Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  4 Sha'aban 1437 Na: 1437/02 H
M.  Jumatano, 11 Mei 2016

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe wa Hizb ut Tahrir Uko Wazi Kabisa na Si Tishio kwa Usalama

Chama cha Kisiasa cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir Kenya kimesikitishwa sana na hatua iliyochukuliwa na vyombo vya usalama nchini Kenya kusitisha Kongamano lao jijini Mombasa. Kongamano hilo chini ya kauli mbiu "Khilafah Tuitakayo kwa Njia ya Utume" lililo andaliwa kufanyika mnamo Jumapili 8 Mei 2016 kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni lilisimamishwa dakika ya mwisho kwa madai ya 'sababu za kiusalama'. Mada kuu ilikuwa ni kudhihirisha sura halisi ya Khilafah katika utekelezaji wake wa sheria za Mwenyezi Mungu (swt) kupitia miundo yake, njia ya kuisimamisha tena na haki za raia wake ambao wanajumuisha wasiokuwa Waislamu.    

Mada hiyo ililenga kuzifafanua fikra duni zinazo elekezewa Khilafah pamoja na sheria nyinginezo za Kiislamu ambazo vilevile zinakabiliwa nazo kupitia Wamagharibi. Pia ilikuwa ni kuangazia kwa nini Afrika inahitaji Khilafah; serikali ambayo ina uwezo wa kutatua changamoto zinazo likumba bara hili ikiwemo uporaji wa kiuchumi na ukoloni mamboleo wa kisiasa pamoja na wa kijamii kupitia urasilimali.   

Licha ya hayo ukweli ni kuwa baadhi ya wanachama wa chama hiki walivikabili vyombo vya usalama jijini Mombasa ili kuzungumza navyo kuwa kufanyika kwa kongamano hili hakutaathiri sheria zozote za Kenya; lakini, bado walisisitiza juu ya uamuzi wao wa kulisitisha kongamano kwa muda usiojulikana kwa madai ya 'sababu za kiusalama'. Kwa kukatikiwa na uamuzi wao ni wazi kuwa polisi walitegemea na kuegemea porojo juu ya kongamano hilo kuwa linahatarisha usalama. Ni kwa nukta hiyo ndio tuna shaka na vyombo hivyo vya usalama kuwa havikufanya uchunguzi wa kisawa sawa badala yake vilifanya uamuzi wao kwa kutegemea uvumi kutoka kwa wale wanaotaka kuleta mgawanyiko miongoni mwa walinganizi wa Uislamu na Khilafah walio imara na wenye ikhlasi.    

Kwa hakika hatua hii iliyochukuliwa inashangaza na inatiashaka ikizingatiwa kuwa Hizb ut Tahrir nyuma ishawahi kufanya makongamano ya kimataifa na wala hakukushuhudiwa wala kuhusishwa na utovu wowote wa usalama. Na sio hilo tu; kwa miongo sita iliyopita wanachama wake wamejulikana kuwa wachangiaji wakubwa katika sekta tofauti ikiwemo elimu, matibabu, uhandisi, nk.      

Mwisho, tunasema kinaga ubaga kuwa hatua hii iliyochukuliwa inalenga kuwachafulia jina walinganizi wa haki wenye ikhlasi – mabalozi wa Uislamu ambao hawana silaha zozote; isipokuwa, wana imani na bishara njema ya Mola wao kuwa watapewa Khilafah duniani kama walivyopewa wale waliokuwa kabla yao. Na kutokana na silaha hiyo Hizb itaendelea katika ulinganizi wake adilifu na kuvuka vizuizi vyote dhidi yake kwa Rehma na Huruma za Mwenyezi Mungu (swt). Licha ya hayo, Hizb ut Tahrir inavichukulia vikwazo hivi kuwa ni alama za kukaribia kwa nusra ya Mwenyezi Mungu (swt).

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu