Ijumaa, 24 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  23 Sha'aban 1445 Na: H.T.L 1445 / 12
M.  Jumatatu, 04 Machi 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon:
Khilafah ndio Mkombozi wa Ardhi na Mtetezi wa Waja
(Imetafsiriwa)

Kwa mnasaba wa miaka mia moja ya kuanguka Khilafah Uthmani mnamo Machi 3, 1924, Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon ilifanya kongamano mjini Tripoli lenye kichwa: “Khilafah ndio Mkombozi wa Nchi na Mtetezi wa Waja.” Ukumbi wa kongamano ulijaa wahudhuriaji. Programu ya kongamano ilikuwa kama ifuatavyo:

Kwanza kwa usomaji mzuri wa aya za Mwenyezi Mungu kutoka Surat Al-Isra, zilizosomwa na Sheikh Khaled Seif.

Kisha, Dkt. Muhammad Jaber, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, akaanzisha kongamano hilo kwa hotuba ambapo alibainisha kwamba tatizo halisi la Waislamu linatokana na kutokuwepo mahali pa usalama kwa Waislamu, mlinzi wao na mtetezi wao mbele ya adui yao. Kutokuwepo Khilafah, na kazi hiyo ni sababu ya kujitolea, kwa matumaini kwamba kongamano lijalo litakuwa chini ya kivuli cha Khilafah na kwa kichwa “Kuiwezesha Khilafah.”

Ikifuatiwa na hotuba ya Ustadh Ahmed Al-Qasas ambapo alizungumzia umuhimu wa Bayt al-Maqdis kwa mtazamo wa mapambano yaliyomo baina ya hali na batili tangu bwana wetu Musa, amani iwe juu yake, na hadhi ya Bayt al-Maqdis katika Uislamu, na jinsi Khilafah ilivyoifungua katika zama za Al-Farouq Omar, na jinsi Khilafah ya Abbasiya ilivyoikomboa mikononi mwa kiongozi mtukufu Salahudin, na jinsi Khilafah Uthmaniya, hususan Khalifah Abdul Hamid II, alivyoihifadhi, na jinsi Bayt al-Maqdis ilivyoanguka baada ya kuanguka kwa Khilafah. Al-Qasas pia iligusia jinai ya umbile la Kiyahudi huko Gaza kwa msaada wa dola kubwa na madhalimu wa Kiislamu. Lau Waislamu wangekuwa na Khilafah, Mayahudi na wafuasi wao wasingesubutu kutekeleza mauaji haya.

Kisha hotuba ya pili ilikuwa ya Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, Mhandisi Salah Eddine Adada, ambaye alizungumza kuhusu minyororo ya vibaraka wa Kiarabu watawala wa Ummah, watu binafsi pamoja na watu wenye nguvu. Ummah unachemka na unangoja fursa ya kuwaondoa na kutawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu, akionyesha uwepo wa rai jumla miongoni mwa Ummah kuhusu kuikubali Khilafah na kusimamishwa kwake, akisisitiza uwezo wa Ummah wa kuikumbatia Khilafah.

Kisha kinda ya video iliyotayarishwa na Afisi Kuu ya Habari na Chaneli ya Al-Waqiyah ilionyeshwa, iliyotiwa moyo na tukio hilo na kufungamanisha matukio yanayotokea katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na dori ya majeshi.

Kisha Sheikh Ahmed Al-Sufi akazungumza kuhusu dori ya wanachama, wanazuoni, na majeshi, maafisa na viongozi wa Ummah, katika kujitahidi kusimamisha dola ya Khilafah ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu alituahidi na kwamba Mtume Wake Mtukufu (saw) aliitaja.

Kwa kumalizia, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon alisoma taarifa ya mwisho ya kongamano hilo, ambapo alisisitiza kazi ya Hizb na Ummah ya kuangamiza fikra na uhalisia wa Sykes na Picot zilizozigawanya nchi za Kiislamu. na kuwazuia kusaidiana wao kwa wao.

Vile vile alitilia mkazo kazi ya Hizb katika majeshi ya Ummah na akabeba mradi kwao kutekeleza wajibu wao wa kuwapindua watawala kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kurudisha madaraka kwa Umma.

Taarifa hiyo pia ilituma risala tatu:

- Kwa Waislamu ulimwenguni kwa jumla, na Waislamu nchini Lebanon haswa.

- Kwa watu wenye nguvu katika majeshi.

- Kwa wabebaji Dawah katika Hizb ut Tahrir, wakiongozwa na Amir wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, waheshimiwa wanachama wa afisi yake, na wale wanaofanya kazi katika kutafuta Nusrah kutoka kwa majeshi.

Taarifa hiyo ilimalizika kwa kuwashukuru waliohudhuria kwa kuitikia mwaliko huu, na pia alitoa shukrani za pekee kwa afisi kuu ya habari ya Hizb na idara ya televisheni inayowakilishwa na Chaneli ya Al-Waqiyah, kwa juhudi zao za kufanikisha kongamano hilo.

Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba matendo haya yatafikia kilele cha ushindi na afueni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa kusimamishwa Khilafah Rashidah ya Pili kwa Njia ya Utume, kuikomboa nchi na kuwatetea waja.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu