Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  17 Rabi' I 1445 Na: 1445 / 03
M.  Jumatatu, 02 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Imetosha Sasa! Je! Kuna Yeyote wa Kutilia Maanani?!
(Imetafsiriwa)

Janga jengine limeongezeka juu ya maelfu ya majanga ambayo yamekuwa kitovu cha maisha ya Wairaqi wenye msiba, baada ya moto kuzuka katika ukumbi wa matukio katika wilaya ya Hamdaniya yenye Wakristo wengi, katika Jimbo la Nineveh, na kuua zaidi ya watu mia na kujeruhi kadhaa.

Tukio hili sio la pekee, kwani limetanguliwa na matukio mengi, ya muhimu zaidi:

- Mnamo 2013, watu 100 walikufa baada ya mgahawa wa Lebanon wa kuelea majini huko Baghdad kuzama.

- Mnamo Machi 2019, zaidi ya watu 120 walikufa na wengine kupotea, katika feri iliyo zama mjini Mosul.

- Mnamo Julai 2021, moto katika hospitali ya Al-Hussein katika Jimbo la Dhi Qar ulisababisha vifo vya watu wapatao 64 na majeruhi kadhaa.

- Ilifuatiwa, katika mwaka huo huo, na mkasa wa kuungua kwa Hospitali ya Ibn al-Khatib katika mji mkuu, Baghdad, ambapo ilisababisha vifo vya watu wapatao 82 na majeruhi kadhaa pia.

- Mbali na mioto ya msimu inayofagia mashamba ya ngano kaskazini na kusini.

Katika matukio haya yote na mengine mengi, watu wa Iraq hawakuona hatua yoyote ya umakinifu au masuluhisho halisi, na uchunguzi na hatua za serikali zilizofuatia matukio hayo hayakufanikiwa kuhifadhi maisha ya Wairaqi na kukomesha msururu huu wa upotezaji maisha, na sababu ya hili ni ufisadi ulioenea nchini.

Hivi ndivyo Majid Shankali (Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira katika Bunge la Iraq) alivyo sema katika mahojiano na Al Jazeera Net: "Ni kazi ya Ulinzi wa Raia nchini Iraq kwa mujibu wa sheria kukagua vituo vya biashara mara kwa mara, lakini Uingiliaji wa maafisa na watu wenye ushawishi huzuia utekelezaji wa sheria." Akisisitiza kwamba "ufisadi ulioenea katika taasisi za serikali ndio sababu kuu ya kile kinachotokea, na kwamba 95% ya uwekezaji wa sekta ya kibinafsi na ya umma unakosa kabisa mahitaji ya ulinzi wa raia, pamoja na milango ya dharura, mifumo ya onyo la mapema, zimamoto, na hali za usalama."

Matokeo ya uchunguzi huu yalisababisha kufutwa kazi kwa maafisa kadhaa huko Al-Hamdaniya, na kukamatwa kwa mkurugenzi wa ukumbi huo, na hili lilikataliwa na Askofu Mkuu wa Katoliki wa Syriania wa Mosul, Mar Benedict Younan Hanno, kulingana na kile kilichoripotiwa na Gazeti la Al-Yaum, kama alivyowaambia waandishi wa habari: "Matokeo ya uchunguzi yamekataliwa kabisa, na hayaakisi ukweli wa kile kilichotokea."

Hanno alisema kwamba kamati ya uchunguzi haikuzingatia ushuhuda wa mashahidi, na alidai kwamba mashirika ya kimataifa yachunguze tukio hilo la kutisha. Aliongeza: "Uchunguzi wote wa serikali unaelekeza sababu za majanga nchini kuwa matukio ya ajali. Hatupaswi kukaa kimya juu ya kile kinachotokea," akiashiria kuwa "misamaha na ufutaji kazi huenda ikawa matokeo ya kufilisika kisiasa."

Enyi Watu wa Iraq: Kuna tofauti kubwa kati ya wale wanaouona utawala na usimamizi kama ngawira, na njia kufikia utajiri na kujinafsi, na wale wanaouona kama amana nzito na jukumu kubwa. Abu Dharr alisema kwamba alimuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amfanye kuwa gavana (Wali), lakini akamgonga begani mwake na akasema,

«يا أَبَا ذَرٍّ، إنَّكَ ضَعِيفٌ، وإنَّهَا أَمَانَةُ، وإنَّهَا يَومَ القِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ، إلَّا مَن أَخَذَهَا بحَقِّهَا، وَأَدَّى الذي عليه فِيهَا»

Ewe Abu Dharr, hakika wewe ni dhaifu, na hakika hiyo ni amana, itakayo sababisha fedheha na majuto Siku ya Kiyama isipokuwa kwa yule atakayeitendea haki yake, na kutekeleza wajibu wake juu yake.” (Imepokewa na Muslim). Usimamizi wa umma ni jambo hatari, na mtawala anabeba athari zake katika ulimwengu huu na kesho Akhera. Ana jukumu la kusimamisha haki na uadilifu miongoni mwa raia, na matokeo yake ni hasara ikiwa hatauchukua kama unavyostahili, na kutekeleza majukumu yake na uadilifu.

Hivi ndivyo Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) walivyouelewa. Umar, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, aliogopa jukumu hili kiasi kwamba ilibidi afanye ukaguzi yeye mwenyewe, na kuwafuatilia magavana wake na wafanyikazi, na akasema msemo wake maarufu: "Ikiwa mbuzi atakufa kwenye fuo za Furat katika kijiji, naogopa kuulizwa juu yake."

Wakati jua la Khilafah lilipokutwa juu ya nchi zote za Waislamu, na Ruwaibida wakatawala juu ya Ummah, haki zilipotea, dhulma ikashamiri, machafuko yakaongezeka, na ufisadi umeenea.

Enyi Waislamu nchini Iraq na Kwengineko: Jueni kuwa hamuna usalama na hamuna hadhi ya damu yenu, isipokuwa kwa kufanya lile Mwenyezi Mungu amekulazimisheni, ambalo ni kufanya kazi kwa bidii kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Daima tumekulinganieni mufanye kile kinacho kukirimuni, lakini kutochukua hatua kwenu kumeongeza tu udhalilishaji kwenu, na leo. Imetosha imetosha, wimbi limefikia kilele chake, hamuna chaguo ila kubadilisha hali yenu kwa kuitikia amri ya Mola wenu, kwani Yeye ndiye Mlezi wenu na hatayatelekeza matendo yenu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu