Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  4 Muharram 1445 Na: 1445 / 01
M.  Jumamosi, 22 Julai 2023

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Kutoka Kizazi cha Kwanza cha Mashababu wa Hizb ut Tahrir

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)

Ikiwa na nyoyo zinazougua zinazotafuta tu ujira, Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inaomboleza pamoja na watu nchini Jordan na Ummah wa Kiisilamu, Mbebaji Dawah, mmoja wa Mashababu wake wema, safi na wacha Mungu, na hatumtakasi mtu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu, kutoka Kizazi cha kwanza cha Hizb Ut Tahrir:

Mheshimiwa Hajj Muhammed Musa Abdulhaleem Obaid Al-Faqeeh (Abu Jafar)

Ambaye amerudi kwenye rehma ya Mwenyezi Mungu Mwenyezi leo, Jumamosi, 4 Muharram 1445 H, sawia na 22/07/2023, na ambaye alitumia maisha yake kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah, akibeba ulinganizi huu kwa bidii, uvumilivu, na kwa uaminifu, na juu ya agano, tunamchukulia kuwa hivyo, licha ya madhara na ugumu alioukabili.

Hajj Abu Jafar, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa amejiunga na Hizb ut Tahrir na kubeba Da'wah katika safu zake, miaka ya hamsini, na kwa sababu hiyo alikabiliwa na mateso na shida nyingi mikononi mwa huduma za usalama na ujasusi, Hasa katika miaka ya thamanini. Alikufa kwa sababu ya maradhi ya muda mrefu ambayo aliugua kwa zaidi ya miaka mitano, ambayo aliishi kwa subra na kutafuta tu thawabu, akiwa na umri wa miaka 85.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mwenyezi amsamehe na kumpa rehma kubwa juu yake, na kumkusanya pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, na wema katika bustani za neema - ni maswahaba watukufu walioje hao. Tunamuomba pia Mwenyezi Mungu (swt) kuipa ilham familia yake kwa subra, faraja, na rambirambi njema, na tunasema tu yale aliyotuamrisha Mwenyezi Mungu kusema:

[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah:156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hotuba ya Sheikh Saeed Radhwan (Abu Imad) katika kikao cha kutoa rambirambi za Hajj Muhammed Musa Abdulhaleem Obaid Al-Faqih

ha

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu