Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 26 Shawwal 1443 | Na: 1443 H / 035 |
M. Alhamisi, 26 Mei 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mfumko wa Bei Wawaacha Wanawake Waislamu nchini India Kutelekezwa katika Mgogoro Hatari wa Kiafya
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 14 Mei, gazeti la Times la India lilichapisha ripoti kuhusiana na jinsi viwango vya mfumko wa bei vimeathiri pakubwa maisha ya kiuchumi ya wanawake wa Kiislamu na kuwaacha katika hatari ya matatizo makubwa ya kiafya. Mamia ya wanawake wa Kiislamu wanapanga foleni nje ya kliniki wakiwa na hali mbaya wanaohitaji usaidizi wa kijamii na kifedha. Lakini, mahitaji yao hayatimiziwi na wengi hawawezi kufikia aina yoyote ya usaidizi ili kuinua hali zao. Wanawake wengi waliopewa talaka na hawana mfumo ufaao wa kukidhi mahitaji yao mara nyingi huachwa katika hali mbaya kutokana na unyanyapaa wa kikafiri ambao wanawake walioachika wanakumbana nao. Safura, kifua kikuu, polycystic ovaries, kisukari, magonjwa ya ngozi na upungufu wa vitamini ni hali zinazoripotiwa kwa kawaida. Wanawake wengi wana mlo wa kimsingi sana, mara nyingi wanakula wali-dal au chai-roti kila siku, bila kupata matunda, nyama au mboga mboga, mayai au maziwa. Dkt Aseema Mumtaz, akifanya kazi na wanawake hao kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa alisema ana makumi ya wanawake wanaokuja kwake ambao wana upungufu mkubwa wa damu. Anasema: “Ingawa tunawapa protini, virutubishi vya calcium, ambavyo kamwe haviwezi kufidia lishe mtu anayoipata kutoka kwa chakula.” Mujtaba Hasan Askari, mwanzilishi wa Wakfu wa Helping Hands alieleza: “Bei ya juu ya vyakula imesababisha kupungua kwa kiwango cha lishe cha chakula. Imesababisha utapiamlo moja kwa moja hasa kwa watoto.”
Hali hii ya hatari ina sababu moja pekee ambayo haiwezi kulaumiwa kwa vita vya Ukraine au ukosefu wa utulivu wa ulimwengu. Ukweli ni kwamba mfumo mzima wa kijamii na kisiasa umeegemezwa juu ya kutumikia mahitaji ya kipote cha mabwenyenye wachache na kuwaondoa mafukara kama kipaumbele, hivyo wanyonge wanazidi kuwa wanyonge. Zaidi ya hayo, mfumo wa uchumi wa kirasilimali umeonekana kuwa na dosari kabisa na hauwezi kutimiza mahitaji ya raia.
Kudhamini mahitaji ya wanawake, hususan wanawake wasio na waume kama wajane, ni jukumu la Khalifa chini ya mfumo wa kisiasa wa Kiislamu, Khilafah. Mtume (saw) kama kiongozi wa dola mjini Madina alisema: «مَنْ تَرَكَ مَالاً فَلأِهْلِهِ وَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضَيَاعًا فَإِلَيَّ وَعَلَيَّ» “Yeyote aliyeacha mali (baada ya kufa) basi ni ya jamaa zake, na yeyote aliyeacha deni au watu wanaomtegemea yeye, basi ni juu yangu kulilipa na kuwasimamia.” Kuishi bila ya kuwepo dola ya Khilafah na bila ya hukmu hii ya Kiislamu kumewaacha mamilioni ya wanawake Waislamu, sio tu nchini India bali kote katika ardhi za Waislamu katika hali ngumu ya kifedha na taathira za maisha na kifo. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَيُطۡعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَى حُبِّهِ مِسۡكِينً۬ا وَيَتِيمً۬ا وَأَسِيرًا]
“Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.” [Al-Insan: 8].
Katika mfano mtukufu wa Khalifa wa pili wa Waislamu, Umar Ibn Al Khattab (ra), tuliona jinsi alivyofanya doria mitaani ili kuhakikisha kwamba mahitaji ya watu wake yanatimizwa, na jinsi alivyobeba chakula mgongoni mwake kutoka Bait Al Maal (Hazina Kuu) kumlisha mama na watoto wake ambao walikuwa na njaa kutokana na umaskini. Angekosa usingizi kwa ajili ya hata kondoo mlimani kutokuwa na riziki ya kutosha. Chini ya mfumo huu wa Kiislamu, wanawake walikuwa na haki ya fedha za Bait Al Maal, ili kuhakikisha kamwe hawalazimiki kuomba mahitaji yao ya kimsingi au kuteseka kutokana na dhiki ya kifedha.
Chini ya kivuli cha uongozi wa Kiislamu wa Khilafah, hakuna chaguo kwa kiongozi kuacha masuala ya usalama wa kimwili au kifedha ya wanawake kwa kubahatisha au athari za kikafiri. Serikali inawajibu wa kuwaandalia mahitaji yao ya kimsingi na hali ya maisha yenye utu kiasi kwamba walindwe dhidi ya kuhangaika kwa siku moja kujilisha wenyewe na familia zao. Kwa hakika mfumo wa utawala wa Kiislamu upo kama njia ya kuwainua wanadamu kutoka katika aina zote za ukandamizaji, dhulma, kupuuzwa na udhalimu na kutoa mahitaji ya kimsingi na usalama wa kifedha kwa kila mwanadamu. Njia pekee ya wanawake Waislamu, na kwa hakika wanawake wote wa nchi za Kiislamu kujinasua na ugomvi huu wa kifedha ni kuziondoa tawala fisadi, zisizo na uwezo na zisizo na huruma zinazotawala ardhi zetu na kusimamisha tena Khilafah inayotawaliwa na Khalifah muongofu atakayehudumu kama msimamizi wa watu wake kama alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt).
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |