Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  24 Shawwal 1444 Na: 1444 H / 036
M.  Jumapili, 14 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Damu ya Mashahidi Haitalipishwa Kisasi isipokuwa kwa Kutokomeza Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Takwimu zilizochapishwa na Wizara ya Afya huko Gaza mnamo Alhamisi alasiri zilionyesha kuwa wengi wa wahasiriwa wa hujuma inayoendelea ya Mayahudi kwenye Ukanda wa Gaza tangu alfajiri ya Jumanne ni watoto, wanawake na wazee. Jumla ya mashahidi waliokufa kutokana na uchokozi huu imefikia 25, huku idadi ya waliojeruhiwa ikifikia 76.

Kulingana na takwimu, 11 kati ya jumla ya wote waliokufa mashahidi walikuwa watoto, wanawake, na wazee (watoto 6, wanawake 3 na wazee wawili). Kwa upande wa waliojeruhiwa, zaidi ya nusu (40 kati ya 76 waliojeruhiwa) walikuwa watoto, wanawake, na wazee (watoto 24, wanawake 13, na wazee watatu wenye zaidi ya umri wa miaka 60).

Kuongezea hayo ni maangamivu na uharibifu mkubwa kwa makumi ya nyumba na vifaa ambavyo vilishambuliwa na uvamizi huo wakati wa uvamizi wake wa mara kwa mara kwenye Ukanda wa Gaza kwa siku ya tatu mfululizo.

Waathiriwa wa kwanza wa uvamizi huu walikuwa watoto 4 na wanawake 6 ambao waliuawa kwa khiyana wakiwa wamelala wakati ndege za kivita za Kiyahudi ziliposhambulia nyumba tatu salama za makaazi, saa nane usiku mnamo Jumanne. Ziliwalenga kwa msururu wa mashambulizi ya wakati mmoja, na hivyo kupoteza maisha ya mashahidi 13. Miongoni mwa waliolengwa ni viongozi 3 wa Brigedi za al-Quds, kitengo cha kijeshi cha harakati ya Jihad ya Kiislamu nchini Palestina.

Uvamizi huu wa kikatili na uhalifu wa kutisha sio wa kwanza kwa umbile la Kiyahudi, na hautakuwa wa mwisho. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kabla ya uvamizi huu wa hivi punde zaidi, Wapalestina 123 wameuawa mashahidi wakiwemo wanawake na watoto. Na watawala wa Waislamu wanaendelea na uadui wao na uzembe wao. Kila mmoja wao ana shauku ya kupata ridhaa ya Mayahudi na kulinda eneo lao ili kulinda viti vyao vya enzi (vya madaraka) na ufujaji wao wa mali ya Ummah. Pia, kwa sababu Ummah haufahamu njia ya kukomesha mauaji haya, ambayo ni kutokomeza uvimbe huu wa saratani katika mwili wa Ummah, ambao hautakuwa mikononi mwa watawala hawa Ruwaybidha (watepetevu), wala kwa juhudi za watu binafsi au makundi, bila kujali wana ujasiri na kujitolea kiasi gani, bali kwa harakati za majeshi za kuwaondoa watawala hao na kusonga mbele kuikomboa Palestina yote. Ummah utawaunga mkono kwa vijana, wazee, na wanawake wake ambao wana kiu ya ushindi na izza, hata kama watatoa maisha na mali zao kwa ajili hiyo.

Enyi Umma wa Uislamu: Je, haijatosha kwamba umbile la Kiyahudi limekiuka damu ya familia zenu, ndugu zenu, watoto wenu, wanawake, matukufu na adhama zenu huko Gaza, Al-Aqsa na Palestina yote? Hawa ndio Mayahudi waliowauwa Mitume na ni maadui wa Uislamu, na kama Mola Mtukufu anavyosema:

[قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ]

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Aal-i-Imran: 118].

Enyi Maafisa wa Majeshi ya Kiislamu: Ikiwa damu ya wanawake na watoto inayomwagwa kila wakati bila ya hatia au dhulma haikusukumini kuwalipizia kisasi, na ikiwa machozi na vilio vya kina mama na wake waliofiwa havichemshi damu tukufu ndani ya mishipa yenu, basi ni nini kitakachokufanyeni muhamasike na kuwaondoa watawala wenu, na musonge mbele kuwasaidia na kuwanusuru Waislamu mpaka ifikiwe kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“…Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [At-Tawba: 14].

Basi inukeni kwa pamoja ili kupata izza ya dunia hii na Akhera, na alichonacho Mwenyezi Mungu (swt) ni bora na ni cha milele.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu