Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  24 Jumada I 1444 Na: H.T.L 1444 / 04
M.  Jumapili, 18 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, almaarufu kama NGO, yanashirikiana na Huduma za Ujasusi za Kimataifa
(Imetafsiriwa)

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani wa Lebanon, Muhammad Fahmy, alifichua katika mahojiano kwenye Al-Jadeed TV ndani ya kipindi cha “Al-Ria'asa”, na katika habari iliyotumwa kwenye tovuti ya idhaa hiyo mnamo 11/13/2022 na kupeperushwa na tovuti kadhaa za habari, "kwamba uwanja wa Lebanon umeingiliwa na mashirika ya kijasusi ya kimataifa kupitia baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali" ambayo yana zaidi ya vyama 11,500 nchini Lebanon! Nusu yao yanafanya kazi chini ya mbawa za huduma za kijasusi za kimataifa, dhidi ya Lebanon... Hii ni habari iliyothibitishwa." Kwa hivyo, Lebanon ni ukumbi wa huduma za usalama wa kimataifa na mawakala wao na kisha wanazungumza juu ya ubwana, huria na uhuru!

Lebanon, tangu kuanzishwa kwake na Ufaransa ambayo iliitenganisha na Umma, haijajua uhuru, ubwana, au huri, bali kukaliwa, utumwa na vita. Hii hapa moja ya nchi tajiri kwa mafuta na gesi, ilhali inangoja Amerika kuipa kibali cha kuzichimba! Wakati huo huo, inaporomoka kiuchumi na inangojea suluhu za Kimagharibi kupitia joka la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia, na kuna nafasi ya rais ndani yake, na inangojea uteuzi kutoka ng’ambo, bali kutoka Amerika na ubalozi wake nchini Lebanon!

Fahamu ya dola nchini Lebanon haipo katika kila kitu isipokuwa katika kukamilisha uwekaji wa mipaka na umbile la Kiyahudi, na kulikabidhi robo ya utajiri wa maji wa Lebanon wa 2,500 km2, na mabilioni ya mita za ujazo za gesi, pamoja na ulinzi wa mipaka yake na wanaojifanya kuwa wapinzani, sio kuanzia leo bali tangu Julai 2006 vita na kutiwa saini kwa Mkataba wa 1701. Fahamu ya dola haipo katika kila kitu isipokuwa katika vita vyake dhidi ya Waislamu na kuwatupa jela bila ya mashtaka na tuhma za uwongo miaka na miaka, katika kuwatoza watu kodi na kuongeza ada za miamala, katika kumwachia mtawala wa benki kupandisha na kushukisha sarafu sio kupitia sheria na amri, lakini kupitia nyaraka tu, na kwa kuwatesa Waislamu kutoka miongoni mwa watu wa Syria, na kukaa kimya juu ya uvamizi dhidi ya watoto wao na familia ambazo zilitafuta hifadhi kwa ndugu zao nchini Lebanon ili kuepuka utawala wa Assad.

Enyi Waislamu wa Lebanon, miungano hii yenye kutiliwa shaka na miovu ni sehemu ya vita dhidi ya Uislamu na hukmu zake, na mashambulizi sasa ni makali dhidi ya dini yenu, heshima yenu na familia zenu. Basi kuweni pale ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amekuamrisheni kuwa, simameni dhidi ya batili na muiangamize, kwa kuongoza kampeni za kufichua, utambuzi, na mapambano ya wazi kwa jumuiya hizi na mielekeo yao, na wala msitegemee dola ya kinyonge ambayo imetoa leseni kwa maelfu ya jumuiya bila ya kuangalia na kujadili, kama Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani alivyosema, wala msifadhaike, kwani batili kwa maumbile yake ni yenye kutoweka  (إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً)“Hakika uwongo lazima utoweke!” [Al-Israa 17:81] lakini inahitaji mwendo wenu na hatua zenu.

Enyi Watu wa Lebanon: Jumuiya hizi zinalingania uovu na upotovu kama vile maovu ya watu wa Lut, upotovu unaoitwa ushoga, na ndoa ya kiraia, na kupatiliza ugumu wenu wa kiuchumi kununua dhamiri zenu kwa sarafu madhubuti, hasa miongoni mwa vijana wa kiume na wa kike na wenye ushawishi, hivyo msidanganywe na pesa zao au kauli mbiu zao za uwongo kama vile haki za wanawake na watoto, na usawa kati ya wanaume na wanawake, uhuru, demokrasia na nyenginezo zilizorithisha nchi yao yale mnayoyaona.

Na jihadhari na maneno yao maovu kama vile jinsia, aina (ya kijamii), wasifu, na mifumo ya kifamilia, ambapo wanataka kuunda aina nyengine kando na zile zilizoumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

(وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَى) “Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike.[An-Najm 53:45]. Wanafanya kazi ya kulazimisha mfumo wao wa maisha juu yenu, kuleta maafa yao kwenye nyumba zenu, na kisha kukiuka kile mnachokiamini zaidi katika suala la heshima na utakatifu. Wala msidanganywe nao, simameni dhidi yao pamoja nasi, na muwafichue kwa rai jumla mpaka washindwe miongoni yetu.

Tunakutangazieni kwamba dola yenu iko karibu, Mwenyezi Mungu akipenda. Dola ya Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, itakuonyesheni uhuru wa kweli, ubwana wa hali ya juu, na ukombozi kutokana na utiifu wowote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake (saw), na itakuonyesheni maana ya dola ya kweli kwa kutatua matatizo yenu na kushughulikia mambo yenu bila kujali dini, rangi na madhehebu, na itavifanya vyama hivyo vya kijasusi vya nje, vyenye saratani kuwa athari na somo kwa wale wenye macho. Basi kuweni pamoja na wanaokuwa makini nanyi, Dini yenu na utukufu wenu.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ)

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.” [At-Tawbah 9:119]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu