Afisi ya Habari
Amerika
H. 22 Shawwal 1445 | Na: 04 / 1445 H |
M. Jumatano, 01 Mei 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu: Kufichuka kwa Mfumo Fisidifu wa Maadili!
(Imetafsiriwa)
Katika wimbi la maandamano ya hivi karibuni katika vyuo vikuu nchini Marekani na kote ulimwenguni, wanafunzi na vitivo wameelezea waziwazi kupinga kwao kwa njia ya amani, kupaza sauti na kampeni ya umma ikitaka kukomesha mauaji ya halaiki mjini Gaza. Maandamano haya ya wanafunzi, ishara ya rai jumla inayokua yamekumbwa na majibu kali na mara nyingi ya vurugu kutoka kwa utekelezaji wa sheria - mgongano mkubwa kwa uhuru unaodaiwa na jamii za kidemokrasia.
Serikali ya Marekani kihistoria imejiweka kama mtetezi wa uhuru wa kuzungumza na haki za binadamu, mwepesi kukashifu ukandamizaji mithili ya huu katika mataifa mengine pindi yanapokuwa hayaendani na sera ya kigeni ya Marekani.
Ilhali, kujitolea huku kunaonekana kupotea kwenye ardhi yake yenyewe wakati maandamano hayo yanapohusu vitendo vya umbile haramu la Kizayuni. Jibu kwa maandamano ya wanafunzi limeakisi mbinu za tawala za kiimla ambazo Marekani inadai kushutumu.
Katikati ya maandamano haya, kuna taarifa kubwa dhidi ya ufisadi wa siasa, dhulma, na kukandamiza wa matakwa sahihi, yanayosababishwa na uhalifu wazi wa mauaji ya halaiki dhidi ya raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Huku waandamanaji wakiwa, wa asili, makabila na dini tofauti tofauti ikiwa idadi kubwa ya wanafunzi wa Kiyahudi na kitivo wenye kutofautisha ukosoaji wao wa sera za Wazayuni za utetezi uliopitiliza wa Mayahudi. Hii inasisitiza upinzani wa pamoja sio dhidi ya dini au watu wake bali dhidi ya mauaji ya halaiki yanayofanywa na dola ya ubaguzi wa rangi ya Kizayuni.
Ukandamizaji huo unaonyesha upendeleo katika uhuru wa kuzungumza nchi Marekani: unanyanyuliwa pindi unapoambatana na masimulizi za serikali na kukandamizwa pindi unapowapinga.
Utekelezaji huu wa kimapendeleo unasaliti misingi ambayo serikali ya Marekani inadai kuitetea, na kufichua sura inayogongana na sura iliyonadiwa ya taifa hili kama nembo ya demokrasia na haki za binadamu.
Wakati ulimwengu unapoangalia kutukia kwa matukio haya katika taasisi za kielimu za kifahari - kutoka Chuo Kikuu cha Columbia hadi Chuo Kikuu cha California, Berkeley - kujitolea kikweli kwa maadili ya Marekani kunatiliwa shaka.
Kinaya hicho kinazidi pindi unapozingatia kuwa taasisi nyingi hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa katika safu za Huduma ya Mambo ya Nje ya Marekani, ikionyesha mgongano kati ya maadili yanayofundishwa na hatua zinazochukuliwa.
Simulizi hii haitoi changamoto tu juu ya maadili ya sera za Marekani lakini pia hubadilisha dhidi ya dhana zengine za kitamaduni, ambapo desturi za Kiislamu zinawafanya wasomi na wanafunzi kihistoria kuwahisabu viongozi wao;
Kujitahidi kuhakikisha kufuata sheria za msigi za maadili na viwango vya Kiislamu.
Matukio haya yanayotukia pia yanaangazia mgogoro mpana wa kithaqafa ndani ya maadili msingi yanayodaiwa kuiendesha Marekani.
Uhakiki huu unaalika tafakari juu ya utetezi wa kweli kwa maadili ambayo Marekani inayafundisha, na serikali ya Marekani inadai kusimama kwa ajili yake, ikihimiza kutathmini upya dori yake juu ya kuongoza wanadamu kwa njia ya kibinadamu na ya haki.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |