Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  4 Rabi' II 1446 Na: HTM 1446 / 09
M.  Jumatatu, 07 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umepita Mwaka Tangu Mauaji ya Gaza Huku Watawala wa Waislamu Wakisalia kama Watazamaji. Hakika Suluhisho Moja na la Pekee ni Khilafah!

(Imetafsiriwa)

Mauaji mjini Gaza yamefikia kumbukumbu yake ya mwaka wa kwanza tangu operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo Oktoba 7, 2023. Tangu wakati huo, mauaji ya kikatili ya Wapalestina yanayofanywa na wanajeshi wa Kiyahudi yameendelea bila kusitishwa, yakiambatana na vitendo vya kikatili vya kinyama na uharibifu mkubwa kwenye Ardhi Iliyobarikiwa. Uharibifu huu haujasaza hata wanyama, mimea, mawe, au miti. Licha ya mauaji yanayoendelea, Mayahudi hawajashinda wala kufanikiwa kufikia malengo yao huko Gaza. Kama kweli wangeshinda, wangesitisha mashambulizi yao na kutangaza ushindi kwa ulimwengu. Badala yake, mashambulizi yao ya mabomu ya anga na ardhini yanaonyesha wazi kwamba dhamira yao bado haijakamilika. Kwa Mapenzi ya Mwenyezi Mungu, uthabiti wa Waislamu nchini Palestina umedumu, ukiakisi imani yao isiyoyumba kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Ugaidi unaofanywa na Mayahudi mjini Gaza ni wa kutisha zaidi kuliko ulipuaji wa mabomu ya atomiki wa Mareka huko Hiroshima na Nagasaki. Hata hivyo, mandhari kubwa zaidi inatoka kwa watawala wa Waislamu ambao wamesalia kimya, wakishuhudia ukatili huu kwa karibu au kwa mbali. Wanashuhudia vifo vya Waislamu wenzao, kukaliwa kimabavu kwa ardhi yao, kuvunjwa kwa misikiti yao, na kunajisiwa ardhi ya Isra' na Mi'raj, huku wakiwa na uwezo kamili wa kukomesha ukatili huu kwa kufumba na kufumbua, lakini wanachagua kuwa watazamaji tu. Baya zaidi baadhi yao wanaendelea kutoa usaidizi kwa umbile la Kiyahudi na Marekani, na hivyo kuwezesha kuendelea kwa vitendo hivyo vya kigaidi na uharibifu. Ni tendo ovu lililoje!

Kiu ya Israel ya damu haiishii tu kwa Palestina. Wavamizi hawa katili sasa wameelekeza macho yao Lebanon, wakimwaga damu huko kama wanavyofanya nchini Palestina. Ilhali, watawala wa Waislamu, wakiwemo wale wa Lebanon, wananyamaza kimya. Iran, ambayo mshirika wake nchini Lebanon alishambuliwa, ilitaka kuonyesha ushujaa wake kwa kurusha makombora kwa 'Israel' katika jaribio la kusababisha “majeraha” madogo kwa umbile halifu. Kitendo hiki kilikusudiwa kutoa hisia kwamba Iran ilikuwa ikijibu uchokozi wa Mayahudi. Hata hivyo, Iran ilisitisha haraka vitendo vyake, na kuuhakikishia ulimwengu kwamba majibu yake yalizingatia sheria za kimataifa—sheria zilizowekwa na maadui zake! Hiki ndicho kiwango cha “kisasi” cha Iran dhidi ya adui ambaye amepoteza maisha ya viongozi wake wengi.

Usaliti wa watawala wa Waislamu dhidi ya Palestina ni dhahiri na wa kina, sio tu kwamba ni dhahiri katika mwaka huu mmoja, lakini tangu mwanzoni mwa uvamizi, na hata kabla ya hapo. Usaliti huu haukomei kwa mtawala mmoja pekee bali unaenea kwa wote, waliopita na wa sasa. Ilikuwa ni kwa usaliti wao ambapo Palestina iliteleza na kuingia mikononi mwa Wazayuni, na kwa sababu hiyo, Ardhi Iliyobarikiwa bado inakaliwa kwa mabavu hadi leo. Katika historia yote, Waislamu wameshuhudia orodha ndefu ya watawala katika nchi mbalimbali, lakini hakuna hata mmoja aliyejitahidi kwa dhati kuikomboa Palestina. Maarufu zaidi miongoni mwao ni wale wanaotoa hotuba bora zaidi za balagha, wakijaribu kuwahadaa watu wao ili waamini kuwa wao ndio mabingwa wa ukombozi wa Palestina.

Ukweli ni kwamba, hakujawa na mtawala hata mmoja ambaye kwa dhati anataka kummaliza Mzayuni na kuicha huru Palestina. Leo, tunashuhudia idadi ya vifo ikipita Wapalestina 40,000, huku wengine wengi wakijeruhiwa na kuyahama makaazi yao. Tunashuhudia uharibifu wa nyumba, misikiti, na majengo kwa aina mbalimbali za mabomu. Tunashuhudia mateso makubwa ya watu wa Palestina. Hata hivyo, pamoja na hayo yote, nyoyo za watawala wa Waislamu hazifunguki, hata kidogo, kutangaza Jihad dhidi ya umbile hilo halifu. Neno “Jihad” linaonekana kutoweka kwenye msamiati wao, na nyoyo zao zinaonekana kama zimekufa. Kama kweli wangetamani kuiregesha Palestina kwa ajili ya Waislamu, wangetayarisha na kuyakusanya majeshi yao kwa ajili hiyo. Walakini, hatua kama hiyo haijatekelezwa. Hakika hili limeshateremshwa kwetu na Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَٰكِنْ كَرِهَ اللَّهُ انْبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ]

“Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa!” [At-Taubah (9): 46].

Hivyo basi, enyi Waislamu, kwa kuzingatia kimya cha watawala wote na vikosi vyao vya majeshi, tunasisitiza kwamba suluhisho pekee la ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni kusimamishwa Khilafah. Hizb ut Tahrir inakulinganieni kwa dhati na bila kuchoka kushiriki katika kazi hii tukufu na ya dharura. Muna khiari ya ima kunyamaza, kuendelea kuwaunga mkono watawala wenu, au kuungana mikono na Hizb ut Tahrir katika kazi zetu za kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ama nyinyi, enyi majeshi ya Waislamu, mnaweza kuchagua kubaki kuwa waaminifu kwa watawala wenu wadanganyifu au kuinuka na kuwaondoa kwenye viti vyao vya starehe vya utawala na kutoa Nusrah yenu (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah. Baada ya kusimamishwa, Khalifa atakukusanyeni upesi kwenda Palestina, bila kuchelewa, InshaAllah. Mnapokwenda kupigana Jihad katika njia Yake, ushindi umekwisha hakikishwa—si na Hizb ut-Tahrir wala na Khalifa ajaye ambaye atakuongozeni, bali na Mola Mlezi wa walimwengu wote:

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawbah (9): 14].

Kwa hiyo, mnangoja nini, enyi majeshi ya Waislamu? Mna wasiwasi gani? Mnataka nini zaidi? Tayari Saad bin Muadh amepata heshima yake kwa kumpa Nusrah Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kitendo muhimu sana kilichopelekea kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu mjini Madina, ikiwezesha dini ya Mwenyezi Mungu (swt) kutekelezwa kwa ukamilifu wake, ndani na nje, kupelekea ushindi wa Uislamu kote ulimwenguni. Tunaomba kwa dhati kwamba Saad bin Muadh mpya atainuka miongoni mwa majeshi ya Waislamu katika zama hizi, ambaye, kupitia Nusrah yake, atasaidia kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na kurudisha utawala wa Kiislamu duniani.

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu