Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 6 Rabi' II 1442 | Na: 1442/012 |
M. Jumamosi, 21 Novemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ulinzi Halisi kwa Mwanawake Uko katika Nidhamu ya Kisiasa
Inayomrudishia Dori yake Muhimu katika Ujenzi wa Vizazi vya Ummah
(Imetafsiriwa)
Wavuti wa Kiarabu ya BBC, chini ya kichwa "Unyanyasaji: siri iliyofichuliwa katika maisha ya waandishi wa habari wa kike wa Kiarabu," uliwasilisha hali tatu mbaya kwa waandishi wa habari wa kike kutoka nchi tofauti za Kiarabu, ambao walizipitia wakati wakiendelea na kazi zao. Ulitoa mwanga kuhusiana nao juu ya suala ambalo sio jipya, lakini linarudia kujitokeza leo kwa idadi ya kushtua na viwango vya juu, kama takwimu za hivi karibuni zilizochapishwa na wavuti ya Uhakiki wa Idadi ya Watu Duniani (World Population Review) zinaonyesha kwamba karibu 35% ya wanawake kote ulimwenguni wamepitia shida ya unyanyasaji wa kijinsia, na kwamba ni 40% pekee kati yao, wanaotafuta msaada, na chini ya 10% yao hutumia sheria kupata suluhisho. Utafiti uliotolewa na Chuo Kikuu cha Amerika cha Beirut mnamo 2015 kwa anwani "Kukabiliana na ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia uliokithiri katika vyombo vya habari vya Lebanon," ulionyesha kuwa unyanyasaji unaathiri kazi ya asilimia 82 ya waandishi wa habari wa kike nchini Lebanon. Nchini Misri, kulingana na utafiti uliofanywa na Hanan El-Gendy, profesa wa vyombo vya habari katika Chuo Kikuu cha Al-Ahram cha Canada mnamo 2015, asilimia 85 ya wanawake wa Misri wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari wanakabiliwa na unyanyasaji wa kimaneno na asilimia 64 wanakabiliwa na unyanyasaji wa kimwili. Hilo lilikuja katika utafiti ulioitwa "Jinsia na Vyombo vya Habari nchini Misri," na utafiti huo ulitokana na dodoso lililosambazwa kwa waandishi wa habari wa jinsia zote katika vituo anuwai vya habari.
Kwa kuzingatia ongezeko la hali ya unyanyasaji, kulingana na kile BBC iliripoti kupitia ulimi wa wanahabari hawa wa kike katika nchi za Kiisilamu, na kuongezeka kwa masafa yake na ukubwa wa idadi iliyotolewa - na uwezekano kwamba zilitolewa katika muktadha wa kuonyesha jamii zetu kuwa zimezama katika uovu uliofichika - kwa hivyo kule kuendelea kwa wanawake kuteseka katika nchi za Kiarabu imekuwa mada ya kawaida. Iwe kwenye vyombo vya habari au makongamano, na pia kwenye tovuti za mawasiliano za kielektroniki, kutufunulia hadithi nyingi za unyanyasaji ambazo ziko kimya, labda kwa kuogopa aibu au kuhatarisha mustakbali wa taaluma; Hii pia ililazimisha kupiga mbiu kati ya serikali zingine, zinazoendeshwa na mashirika ya haki za binadamu na jumuia za wanawake, kutafuta kwa bidii suluhisho bora za kuzuia kuenea kwa uovu huu. Lakini ni wapi mahali pa utata wa kihakika juu ya ufanisi wa mchakato na tiba ambayo serikali zinakusudia kupitisha, na je! Zinauwezo wa kuzitokomeza kutoka kwa mwili wa mujtamaa??
Ni hakika kwamba kile wanachokabiliwa wanawake cha unyanyasaji katika nchi za Kiarabu ndicho wanachokabiliwa wanawake katika nchi zote za ulimwengu na katika nyanja zote za maisha, ikijumuisha katika siasa, vyombo vya habari, taasisi za elimu na jeshi, na nyanja za matibabu. Ni natija halisi na inayotarajiwa katika nchi ambayo wanawake wamepewa uhuru na uwazi kamili kwa mujibu wa mfumo wa kisekula wa kirasilimali. Kukuza utamaduni wa kutowaheshimu wanawake kati ya wanaume wengi, pamoja na kukuza ujinsia katika jamii na kuwachukulia wanawake kuwa ni bidhaa ya kijinsia kupitia burudani, matangazo na njia zingine, na kuwabadilisha kuwa chombo cha kukidhi matakwa ya wanaume, na kwamba lazima waonyeshe urembo wao kwa umma na wachanganyike na wanaume kazini, sokoni na kwenye sherehe ili jamii iwakubali, vinginevyo watakataliwa! Kwa kifupi, ni mfumo mbovu ambao umesababisha kuenea kwa unyanyasaji wa kijinsia kwa kiwango cha janga ambalo linaathiri wasichana na wanawake katika vyuo vikuu, sehemu za kazi, na mitaani, ambalo limesababisha kuzorota kwa dori ya wanawake katika maendeleo jumla ya jamii.
Suluhisho la kuzuia uhalifu kama huu sio kwa kubadilisha au kurekebisha sheria, kwa sababu sheria hizi zimeundwa na wanadamu na zinategemea maoni na dhana potofu za Magharibi, wala si kwa kutia ukali adhabu kwa mhalifu kwa sababu haitamzuia kufanya uhalifu wake katika uhalisia ambao mtazamo wa Uislamu umetoweka katika maisha, na manufaa na maslahi kuwa ndio kupimo ...
Hakika ulinzi halisi ambao mwanamke anautafuta uko katika mfumo unaomrudishia mwanamke haki na hadhi yake na kumregeshea dori yake muhimu katika ujenzi wa vizazi vya umma, na hii inaweza kupatikana tu na kuhakikishiwa kwa kuzingatia nidhamu ya kisiasa ya Khilafah, ambayo inakataza dhulma za kijinsia kwa wanawake kwa lengo lolote lile, ambayo hulinda heshima ya wanawake kwa umbo ambalo liko juu ya kutafuta maslahi yoyote ya kifedha au ya kimada. Hii ni pamoja na kuweka adhabu kali kwa aina yoyote ya ukiukaji wa heshima ya mwanamke, hata kwa tamko moja tu dhidi ya heshima yake.
Ni nini wanachokihitaji sana wanawake na wanaume chini ya kivuli cha maisha ya uasherati waliyolazimishiwa juu yao katika nchi za Waislamu leo, wanachohitajia ni mfumo wa Uislamu ambao unapatikana utulivu na huhifadhi hadhi ya kila mmoja wao. Basi Ewe Mwenyezi Mungu uandalie Ummah huu Khilafah Rashida kwa njia ya Utume haraka kuliko baadaye, kwani hilo kwa Mwenyezi Mungu ni rahisi.
Kitengo cha Wanawake
Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |