Afisi ya Habari
Malaysia
H. 29 Rabi' II 1446 | Na: HTM 1446 / 11 |
M. Ijumaa, 01 Novemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Demokrasia Humpa Mwanadamu, Wakiwemo Wasiokuwa Waislamu, Uwezo wa Kufafanua na Kubainisha Imani na Madhehebu Yetu!
(Imetafsiriwa)
Pendekezo la hivi majuzi la Mswada wa Sheria ya Mufti 2024 (Maeneo ya Shirikisho) limezua mjadala mkali kote nchini Malaysia. Tangu kusomwa kwake kwa mara ya kwanza mwezi Julai, Mswada huo umesonga mbele, ukikaribia kusomwa mara ya pili na ya tatu kabla ya kuidhinishwa kamili na bunge. Mwanzo wa Mswada huu unatokana na mjadala unaoendelea kuhusu Ilm al-Kalam (Usomi wa Kiislamu), ambao umeongezeka hivi karibuni nchini Malaysia. Una wasiwasi kwamba, wakati Palestina inakabiliwa na uhasama mbaya kutoka kwa Mayahudi (La’natuLlah alaihim), baadhi ya mamlaka na makundi ya kidini ndani ya Malaysia yamezama katika mijadala ya kitheolojia huku wabunge wakiwa katika harakati za kuidhinisha sheria zinazohusiana.
Mswada wa Sheria ya Mufti (Maeneo ya Shirikisho) wa 2024 una uzito mkubwa, hasa kwa vile unatafuta kufafanua kisheria “Ahl As-Sunnah wa Al-Jamaah” na kuzuia tafsiri yake kwa mifumo maalum ya kitheolojia. Hasa, unaweka masharti kwa wale wanaoshikamana na shule za Ash'ari na Maturidi katika itikadi (Aqidah), Dhehebu la Shafie katika fiqh (au, katika hali maalum, madhehebu ya Hanafi, Maliki, au Hanbali, au, kile kinachoamuliwa na Kamati ya Fatwa), na Imam Junaid al-Baghdadi na Imam al-Ghazali katika Usufi (Sehemu ya 3). Sharti hili linapendekeza kwamba wale wanaotofautiana na mafundisho haya maalum wanaweza kuchukuliwa kuwa nje ya “Ahl As-Sunnah wa Al-Jamaah” - kuwaainisha kwa ufanisi kuwa ni wapotovu.
Kupunguzwa kisheria kwa “Ahl As-Sunnah wa Al-Jamaah” kunaleta tishio kubwa kwa umoja wa Waislamu. Inaonekana kana kwamba Mamlaka ya Kidini, wakiwa wasanifu wa sheria hii, wamepuuza mafunzo kutoka kwa mifarakano iliyopita, kama vile yale yaliyochochewa na Ilm al-Kalam, na vile vile hatua yenye utata ya Khalifa Al-Ma'mun, ambaye alimfunga na kumtesa Imam Ahmad kwa ajili ya kupinga kanuni ya kitheolojia iliyoamriwa na dola. Hatua kama hizo za kulazimisha hutumika tu kuimarisha “ubabe” ndani ya utawala wa kidini.
Ajenda msingi ya Mswada huu inaonekana kukandamiza maoni yoyote pinzani ya kitheolojia. Kwa kuweka msimbo jambo hili, wale walio madarakani hawakuwalazimisha tu watu kushikilia imani na madhehebu maalum, lakini pia wanatishia kwa udhahiri “kuwaadhibu” wale wanaojitenga nayo. Zaidi ya hayo, Mswada unatoa kinga dhidi ya hatua zozote za kisheria kwa Mufti, Naibu Mufti, Mshauri wa Imani, na Kamati zinazohusika (Kifungu cha 32), na hivyo kuwaweka nje ya uwezo wa kuwajibika kisheria kwa yale waliyofanya ndani ya upeo wa Mswada huo. Je, wanajaribu kujiweka kama kipote cha wasomi ambacho kiko juu ya sheria, wanaojiepusha na uwajibikaji wa makosa yao? Upekee huu unaonekana kukinzana na kanuni za uwazi na uwajibikaji, kama ilivyoonyeshwa na Mtume (saw) katika Hadith inayotutahadharisha dhidi ya utekelezaji usio na usawa wa haki kati ya walio wanyonge na wenye nguvu.
Wasiwasi mwingine ni tabia ya kiholela ya baadhi ya masharti, hasa yale yanayohusiana na kutoa Fatwa. Huku taratibu zikiwepo kwa ajili ya utoaji wa Fatwa (Kifungu cha 10), lakini ikiwa Kamati ya Fatwa itaona mtu binafsi au kikundi kiko nje ya “Ahl As-Sunnah wa Al-Jamaah” au kuwaainisha kuwa ni wapotovu, hakuna sharti la kupata maelezo au ufafanuzi (Tabayyun) kwa wahusika. Mamlaka hii ya upande mmoja ya kufafanua na kuamua ukweli bila kusikiliza pande zinazohusika, itasababisha kuhujumu haki na utaratibu unaofaa.
Zaidi ya hayo, utoaji wa Fatwa juu ya Ahkam Ash-Shariah (hukmu za Mwenyezi Mungu) umebanwa na (kifungu cha) kushikamana tu na Dhehebu la Shafie pekee (Sehemu ya 16). Takhsisi inatolewa tu katika kesi ambapo inapingana na maslahi ya umma, hapo madhehebu mengine yanaweza kuregelewa. Ingawa, maumbile asili ya Fatwa au Ahkam ash-Shariah yanadai kwamba zichukuliwe kwa kuzingatia nguvu za Dalili (ushahidi), badala ya kushikamana na Dhehebu moja. Wanazuoni wenyewe wamehimiza kushikamana na rai yenye nguvu zaidi, si kujifunga na kanuni moja. Je, wasanifu wa Mswada huo hawajui kanuni hizi za kimsingi? Kwa nini wanatafuta kuuwekea mipaka Uislamu wakati Mwenyezi Mungu (swt) Mwenyewe aliupanua?
Maana pana na yenye athari zaidi, hata hivyo, iko ndani ya mfumo wa demokrasia yenyewe, mfumo unaoruhusu wanadamu-bila kujali imani au dini-kuamuru itikadi ya kidini au madhehebu, juu yetu! Kupitia mfumo huu, wabunge wakiwemo wasiokuwa Waislamu wanawezeshwa ipasavyo, kushawishi na kutunga sheria ni aina gani ya mkondo wa imani na madhehebu ambayo Umma huu lazima ufuate!! Hili ni dosari ya kimsingi ya mfumo wa kidemokrasia mbele ya Uislamu, ambapo ubwana ni kwa wanadamu, na kuwawezesha kutunga sheria hata katika masuala ya imani na Shariah. Chini ya mfumo huu, wabunge, bila kujali dini, elimu ya dini, wajinga, au hata wasioamini Mungu, wanakuwa na mamlaka sawa na haki ya kupiga kura, hivyo wana mamlaka na haki katika kuunda imani na matendo ya kila Muislamu!!
Hizb ut Tahrir / Malaysia inapenda kutangaza kwamba dola haipaswi kutekeleza mfumo maalum wa kitheolojia au dhehebu kwa raia wake. Imani na msimamo wa kitheolojia unapaswa kuamuliwa na Waislamu wenyewe kwa kuzingatia nguvu ya vyanzo vyenye mamlaka. Kuainisha mafundisho maalum kama sera ya serikali kunahatarisha kuiwekea mipaka dini ya Uislamu yenyewe. Tunapenda kusisitiza kwamba neno itikadi (Aqidah) limenasibishwa kwa Maimamu fulani kama vile “Itikadi ya Ash’ari”, “Itikadi ya Maturidi”, “Itikadi ya Salafi”, “Itikadi ya Tahawi”, “Itikadi ya Wasatiyya” na kadhalika, kwa hakika sio sahihi na ni kumepotea, na ni mkanganyiko na mgawanyiko miongoni mwa Waislamu. Hii ni kwa sababu msimamo wa Madhehebu katika masuala yanayohusiana na somo la itikadi sio itikadi yenyewe, bali itikadi hiyo ni “itikadi ya Kiislamu” (“Al-Aqeedah Al-Islamiyyah”) iliyoasisiwa katika Shariah kwa dalili za uhakika, na ni haramu kuwa na tofauti ndani yake.
Katika hali ambapo kikundi au mtu binafsi anachukuliwa kuwa amekengeuka kutoka kwa imani ya Kiislamu, hili lazima lithibitishwe na ushahidi wa wazi kutoka katika Qur'an na Sunnah katika mahakama ya sheria. Ikithibitishwa kuwa wameasi, ni lazima waombwe na wapewe nafasi ya kutubu; wakikataa, basi watakabiliwa na adhabu katika Uislamu - kifo.
Mfumo wa sasa wa kidemokrasia umejidhihirisha mara kwa mara kuwa na madhara kwa imani, hasa kwa vile unaruhusu misingi ya kidini kupigiwa kura, hata na makafiri. Mambo ya Aqidah na Shariah ni ya msingi; yanapaswa kuzingatiwa na kutekelezwa na Waislamu na dola, kwa mujibu wa Quran na Sunnah, sio chini ya idhini ya bunge. Ni wazi kwamba Ummah unahitaji haraka Khilafah kama suluhisho halali—muundo wa utawala unaotekeleza Quran na Sunna juu ya watu wake, unaozuia migawanyiko inayochochewa na hitilafu za kitheolojia na mijadala iliyofunguliwa na Mutakallimin tangu wakati huo.
Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Malaysia |
Address & Website Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor Tel: 03-8920 1614 www.mykhilafah.com |
Fax: 03-8920 1614 E-Mail: htm@mykhilafah.com |