Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 1 Jumada II 1446 | Na: 1446 / 08 |
M. Jumanne, 03 Disemba 2024 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)
Kwa imani katika qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) na kutaka malipo Yake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inamuomboleza Mbebaji Da’wah katika safu zake:
Hajj Mustafa Abdullah Al-Issa Al-Jaber Al-Aboushi (Abu Anas)
Aliyefariki kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu asubuhi ya leo, Jumanne, 3/12/2024, akiwa na umri wa miaka 80.
Abu Anas alitumia miaka yake kubeba Dawah kwa ajili ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida. Alijiunga na Hizb ut Tahrir mapema katika ujana wake na alikuwa mvumilivu, mkakamavu, na mwenye bidii katika kutangaza haki. Alifungwa katika safari yake ya da’wah katika jela za madhalimu na akabaki imara katika kubeba Dawah hadi kifo chake, alikuwa mkweli kwa yale aliyomuahidi Mwenyezi Mungu. Sisi tunamhisabu kuwa hivyo na wala hatumtakasi yeyote kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye mhasibu wake.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu kwa rehema yake inayokizunguka kila kitu, amuingize katika Jannah yake pana, na amjaalie kuwa miongoni mwa watu wa Al-Firdaus Al-A'la (Pepo ya juu kabisa) pamoja na Mitume, wakweli, mashahidi, na watu wema - na hao ni maswahaba bora walioje. Vile vile tunamuomba Mwenyezi Mungu ayafanye makubwa malipo ya familia yake na awajaalie kuwa miongoni mwa wenye subira wanaotaka malipo yake.
[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara:156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Kalima ya Ustadh Marwan Obaid
katika Mazishi ya Hajj Mustafa Abdullah Al-Issa Al-Jaber Al-Aboushi (Abu Anas) Mwenyezi Mungu Amrehemu
Kalima ya Ujumbe wa Hizb ut Tahrir iliyowasilishwa na Ustadh Bilal Al-Qasrawy
katika Kikao cha kutoa Rambirambi kwa Hajj Mustafa Abdullah Al-Issa Al-Jaber Al-Aboushi (Abu Anas) Mwenyezi Mungu Amrehemu
Jumatano, 02 Jumada Al-Akhir 1446 H sawia na 04/12/2024 M
Kalima ya Ustadh Muhammad Abu Al-Haega
katika Kikao cha kutoa Rambirambi kwa Hajj Mustafa Abdullah Al-Issa Al-Jaber Al-Aboushi (Abu Anas) Mwenyezi Mungu Amrehemu
Jumatano, 02 Jumada Al-Akhir 1446 H sawia na 04/12/2024 M
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |