Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 27 Rabi' I 1443 | Na: 1443 H / 014 |
M. Jumatano, 03 Novemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto 10,000 Wameuwawa au Kulemazwa wakati wa Vita nchini Yemen
Mpaka Lini Idadi ya Watoto wa Yemen Itaendelea Kufa?!
(Imetafsiriwa)
UNICEF ilitangaza kuwa watoto 10,000 wa Yemen ima wameuawa au kulemazwa tangu kuanza kwa vita nchini Yemen mwezi Machi 2015 na kuongezea kuwa vifo vingi zaidi vya watoto na majeruhi havirekodiwi na milioni 11 wanahitaji msaada wa kibinadamu na karibu 400,000 wanaugua utapiamlo mkali huku zaidi yawatoto milioni 2 hawako shuleni.
Lugha ya idadi, takwimu na mlinganisho yakaribia kutokuwa na mwisho chini ya vita hivi dhidi ya Yemen na watu wake, sawa na vita na majanga yanayowapata Waislamu kote duniani. Licha ya takwimu hizo za kutisha za mateso hayo ya binadamu, dunia imesimama kama mtazamaji aliyelemaa bila ya kufanya lolote kukomesha maafa haya ya kibinadamu, huku watoto wa Yemen wakilipa gharama kubwa wakati wa vita hivi ambavyo nchi hiyo imekuwa ikishuhudia kwa miaka sita, ya mauaji, na ulengaji wa moja kwa moja na wa kimpangilio uliosababisha mamia ya watoto kulemazwa kabisa kutokana na makombora yaliyotawanyika, mabomu ya ardhini na kulengwa kwa shule na vitongoji vya makaazi.
Miaka sita ya maafa na mgogoro wa kibinadamu, na hadi leo hii, hakuna watawala wa Waislamu, majeshi, serikali au kamati za kimataifa zenye irada ya kisiasa ya kuhitimisha vita hivi vinavyotishia kusambaratika kwa kizazi kizima nchini Yemen. Hii ni huku nchi na kamati nyingi zikijiandaa kuadhimisha Siku ya Mtoto Duniani na kuonyesha mafanikio na mapato yao, katika wakati ambapo umri wa utoto unakiukwa nchini Yemen na kutekelezwa uhalifu muovu zaidi wa kibinadamu kinyume na desturi za kimataifa na kimaadili na sheria za ndani ya nchi juu yake. Hivi ulimwengu huu unaishi katika unafiki gani na ni udanganyifu ulioje unaofanywa na kamati na mashirika haya?
Zaidi ya hayo, kitendawili hiki baina ya watoto wa Yemen na sherehe ya Siku ya Mtoto Duniani kinatoa kiashirio cha khiyana, utumuaji, uzembe, mapuuza na kutojali kwa vijidola hivi na mashirika hayo. Hii ni haswa kwa kuwa tunajua kuwa mfumo wa kirasilimali, viongozi wake, serikali zake na mashirika yake ndio wahusika wakuu katika mzozo huu kwani wanaelekeza watoto wao wa mbwa katika nchi za muungano au wanamgambo wa Houthi wa Iran na Serikali ya Abdrabbuh Mansur na mamluki wa Baraza la Mpito kuchukua fursa ya umwagaji damu, na kusababisha masaibu kwa watoto wa Yemen kwa mfano wa wazi wa ubaya wa mfumo wa kimataifa wa leo na ukatili wa uhalifu unaoufanya dhidi ya Umma wetu na haswa nchini Yemen.
Hakuna kitu kitakachofanya kurasa za picha hii chafu kuwa nyeupe isipokuwa hukumu ya sheria ya Mwenyezi Mungu juu ya ardhi yake kwa kusimamisha utawala wa Uislamu chini ya dola ya Khilafah Rashida, unaokuja hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na hakuna kitakachomaliza mfumo huu mbaya wa kirasilimali isipokuwa mfumo adilifu wa Uislamu. Na hakuna kitakachosababisha mateso haya ya watoto wa Yemen kutoweka isipokuwa kwa kuishi kwa kufuata Uislamu, unaowapa chakula dhidi ya njaa, unaowaweka salama kutokana na hofu na badala ya taabu zao huweka furaha na nuru.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |