Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  15 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 20
M.  Ijumaa, 18 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Mngurumo wa Jeshi la Waislamu chini ya Khilafah unatosha kupambana na Umbile Haramu la Kiyahudi”
Chini ya Bango hili, Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh iliandaa Maandamano katika Misikiti ya Dhaka na Chittagong

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, leo (18/10/2024) iliandaa mikusanyiko ya maandamano na kupinga katika majengo mbalimbali muhimu ya misikiti ya Dhaka na Chittagong siku ya Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa. Kutokana na maandamano hayo, Umma wa Kiislamu ulilinganiwa uharakishe kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo chini ya uongozi wake mngurumo wa majeshi ya Waislamu ungetosha kupambana na umbile haramu la Israel kutokana na mauaji ya halaiki. Khilafah tukufu itaunganisha vikosi vya majeshi ya Waislamu na kulifurusha umbile hili la Kiyahudi lililolaaniwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تُقَاتِلُوا الْيَهُودَ حَتَّى يَخْتَبِئَ الْيَهُودِيُّ وَرَاءَ الْحَجَرِ فَيَقُولُ الْحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ يَخْتَبِئُ وَرَائِي تَعَالَ فَاقْتُلْهُ»

“Kiyama hakitasimama hadi mupigane na Mayahudi, mpaka Yahudi atajifiche nyuma ya jiwe au mti, na jiwe hilo au mti huo utasema: ‘Ewe Muislamu, ewe mja wa Mwenyezi Mungu, huyu hapa Myahudi nyuma yangu; njoo umuue” (Sahih Muslim). Wazungumzaji katika mikusanyiko hiyo pia waliangazia mada zifuatazo:

- Dola za Kikoloni za Kikafiri za Kimagharibi, hasa Marekani, kwa kutoa silaha na pesa, na kwa upande mwingine, vibaraka wa Magharibi, watawala wa Misri – Jordan na nchi nyingine za Waislamu, kwa kuyafungia majeshi ya Waislamu katika kambi wanaisaidia Israel inayokalia kwa mabavu kutekeleza mauaji na uharibifu. Vilio vya kuomba msaada kutoka kwa watu wa Gaza na Ardhi Iliyobarikiwa vimefikia upeo wa macho. Sauti zao zimefika mbinguni. Wanasema, “Enyi Ummah wa Uislamu, ima mutusaidie, au tutakufa na kuangamizwa. Basi udhuru wenu ni upi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt)?”

- Amerika inataka kulimakinisha umbile hili la Kiyahudi katika ardhi za Kiarabu na Dola ya Kishirikina ya India katika eneo letu - ambao ni maadui wanaochukiwa wa Uislamu na Waislamu, ili kudumisha utawala wake wa Kikoloni kote duniani kote. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُواْ الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُواْ]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Ma’idah: 82].

- Tawala za kisekula katika nchi za Waislamu - vibaraka wa Magharibi, zinashirikiana katika vita vinavyoongozwa na Marekani dhidi ya Uislamu na Waislamu. Watawala wa Kiarabu katika Mashariki ya Kati na watawala wa Waislamu katika eneo letu, wanasaidia mtawalia kuimarisha mikono ya umbile haramu la ‘Israel’ na India. Ili kuchelewesha kudhihiri Khilafah - mlinzi wa Umma wa Kiislamu - wanaeneza uongo, propaganda na ukandamizaji dhidi ya wito wa Khilafah na Hizb ut Tahrir - chama cha wakweli chenye kubeba wito wa Khilafah. Lakini Ummah wa Kiislamu una imani kamili na bishara njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النَّبُوَّةِ» “kisha itakuweko Khilafah kwa njia ya Utume” (Hadith: Musnad Ahmad).

Wazungumzaji pia walisema kwamba, hakika katika Ummah kuna maelfu na maelfu, au zaidi, ya askari wanaopenda kifo katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), kama vile adui anavyopenda uhai. Hata hivyo, watawala hawa vibaraka wamekuzuieni musiwanusuru ndugu zenu, na badala yake, wanamuunga mkono adui yenu katika kuwaua ndugu zenu. Kwa hivyo, munapaswa kuvitaka vikosi vya jeshi kukiondoa kikwazo hiki kwa kuwaondoa hawa watawala vibaraka na kukabidhi mamlaka kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah. Mngurumo wa jeshi la Waislamu chini ya Khilafah unatosha kulifurusha umbile haramu la Kiyahudi.

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [Surah At-Tawba: 14]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu