]
Kaka zangu na dada zangu, mgogoro umepamba moto juu ya Hizb ut Tahrir tangu kuasisiwa kwake. Kutokana na vitendo vya watu wengi ambao Mwenyezi Mungu amewapofua uoni wao, kutokana na ukafiri wao, au kwa sababu ya unafiki wao Mwenyezi Mungu akaondoa hisia kutoka katika nyoyo zao, hivyo wakashiriki katika madhambi na uovu wakidhani kuwa wanaweza kuzuia kurudi kwa Khilafah. Walikuwa ni mataifa yaliyo shutushwa na neno la Haki, na makundi na watu binafsi wanaoogopa neno la haki, na makundi yote yawezungukwa na njama yao ovu, na Mwenyezi Mungu Ta’ala ni Mkweli:
[وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ] “… Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya.” [Fatir: 43].
Ama kwa nchi za kikoloni za kikafiri zinazo chukia Uislamu na kurudi kwa dola yake, kwa chuki yao kwa Khilafah mithili ya makruseda, nchi hizi na vibaraka wao wamefanya kila aina ya juhudi iwezekanayo kuchora mbinu ovu na kutengeza mbinu chafu za kuwashtaki wafanyikazi wa dola ya Khilafah, kuwakamata na kuwatesa kufikia hadi ya kupata Shahada ndani ya magereza yao, huku wakati mwengine wakijihalalishia haya kwa madai ya uhalifu wa ugaidi, na nyakati nyingine kwa madai kuwa ni ukanda wa uzalishaji ugaidi. Hivi majuzi walikuja na madai ya ugaidi wa mtandaoni! Na kwamba chama hichi kinajaza kurasa za wanachama wake kwa maoni na fikra za ugaidi zenye kuchochea ghasia, hivyo basi wanawanyanyasa wanachama wa chama hichi katika kurasa zao na kuwaandama kwa kuwakamata na kuwatesa kwa kisingizio cha kutekeleza ugaidi wa mtandaoni! Na kila jicho linaweza kuona kuwa kurasa za wanachama wa chama hichi zinamulika neno la haki na kuonyesha uhalisia, huku kurasa zao watu hawa zikiwa zimejaa utapeli, udanganyifu, uongo na uzushi! Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali, wamepotoka kiasi gani hawa …
Ama kwa wale wenye nyoyo zinazo ugua, wanafiki na wale wanao eneza uzushi: ukiukaji na uzushi wao haukuanza leo bali zamani, lakini kashfa yao na madai yao ya urongo mwanzoni yalikuwa yameangazia dhidi ya uongozi na maafisa wa chama huku wakihadaa kupitia kuonyesha imani katika fikra na njia ya chama … Hivi ndivyo walivyo jitokeza na kuficha lengo lao halisi, ambalo ni kutingisha mwili wa chama hiki na sio tu uongozi wake pekee. Lakini katika miaka ya hivi karibuni wameanza kushambulia umbo la chama hiki, fikra na njia yake. Wameangazia shambulizi lao juu ya tabanni, Nusra, uongozi wa Ummah, kuhisabu, kikao cha mwezi, nk., na hivyo kujifichua wenyewe kabla ya kufichuliwa na wengine! Lengo walilokuwa wamelificha, ambalo ni kuutingisha mwili wa chama hiki katika fikra na njia yake, limekuwa dhahiri sasa kwa kila anaye weza kuona …Lakini chama hiki kimebakia imara, cha kipekee na chema.
[كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا] “… Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi…” [Ibrahim: 24-25] Sifa njema zote ziwe kwa Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu.
Kaka zangu na dada zangu waheshimiwa, nchi za kikoloni za kikafiri na vibaraka wao kamwe hawatapumzika, bali wataendelea kutengeza mbinu chafu, moja baada ya nyingine kwa sababu uzuiaji mafanikio ya chama hiki ya kusimamisha Khilafah ni kadhia nyeti kwao kama ambavyo kusimamisha Khilafah ni kadhia nyeti kwa chama hiki na waumini wote. Maadui wa Uislamu kwamwe hawatakoma njama zao dhidi ya chama hiki na Khilafah, na wataendelea. Ingawa wana uwezo zaidi kuliko sisi katika mbinu, licha ya hayo tuna mambo manne yanayo tupa hakikisho na kutia nguvu azma yetu na kamwe hatutatingishwa na mgogoro au kudhoofishwa na mzozo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu; bali watatuongezea nguvu juu ya nguvu, na upangaji njama ovu utawageukia dhidi yao wenyewe na utawapelekea kuangamia kwao.
[وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ] “Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibrahim: 46].
Na Hizb inaendelea kutangaza haki na haiogopi lawama ya yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hadi isimamishe tena Khilafah kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, licha ya matakwa ya watu hao.
Haya hapa ndio mambo hayo manne:
Jambo la kwanza: Pamoja na uzito huja wepesi, hili liko katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika zaidi ya aya moja:
[حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ] “Hata Mitume walipokata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya wakosefu.” [Yusuf: 110].
Hili limethibitishwa kupitia Seerah ya Mtume (saw) kuwa ushindi uko karibu kila uzito unapo ongezeka… Katika Seerah ya Ibn Hisham:
“Ibn Ishaq asema: Khadijah bint Khuwaylid na Abu Talib walifariki mwaka mmoja, na majanga yakamfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa mpigo… hii ilikuwa miaka mitatu kabla ya hijra… Ibn Ishaq asema: Pindi Mwenyezi Mungu Azza wa Jal alipotaka kuifanya Dini yake itawale na kumuimarisha Mtume wake (saw) na kutimiza ahadi yake (swt) … Yeye (saw) alikipokea kikundi cha Al-Khazraj … Yeye (saw) aliwalingania kwa Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal … wakamuitikia na kumkubali …”
Msimu uliofuata, ahadi ya kwanza ya utiifu (Bay’ah) ya Aqaba ikafanyika, kisha ahadi ya pili ya utiifu, kisha Hijra na kusimamisha dola … hivyo basi pindi waumini wanaofanya kazi wanapokabiliwa na uzito ni ishara ya wepesi na ushindi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Al-Qawi, Al Aziz, Al-Hakim.
Jambo la Pili: Mwenyezi Mungu ameahidi ukhalifah (utawala),
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ] “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [An-Nur: 55].
Mtume (saw) ametoa bishara njema ya Khilafah baada ya utawala wa kiimla tunaoishi chini yake leo: Imepokewa na Ahmad na Abu Dawoud kutoka kwa Hudhayfa kuwa Mtume (saw) amesema:
«...ثُمَّ تَكُونُ جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»، ثُمَّ سَكَتَ
...“…kisha kutakuwepo na utawala wa kutenza nguvu (ملكًا جبرية) na utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume.’ Kisha yeye ﷺ akanyamaza.”
Jambo la Tatu: Ahadi ya Mwenyezi Mungu ya utawala na bishara njema ya Mtume (saw) ya kurudi kwa Khilafah imeandikwa katika Qadar ya Mwenyezi Mungu, katika Elimu yake (swt) katika Al-Lawh al-Mahfoudh. Wakati wake umeandikwa na Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al-Hakim na hautacheleweshwa. Na kila siku ichapo hutusongeza karibu na wakati huo uliowekwa, na sio kutusongeza mbali nao, na hivyo nafsi zetu zina hamu na kuning’inia katika matarajio haya.
Jambo la Nne: Mwenyezi Mungu (swt) hatawateremsha malaika kusimamisha Khilafah kwa ajili yetu, bali ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kuwakirimu wale miongoni mwa watu ardhini wanaostahiki kuisimamisha kupitia mikono yao wenyewe, kwa bidii na kazi ya umakinifu na kuwa na ari na kufanya kazi hii kwa kujitolea. Hizb ut Tahrir inayofanya kazi kwa ajili ya Khilafah kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inaistahili na kuistahiki. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kutukirimu kwa ushindi na ufunguzi (Fath) na kwamba tuwe wanajeshi wa Khilafah na kuishuhudia, na Takbir zetu za Idd ziungane na Takbir
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ] “Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Ar-Rum: 4-5].
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd
Wassalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
Ndugu Yenu
Ata Bin Khalil Abu Al Rashtah Mkesha wa 10 Dhul Hijjah 1440 H
Amiri wa Hizb ut Tahrir sawia na 11/8/2019 M
Mwisho wa hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Allah amuhifadhi.
Pia ni furaha yangu kutoa pongezi zangu na zile za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wafanyikazi wake wote, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah na kwa Waislamu wote katika Idd hii yenye baraka.
Enyi Waislamu:
Idd hii imeitwa Idd ul-Adha kama ukumbusho kwetu pindi bwana wetu Ibrahim alipotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu ya kumtoa sadaka mwanawe mwema Ismail (as). Walipoiamini ndoto hiyo, Mwenyezi Mungu (swt) alisifu kujitolea kwao na kumleta kondoo mkubwa kama badala ya bwana wetu Ismail.
Anwani ya kujitolea huko ndiyo anwani ya maisha ya dunia, ni makaazi ya muda na baada yake kutakuwepo na makaazi ya milele. Maisha ya dunia ni fursa ya kujitolea baraka za muda ili kupata neema za milele.
Ummah wa Kiislamu ni vizazi vya kufuatana, na kila kizazi kina muda wake na kila muda una hali ambayo ni kadhia nambari moja ambayo Ummah mzima ni lazima ujitolee kwayo. Kadhia ya kizazi cha Ummah wakati wa zama za Salahuddin al-Ayyubi ilikuwa ni kuwafurusha Makruseda kutoka Ash-Sham, na kadhia ya kizazi cha Ummah huu wakati wa zama za Qutuz ilikuwa ni kuwafurusha Mongoli kutoka katika biladi za Waislamu, na kadhia ya kizazi cha Ummah huu katika zama za Muhammad al-Fatih ilikuwa ni ufunguzi wa Konstantinia.
Lakini Salahuddin, Qutuz na Muhammad al-Fatih walikuwa wakiitegemea dola ya Kiislamu katika kupanga safu za Ummah na kukusanya nguvu zao kufanya yale waliyoyafanya. Kizazi chetu wakati huu hakina dola kuukabili kwayo ulimwengu. Hivyo basi kadhia ya kizazi hiki cha Ummah wa Kiislamu – kizazi chetu, ni kusimamisha tena dola ya Kiislamu, Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Kurudi kwa Khilafah kutaufungulia tena Ummah mlango wa historia kama ilivyo vifungulia kila wakati vizazi vilivyotutangulia. Ni fursa ya Ummah wa Kiislamu kurudi katika dori yake ulimwenguni kupitia kuwa taifa bora lililotolewa kwa watu, kubeba nuru na kheri kwa walimwengu, na kufanya kazi nao kuiunda dunia iwe katika hali yake nzuri zaidi kama anavyotaka Mola wake, kuijenga upya kwa msingi wa mwamko halisi unao hifadhi utajiri wa Waislamu na kuhifadhi sitara ya vijana, na kuondoa mawingu ya ufisadi yaliyotanda dunia nzima.
Enyi Waislamu:
Kwa watu wa Ummah huu ambao wangali wanasitasita au kushughulishwa kutokana na kufanya kazi ya kuregesha utawala wa Uislamu, na kwa watu wanaomiliki uwezo na ulinzi na nguvu na mamlaka, katika Idd hii, tunawakumbusha kuwa maisha ni fursa ya kupita, na hakuna fursa nyingine baada ya fursa hii. Patilizeni umri wenu katika kile kinachomridhisha Mola wenu na tumieni wakati wenu katika lengo nambari moja la Ummah huu, kadhia ya kusimamisha tena dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Enyi Waislamu:
Hizb ut Tahrir, pamoja na wanachama, wanazuoni na wajuzi wake, wananyosha mikono yao kwenu, ili kufanya kazi nao kuregesha utawala kwa Uislamu na kuunda dola ya Kiislamu kwa mara nyengine tena.
Tunawalingania Waislamu wote kuwataka watu wenye nguvu na ulinzi kuregesha ubwana kwa sheria ya Mwenyezi Mungu.
Tunawalingania watu wenye nguvu na ulinzi kubadilisha hali ya batili.
Tunawakaribisha nyote kuchukua fursa hii.
Tunawakaribisha kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar
Idd Mubarak
Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |