Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  15 Dhu al-Qi'dah 1441 Na: 1441 H / 028
M.  Jumatatu, 06 Julai 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

            Kitengo cha Wanawake katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kimezindua Kampeni katika Kumbukumbu ya 25 ya Mauwaji ya Halaiki ya Srebrenica:
“25 Baadaye: Mafunzo kutoka Srebrenica”

Mnamo 11 Julai, 1995, majeshi ya Serb yalivamia eneo la Waislamu la Srebrenica nchini Bosnia ambapo maelfu ya Waislamu walikuwa wametafuta himaya kutokana na mashambulizi ya jeshi la Serbia kaskazini mashariki mwa Bosnia. Mji huo ulikuwa umetengwa na Umoja wa Mataifa (UN) kama "eneo salama" na kutangazwa kuwa chini ya ulinzi wa UN. Siku zilizo fuatia kutekwa kwa Srebrenica, wanaume na wavulana wa Kiislamu 8000 waliuwawa kinyama na Waserbia hao. Ilitangazwa kuwa ndio ukatili mbaya zaidi kufanyika katika nchi ya Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia. Sambamba na mauwaji haya, wanawake, watoto na wazee kati ya 25,000 na 30,000 walifurushwa kutoka mjini humo kama sehemu ya kampeni ya kikatili ya Kiserbia ya mauwaji ya kimbari ya Waislamu kutoka katika ardhi zinazo pakana na Jamhuri ya Serbia. Waislamu wa Srebrenica waliahidiwa ulinzi na Umoja wa Mataifa lakini ulinzi huo kamwe haukuja. Waliahidiwa kwamba serikali za kimagharibi zingesitisha mashambulizi ya Waserbia kupitia NATO lakini usaidizi huo kamwe haukuwa. Hakika, sio tu kwamba Umoja wa Mataifa ulishindwa kuzuia kutekwa kwa Srebrenica na mauwaji ya halaiki yaliyo fuatia, uliwapokonya zana za kijeshi wapiganaji wa Kiislamu wa Bosnia mjini humo, wakidhoofisha mikono yao dhidi ya adui yao. Katika kijiji cha Potocari, kambi nyengine ya kuweka amani ya Umoja wa Mataifa, maelfu ya Waislamu kutoka Srebrenica waliokuwa wanatafuta hifadhi kutokana na vikosi vinavyo songa vya Serbia, walikabiliwa na kampeni ya kigaidi mikononi mwa majeshi ya Serbia walioingia eneo hilo.

Waliwauwa mamia ya Waislamu, kukata koo za watoto na kunajisi idadi isiyo julikana ya wanawake na wasichana wa Kiislamu. Mwingi wa uhalifu huu ulishuhudiwa na vikosi vya UN vilivyo shindwa kuwazuia.

Miaka ishirini na tano baadaye kutokana na mauwaji ya kinyama ya Srebrenica, waathiriwa wa janga hili wangali wanasubiri haki dhidi ya maelfu ya wanajeshi wa Serbia waliotekeleza uhalifu huu mbaya zaidi dhidi yao na familia zao. Tamaa hakuna kwamba kamwe watashinda vita vyao vya kupata haki. Mauwaji ya halaiki ya Srebrenica ni mojawapo tu ya msururu wa ukatili unaofanywa na majeshi ya Serbia dhidi ya Waislamu wa Bosnia katika vita vya Bosnia huku serikali za ulimwengu - za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu – zikitazama.  Vita vya Bosnia vya miaka mitatu, kuanzia 1992 hadi 1995, vilionyesha mauwaji ya kimbari ya Waislamu katika mamia ya miji na vijiji huku pande zote za Waserbia nchini Bosnia na serikali ya Jamhuri ya Serbia ya Slobodan Milosevic ikitafuta kuunda rawaza yao ya kitaifa ya Serbia Tukufu, kwa eneo la Serbia lililo takata kutokana na ukabila kando kando ya Mto Drina.

Majeshi yao kwa mpangilio maalumu yalivunja majumba, na kuwakamata, kuwatesa na kuwachinja maelfu ya Waislamu kinyama, ikiwemo wanawake, watoto na wazee. Watu 100,000 waliuwawa wakati wa vita hivyo, 2.2 milioni wakikosa makao na wanawake na wasichana wa Kiislamu 50,000 walinajisiwa na majeshi ya Serbia, huku wengi wakitungwa mimba kutokana na uhalifu huo wa kinyama. Maelfu ya Waislamu wa Bosnia pia waliwekwa kizuizini katika kambi za mateso za Waserbia ambako walinyimwa chakula, kuteswa na kuuwawa.

Miaka kadhaa baada ya mauwaji ya halaiki ya Srebrenica, ulimwengu uliahidi, "Kamwe Haitatokea Tena" na kwamba mafunzo yatapatikana kutokana na doa hili jeusi katika historia ya sasa. Hata hivyo, leo tunaona chinja chinja na uhalifu wa vita vya Bosnia na mauwaji ya halaiki ya Srebrenica yakijirudia dhidi ya Waislamu katika ardhi kote ulimwengu… katika baadhi ya mifano ambayo katika mizani imepita Srebrenica. Pia tumeshuhudia mwendelezo wa ugumba na utepetevu wa UN, pamoja na serikali za Kimagharibi na za Waislamu, katika ukatili usio idadi unaotekelezwa dhidi ya Waislamu leo – ikiwemo Syria, Myanmar, Kashmir, Palestina, Yemen, Turkestan Mashariki na India.

Ili kukumbuka kumbukumbu ya 25 ya mauwaji ya halaiki ya Srebrenica, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni kwa anwani, "Miaka 25 Baadaye: Mafunzo kutoka Srebrenica" ili kuangazia mafunzo halisi yanayo paswa kusomwa kutokana na janga hili la kibinadamu na jinsi turathi hii ya mauwaji ya halaiki yaliyo usibu Ummah wetu itaweza kuvunjwa ili historia isiendelee kujirudia. Itazungumzia namna kumbukumbu ya matukio haya ya kinyama yaliyo pita yanapasa kutusaidia kuunda upya mustakbali wetu ili kunali usalama na haki kama Waislamu, ikiwemo nchi zetu. Hakika, Mtume (saw) amesema:

 «لاَ يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang'atwi katika tundu moja mara mbili.”  

Kampeni hii yaweza kufuatiliwa katika:

http://www.hizbuttahrir.today/en/index.php/hizbuttahrir/19753.html
https://www.facebook.com/WomenSharia/        

 Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu