Afisi ya Habari
Australia
H. 23 Rabi' I 1445 | Na: 02 / 1445 H |
M. Jumapili, 08 Oktoba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waislamu wa Palestina Wamefichua Udhaifu wa Uvamizi wa Kiyahudi, lakini yako wapi Majeshi ya Waislamu?
(Imetafsiriwa)
Juhudi za upinzani nchini Palestina zililipuka mnamo Jumamosi asubuhi kwa shambulizi la alfajiri la kushtukiza kutoka Gaza. Mapigano na wavamizi wa Kiyahudi yalitokea, na kuua kadhaa na kuwakamata wengi zaidi. Vituo vya mpakani vilikanyagwa, vifaru vya adui vilipinduliwa na vikosi vya wavamizi kwa uoga vilikimbia vituo vyao.
Kwa kutabiri, walinzi wa uvamizi huo wamekimbilia kuutetea, wakiwachora wavamizi kama wahasiriwa na Waislamu jasiri wa Palestina kama wavamizi.
Waziri Mkuu Anthony Albanese amesimama na viongozi wengine wa Magharibi wakilaani 'Mashambulizi ya hivi karibuni', akitangaza 'Australia inasimama na rafiki yetu [Israel] katika wakati huu' na kusisitiza 'haki ya [Israeli] ya kujithami'.
Hizb ut Tahrir / Australia ingependa kukariri yafuatayo:
1. Palestina ni ardhi iliyokaliwa kimabavu, kila shubiri mraba yake. Hakuna suluhisho la uvamizi huu isipokuwa kuendelea na juhudi za upinzani hadi mageuzi kamili ya uvamizi yatakapopatikana.
2. Uvamizi wa Kiyahudi ulipandikizwa juu ya Palestina tu ili kutumikia malengo ya sera za kigeni za Magharibi. Pindi uvamizi huu unapokuwa hautumikii tena kusudi lake, dola za Magharibi zitawatelekeza huko Palestina kama vile zilivyowatelekeza kila wakati barani Ulaya.
3. Udhaifu na uoga wa vikosi vya uvamizi umewekwa wazi kwa wote kuuona. Ikiwa Waislamu wachache wanaweza kuutikisa uvamizi na 'jamii nzima ya kimataifa' kwa asubuhi moja pekee, ni kipi basi kinachoweza kupatikana kwa juhudi za pamoja za majeshi yanayozunguka ya nchi za Waislamu?
4. Hatupaswi kamwe kupoteza uoni katika ukweli kuwa ni jukumu la majeshi kupinga uvamizi na kuregesha hali shwari. Hasa, majeshi ya Waislamu yanayozunguka, ambayo viongozi wao wanawafungia kwenye kambi zao, wakishuhudia kama watazamaji ujasiri wa watu binafsi huku wakikaa kimya ndani ya vifaru na ndege zao.
5. Siku mbili tu zilizopita, Waziri Mkuu Albanese alijiingiza tena ndani ya jamii ya Waislamu, akijizungusha pambizoni mwa washirika wake wa Kiislamu, akizungumza kwa niaba yetu na kueneza sauti juu ya kujitolea kwa Australia kwa haki katika kushughulikia uvamizi wa nchi hizi kupitia kura ijayo ya maoni. Inatarajiwa kwamba Waislamu hao sasa wanahisi majuto baada ya unafiki wa wazi kutoka kwa Waziri Mkuu, kana kwamba kushughulikia uhalifu wa zamani wa kikoloni kamwe ilikuwa ni alama ya dola za Magharibi!
6. Juhudi za Waislamu nchini Palestina, na upinzani mtukufu wa Ummah na usio malizika na uvamizi na dhulma, unasimama tofauti kabisa na hofu iliyosababishwa na Magharibi juu yetu sisi wengine. Palestina ni kesi ni mfano tgu uliopo leo, lakini dhulma za ukoloni zinaenea kila kona ya ulimwengu. Ukombozi wa Palestina wa Waislamu utakuwa ndio mwanzo wa ukombozi wa wanadamu kutoka kwa vifungo vya Magharibi, na siku hiyo iko karibu zaidi kuliko vile tunavyofikiria inshaAllah.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Australia |
Address & Website Tel: |