Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 7 Rabi' II 1446 | Na: 1446 / 03 |
M. Alhamisi, 10 Oktoba 2024 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Ahzab: 23]
Kalima ya ujumbe wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan Katika mazishi ya Hajj Youssef Mustafa Al-Toubasi (Abu Osama)
Imetolewa kwa niaba ya ujumbe huo na Ustadh Bilal Al-Qasrawi
Kutokana na imani kwa Qadhaa ya Mwenyezi Mungu, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inamuomboleza:
Hajj Youssef Mustafa Al-Toubasi (Abu Osama)
Aliyefariki dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu leo, Alhamisi, 10/10/2024. Yeye ni mmoja wa mashababu wa kizazi cha kwanza cha Hizb ut Tahrir, ambapo alijiunga na kubeba ulinganizi huu katika safu za Hizb ut Tahrir katika miaka ya hamsini ya karne iliyopita, baada ya maisha yaliyojaa kazi ya kuanzisha tena maisha kamili ya Kiislamu na kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu.
Uzee wake, maradhi, mateso, na kufungwa jela mara tatu mikononi mwa madhalimu havikumzuia kuendelea na shughuli yake na mapambano, subira na kutafuta malipo, kwani alitumia maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, mpaka alipofariki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amghufirie maiti wetu, na ampe makaazi mahala pema katika Pepo Yake pamoja na Manabii, na wakweli, na mashahidi na watu wema na hao ndio marafiki wema.
Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu na ampe makaazi mema katika Pepo Yake awape ujira mkubwa familia yake na jamaa zake na awape subira na faraja, na hatusemi isipokuwa yale tu yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt), ni cha Mwenyezi Mungu alichotoa, na ni cha Mwenyezi Mungu alichochukua na kila kitu Kwake kina Qadar.
﴿إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴾
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Baqara: 156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |