Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 10 Rabi' I 1441 | Na: 1441 H / 006 |
M. Alhamisi, 07 Novemba 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna Sheria (Shari’) isipokuwa Sheria ya Mwenyezi Mungu na Hakuna Hukmu isipokuwa Hukmu Zake (swt)
(Imetafsiriwa)
Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, alitoa hukmu iliyoweka umri wa ndoa kwa jinsia zote kuwa ni miaka 18, isipokuwa katika kesi maalum kwa mujibu wa mahakama yenye uwezo.
Uamuzi huu unakuja baada ya msururu wa majadiliano na mapendekezo kutoka kwa Baraza la Mawaziri na ile inayoitwa miungano ya wanawake ambayo inajali haki za wanawake kama inavyodai, ili kufuata njia ya usekula (isiyokuwa na Dini) na ili kukaa mbali na hukmu za Uislamu na sharia ya Mwenyezi Mungu (swt). Awali, kulikuwepo na viashirio kama kuruhusu na hata kushajiisha sherehe, mbio ndefu, uimbaji na mashindano ya urembo ya mchanganyiko zikigongana na sharia za mirathi na usimamizi (Qiwama) na kuandaliwa mamia ya semina, mikutano, makala, warsha na masomo juu ya “kuwa makini katika ndoa za mapema” au ndoa za chini ya umri kama wanavyoziita.
Yote haya na mengineyo yalikuwa ni kwa ajili ya kutimiza maagizo ya Magharibi. Kama Waziri wa Mambo ya Wanawake ndani ya Mamlaka ya Palestina, Amal Hamad alivyosema: “Ndoa chini ya miaka 18 inakwenda kinyume na makubaliano ya kimataifa (CEDAW) na mila na mikataba ya kijamii na mikataba ya raia na haki za kisiasa na Makubaliano juu ya Haki za Mtoto na Sheria ya Mtoto, ambayo Baraza la Utungaji Sheria lilipitisha, ambayo ilizingatia kuwa umri wa utoto ni mpaka miaka 18.” Hamad alisema kwamba hatua hii inakuja katika muktadha wa kufanyakazi kulinda mshikamano wa mujtama na kupunguza kesi za talaka ndani ya jamii ambazo zimefika kiwango cha asilimia 50 kwa kundi la waliochini ya miaka 18.
Ole wenu! Mnawezaje kuvuka mipaka dhidi ya sharia za Mwenyezi Mungu (swt), anayesema ndani ya Kitabu Kitukufu:
[وَأَنْكِحُوا الْأَيَامَى مِنْكُمْ] “Na waozeni ambao hawajaolewa miongoni mwenu.” [An-Nur: 32].
“Aiyim” ni wanawake ambao hawajaolewa. Ushahidi ni jumla kwa kila mwanamke ambaye hajaolewa pasina na kufunga umri maalumu kwa ndoa. Kwa hiyo wewe ni nani kiasi kwamba unabadilisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kuvuka mipaka yake?! Mwenyezi Mungu (swt), ndiye Ambaye Pekee Anayevifahamu viumbe Vyake.
[أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ] “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, mwenye khabari?” [Al-Mulk: 14].
Unawekaje umri wa ndoa kuwa miaka 18 na kutunga sheria kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu ambayo imefanya kubalegh kuwa ndio mpaka baina ya kuhesabiwa au la, kwa kutahadhari kwamba msichana anaweza kuolewa hata kabla ya hedhi kwa mujibu wa aya:
[وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِنْ نِسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ...] “Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wao eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi” [At-Talaq: 4].
Inamaanisha kwamba msichana anaweza kuolewa kabla hajapata hedhi na sio tu kwa kuingia umri wa Takleef (kuhesabiwa). Idadi kubwa ya talaka inayoonekana sio kwa sababu ya kuolewa mapema. Lakini ni kwa sababu nyingi, ya umuhimu zaidi ni malezi yasiyokuwa sahihi kwa msichana. Hilo humfanya kutokuwa na uwezo wa kubeba majukumu ya nyumba ya mumewe na watoto kwa sababu hakulelewa kuwa mama na mke nyumbani bali alilelewa kama mfanyikazi na mshindani dhidi ya mwanamume katika maeneo ya kazi!
Enyi Watu wa Ardhi Tukufu:
Uislamu haukumlazimisha mwanamke kuolewa mapema, lakini inaruhusiwa kwa mujibu wa Uislamu. Na kufunga umri ni kutia ufisadi ndani yake. Lazima mupinge maamuzi haya ambayo ni fikra za Kimagharibi na ni ukiukaji wa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), na inaeneza uchafu ndani ya mujtama hususan katika zama hizi za uwazi, uhuru na kushajiishana kuwa na mahusiano nje ya mpangilio wa ndoa (uzinifu).
[إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ] “Kwa hakika wale wano penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [An-Nur: 19]
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |