Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 8 Muharram 1441 | Na: 1441 H / 001 |
M. Jumamosi, 07 Septemba 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ulazimishaji wa Wanawake wa Uyghur Kutobeba Mimba katika Kambi za Uchina: Mkono Mwengine wa Utawala huo Katika Kampeni Yake ya Mauaji dhidi ya Waislamu wa Turkistan Mashariki
Katika wiki za hivi karibuni, vyombo vikuu vya habari kama vile Gazeti la The Independent la UK vimechapishwa ripoti kutoka kwa wanawake wa Uyghur ambao walikuwa wametiwa korokoroni ndani ya kambi za mjumuiko ndani ya Turkistan Mashariki, kuhusu wanawake Waislamu wa Uyghur kwamba wamelazimishwa kutobeba mimba wakati walipokuwa kizuizini. Wafungwa wameeleza kuwa mara kwa mara walikuwa wakidungwa dawa wasizozifahamu ambazo baada ya muda hedhi zao zilisimama. Napia wameelezea kuagizwa kuvua nguo na maafisa wa gereza na kupitia mateso na aina nyingine za unyanyasaji. Hii ni kando na kujazwa katika sehemu ndogo zilizo na takribani wanawake 50 wengine, katika sehemu iliyo na kipimo cha futi 20 kwa futi 10. Awali kulikuwepo na ripoti nyingi za mamlaka ya Uchina ndani ya Turkistan Mashariki zinazolazimisha wanawake Waislamu wa Uyghur kufanyiwa uavyaji mimba hata kama zilikuwa zimepevuka. Taasisi ya Utafiti wa Watu ambayo inapigia debe kwa marufuku ya kuwepo kwa mipango ya kinyama ya kudhibiti idadi ya watu na kuilaumu Uchina katika kulazimisha kutobeba mimba kwa idadi kubwa ikisema, “Idadi ya sasa ya Uyghur iko chini ya asilimia 1 ya idadi jumla ya Uchina. Ili kuzuia na kudhibiti ukuaji wa kimaumbile wa idadi kwa kiwango hicho ndani ya nchi yoyote ni kuangamiza na mauaji kiujumla. Hivyo basi, sera ya kudhibiti uzazi ya Uchina ya kulazimisha uavyaji mimba na kutobeba kwa wa Uyghur sio sera ya kuhakikisha ubora wa idadi ya wa Uyghur. Kinyume chake ni kukimaliza polepole kwa kuwalazimishia vikwazo vya kisiasa, kiuchumi na kijamii.” Yote haya yakiwa ni ziada kwa mpango wa utawala wa Uchina katika kutoa ushajiisho wa kifedha kwa Wachina wa Han wasiokuwa Waislamu wanaume kuwaoa wanawake Waislamu wa Uyghur ili kuzaa watoto waliochanganya kizazi cha wa Han-Uyghur ili kuweza 'kuondosha' idadi ya Waislamu ndani ya Turkistan Mashariki. Ni kitendo kinachojulikana kama 'usafishaji wa chembe': sera ya uzazi inayolenga kusafisha kabila la wa Uyghur Waislamu.
Utawala dhalimu wa Uchina unaendelea kutekeleza njama ovu na za kutamausha za kimujtama ili kujaribu kufutilia mbali idadi ya Waislamu wa Uyghur ndani ya Turkistan Mashariki na utambulisho wao wa Kiislamu. Ilhali tawala dhaifu za ulimwengu wa Waislamu, zilizo na matumaini ya kulinda na kupanua maslahi yao ya kifedha na Beijing,wanaendelea kushirikiana na dola hii inayopinga Uislamu na Waislamu na ambayo inawakandamiza zaidi ya Waislamu milioni 1 waliomo ndani ya kambi zake za vizuizi ambazo ni sehemu ya kampeni yake ya kinyama ya kithaqafa ya kimauaji inayolenga kufutilia mbali alama za Uislamu ndani ya Turkistan Mashariki. Mwezi wa Julai, tawala kadhaa za Waislamu ikijumuisha Ufalme wa Saudi Arabia, UAE, Kuwait, Oman, Misri, Pakistan na Sudan, walitia saini barua ya wazi wakiunga mkono ya kile kisichoingia akilini iliyojulikana kama Uchina “kufaulu kwa hali ya juu katika haki za binadamu,”kimsingi wanaitetea Uchina katika mpango wake wa kukandamiza wengi kupitia upenyezaji wa fikra ya kishirikina ya kikomunisti kwa Waislamu wanaume,wanawake na watoto. Uongozi wa Pakistan pasina na aibu wanaipongeza Uchina katika Baraza la Haki za Wanadamu la UN “kwa kuwajali raia wake Waislamu” ilhali pia kuitenga kadhia la usafishaji wa kabila dhidi ya Waislamu wa Uyghur kuwa ni 'sera ya ndani' ya Uchina. Pia kuna ripoti za hivi karibuni kwamba Uturuki inawafurusha Waislamu wa Uyghur ikijumuisha wanawake ambao walikuwa wametafuta uhifadhi nchini humo, kuwarudisha katika mikono ya dola dhalimu, ili kuweza kutiwa korokoroni katika Gulag zao. Hakuna shaka, matarajio ya kupata mikataba ya mamilioni ya dolari pamoja na kuhamishwa kwa dolari bilioni 1 ndani ya mwezi wa Juni kutoka kwa Benki Kuu ya Uchina ili kuboresha hifadhi ya kubadilishana sarafu (kama ilivyoripotiwa na Bloomberg) inayo dori ya kucheza kwa Erdogan katika kuwasaliti zaidi Waislamu wa Uyghur. Kiuwazi ipo “kampeni kabambe endelevu ya mauaji ya mujtama na thaqafa” unaoendelezwa na utawala wa Uchina ili kukifutilia mbali kizazi cha Waislamu ndani ya Turkistan Mashariki haimaanishi kitu kwa tawala hizi za aibu na Waislamu waoga ambao wameuza roho zao kwa dolari. Hakika, maangamivu haya ya kithaqafa ya utambulisho wa Kiislamu wa ndugu zetu na dada zetu wa Uyghur na hairuhusiwi kuendelea! Hakika, ni lazima tuitikie maamrisho ya Mwenyezi Mungu wetu (swt) Aliposema,
(وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ) “Na wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [8:72]. Lakini njia pekee ya kutekeleza jukumu letu kwa Waislamu wa Turkistan Mashariki ni dharura kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume – kwa kuwa ndio uongozi wa kweli wa Kiislamu pekee ambao unao uwezo wa kisiasa kusimama dhidi ya dola yoyote ile ambayo ina watesa Waislamu na ambayo haitanunuliwa na pumbazo la utajiri! Bali itatumia kila zana yake iliyoko nayo kuweza kutia hofu ndani ya mioyo ya maadui wa Uislamu na kumuokoa kila Muislamu anayekandamizwa kutoka katika makucha ya wahalifu.
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |