Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 17 Sha'aban 1446 | Na: H 1446 / 088 |
M. Jumapili, 16 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marufuku ya Kyrgyzstan dhidi ya Niqab ni Jaribio la Kutapatapa la Utawala wake wa Kisekula Kukandamiza Kuibuka kwa Kitambulisho cha Kiislamu Miongoni mwa Watu wake
(Imetafsiriwa)
Kyrgyzstan imekuwa nchi ya hivi punde zaidi katika Asia ya Kati kupiga marufuku Niqab. Hatua hii ya kisheria ilianza kutekelezwa mnamo tarehe 1 Februari 2025 na ukiukaji huu utatozwa faini ya 20,000 som ($230). Nguo za Kiislamu za wanawake na ndevu za wanaume zimekuwa zikilengwa na serikali za Asia ya Kati kwa muda mrefu, ambapo dola zenye nguvu ya kisekula zinaogopa ushawishi unaoongezeka wa Uislamu. Wabunge wa Kyrgyzstan wametoa kisingizio duni kwamba marufuku hiyo inahitajika kwa sababu za usalama, ili nyuso za watu zionekane na watu binafsi kutambuliwa. Lakini wapinzani wanasema marufuku hiyo inawanyima wanawake uhuru wa kuvaa wanavyotaka.
Ingawa eneo hilo lina Waislamu wengi, marufuku hiyo inahalalishwa na marekebisho ya Sheria ya Nyanja ya Kidini. Hii ilitiwa saini na Rais Sadyr Japarov mnamo Januari 21. Haitaji niqab waziwazi, inayojulikana nchini humo kama "parandzha." Hata hivyo, inapiga marufuku "nguo zinazofanya kutowezekana kutambua mtu katika afisi za serikali na maeneo ya umma," msemo unaotumiwa katika Asia ya Kati kuelezea niqab. Vifuniko vya uso vinavyohitajika kama sehemu ya kazi au vinayovaliwa kwa ajili ya matibabu.
Katika mkanganyiko wa ajabu ambao ulitoa kisingizio kuwa wanaunga mkono Uislamu, wabunge na viongozi wa kidini wanaoungwa mkono na serikali walisisitiza kuwa marufuku hiyo haipanuki hadi kwa hijab, kitambaa cha kichwa cha Kiislamu ambacho hufunika nywele na shingo lakini huacha uso kuonekana. Kyrgyzstan ndiyo nchi pekee katika Asia ya Kati ambayo inaruhusu hijab katika shule na afisi. Nurlanbek Shakiev, spika wa bunge aliwaambia wabunge alipowasilisha mswada huo mwaka jana: “Hakutakuwa na vizuizi kwa kitambaa cha kichwa. Kina mama na dada zetu wamekuwa wakivaa hijab kama sehemu ya mila na dini yetu."
Ni wazi kwamba bila ya Khilafah hapawezi kuwa na usalama wa kujieleza Kiislamu na chochote kinaweza kuhalalishwa, hata Haramu. Wazo kwamba kuna aina fulani ya upendeleo - kwamba wanawake wa Kiislamu wanaweza kuvaa Hijab huku kina dada wengine wa Kiislamu wakilazimishwa kuacha imani zao za kidini kuhusu kuvaa Niqab - sio hatua nzuri ya kusherehekea. Uislamu unashambuliwa na hilo linawaathiri Waislamu wote. Viongozi wa upinzani wanaotaka kutetea "uhuru" wa wanawake wa Kiislamu kuvaa wanavyotaka pia sio faraja. Wanawake wa Kiislamu hawahitaji uingiliaji kati kutoka kwa uhuru huu wa kiliberali ambao unatokana na msingi ule ule na mfumo wa kisekula uliowapiga marufuku kuvaa kulingana na imani zao za kidini. Kamwe hakuna matokeo chanya kwa ajili ya utekelezaji wa kanuni za Kiislamu wakati maadui wa Uislamu wanakuja na ajenda zao za kirongo za uwezeshaji wa wanawake.
Ongezeko la wanawake wanaovaa niqab katika Jamhuri za Asia ya Kati ni kielelezo cha kuonekana cha kuongezeka la mshikamano wa wanawake wa Kiislamu kwa kitambulisho chao cha Kiislamu ambacho watawala wa kisekula wa tawala hizi wanajaribu sana kukikandamiza ili kuzuia kuzaliwa kwa mfumo wa kisiasa wa Kiislamu, Khilafah, katika eneo hilo. Mnamo mwaka wa 2023, mbunge Sharapatkanpe aloiongoza kampeni dhidi ya niqab baada ya kuzuru eneo la kusini la Osh, ambapo alisema alishangazwa na jinsi wanawake wengi wa eneo hilo walikuwa wakivaa niqab inayofinika kila sehemu, akisema, "Mwanamke mmoja kati ya wanawake wa nne huko Osh huvaa niqab, na idadi yao inaongezeka siku hadi siku."
Heshima ya mwanamke wa Kiislamu, vazi lake la Kiislamu na faradhi zake zote za Kiislamu hazitalindwa kikamilifu chini ya mfumo wowote isipokuwa utawala wa Kiislamu wa Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah kwa njia ya Utume. Mtume (saw) akiwa kiongozi wa dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina aliwadhihirishia Waislamu na watu wote uzito wa kulinda hadhi ya mwanamke wa Kiislamu na umuhimu wa vazi lake la Kiislamu pale alipolifukuza kabila la Banu Qaynuqa kutokana na kumnyanyasa mwanamke mmoja wa Kiislamu na kukiuka vazi lake la Kiislamu. Kwa hivyo, tunatoa wito kwa dada zetu Waislamu katika Jamhuri za Asia ya Kati na duniani kote kushikamana na imani zao zote za Kiislamu na kujiunga na kazi ya Hizb ut Tahrir ya kusimamisha dola hii tukufu ya Khilafah kwa haraka ambayo chini yake watapewa ulinzi kamili na nusra ya kutekeleza Dini yao kwa ukamilifu wake.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizbuttahrir.today |