Jumatano, 12 Safar 1447 | 2025/08/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  6 Safar 1447 Na: 1447/09
M.  Alhamisi, 31 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Magereza ya Misri: Kati ya Mateso na Mauaji
Pindi Heshima Inapokanyagwa Haki Huuawa!
(Imetafsiriwa)

Katika tukio jengine la mara kwa mara la uhalifu uliofichwa, kijana mmoja aitwaye Ayman Sabry alikufa ndani ya kituo cha polisi katika Jimbo la Dakahlia kutokana na mateso ya kikatili, ambayo yaliacha alama wazi kwenye mwili wake. Chini ya masaa 48 baadaye, kijana mwengine alikufa ndani ya Kituo cha Polisi cha Al-Saff katika Jimbo la Giza, huku kukiwa na ripoti thabiti za kutelekezwa kimakusudi, dhulma, na ukatili, na kuvigeuza vituo vya polisi kuwa sehemu za vifo cha polepole.

Kama kawaida, utawala wa Misri ulikanusha kuhusika kwa vyovyote vile, ukidai kwamba vifo vyote viwili vilitokana na "sababu za kimaumbile" licha ya ushuhuda wa mashahidi, picha zilizovuja, na hali ya miili hiyo, ambayo yote yanathibitisha kuwa waliteswa. Hivi kwa nini wahusika kamwe hawawajibikishwi? Kwa nini hakuna uchunguzi wa kina na wa uwazi? Kwa nini kesi hufungwa kila wakati kwa maneno "hakuna msingi wa kuleta mashtaka"? Kwa nini serikali inasisitiza kuwalinda na kuwaondolea hatia wahalifu, isipokuwa ni mpangaji mkuu na mtekelezaji wa jinai hizi?

Vifo katika vituo vya polisi na magereza si vya pekee tena au matukio ya kipekee; vimekuwa muundo wa kimpangilio, unaoungwa mkono na chombo cha usalama ambacho hakiogopi kuhisabiwa na hakina kizuizi. Mbali na kupotevu kwa nguvu kunakotekelezwa, kuwekwa kizuizini kiholela, na kunyimwa kesi za haki, vituo vya uzuizini vimekuwa vitovu vya udhalilishaji na umalizaji.

Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, vituo vya polisi vya Misri vinashuhudia hali mbaya kizuizini, makumi ya wafungwa wamesongamana katika vyumba vidogo visivyostahiki hata kwa wanyama, wakinyimwa huduma za matibabu, na kuteswa kama njia ya udhalilishaji au kukiri makosa yao kupitia vurugu.

Hili linagongana na kile Uislamu umekiweka kama wajibu wa dola kwa raia wake. Katika Uislamu, serikali ina jukumu la kulinda maisha, utu na heshima. Pindi dola inapokuwa ni chombo cha dhulma na upanga unaoshikiliwa dhidi ya watu wake yenyewe, inaisaliti amana, inakiuka agano, na inakuwa adui kwa raia wake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mtume (saw) alitahadharisha juu ya hatari ya viongozi wanaowabebesha mizigo au kuwadhulumu watu wao, akasema: «اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ» “Ewe Mwenyezi Mungu, yeyote anayetawalishwa juu ya mambo ya umma wangu akawafanyia uzito, basi nawe mfanyie uzito, na yeyote anayetawalishwa juu ya mambo ya umma wangu akawafanyia upole, basi nawe mfanyie upole.” (Imepokewa na Muslim)

Hii ni dua kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) dhidi ya wale wanaoudhulumu Ummah na kufanya kiburi, basi vipi kuhusu wale wanaoutesa na kuua kwenye magereza? Vipi wale wanaogeuza vituo vya polisi kuwa sehemu za kulipiza kisasi badala ya haki?

Miongoni mwa majukumu ya dola katika Uislamu ni:

Kuhifadhi uhai na heshima, kama alivyosema Mtume (saw): :«إِنَّ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ حَرَامٌ عَلَيْكُمْ كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا فِي شَهْرِكُمْ هَذَا...» “Hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni takatifu na ni haramu kukiukwa kama utakatifu wa siku yenu hii katika mwezi wenu huu” (Imepokewa na Bukhari na Muslim)

Kuwahisabu maafisa wa dola kabla ya mtu mwengine yeyote, kama inavyoonyeshwa na Khalifa Rashid (Khalifa Aliyeongoka) Umar ibn al-Khattab (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye alisema: “Tangu lini mnawafanya watu kuwa watumwa wakati mama zao waliwazaa wakiwa huru?”

Kusimamisha uadilifu kwa wote, bila ya ubaguzi au kinga, kwani kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu hakumtengi dhalimu, bila kujali madaraka yake.

Lakini uhalisia wa leo unathibitisha kwamba dola ya Misri inawalinda watesaji, inawatuza kwa kupandishwa vyeo na mafao, wakati wale wanyoofu, waheshimiwa, na watetezi wa kutabikishwa kwa Uislamu wanakandamizwa, wanafungwa jela, wanapandikiziwa kesi, na kuhukumiwa kwa dhulma.

Enyi Wanajeshi wa Kinanah: Nyinyi ni zana na wawezeshaji wa serikali hii, washirika katika dhambi zake, ima kwa kushiriki katika uhalifu au kunyamazia kimya juu yao. Mtume (saw) amesema:

«مَنْ أَعَانَ ظَالِماً لِيُدْحِضَ بِبَاطِلِهِ حَقّاً فَقَدْ بَرِئَتْ مِنْهُ ذِمَّةُ الله وَذِمَّةُ رَسُولِهِ»

“Mwenye kumsaidia dhalimu ili ashinde madai ya haki basi amejitenga na ulinzi wa Mwenyezi Mungu na ulinzi wa Mtume wake.” (Imepokewa na Ahmad)

Basi musiwe fimbo katika mikono ya madhalimu. Kuweni vile Mwenyezi Mungu alivyokukusudieni, askari wanaoulinda Umma, sio kuushambulia; wanaolinda damu yake, sio kuimwaga; wanaofanya kazi ya kusimamisha Sheria yake, sio kuwalinda madhalimu.

Simameni juu ya wajibu wenu, na timizeni faradhi ya nusrah, na kuweni waungaji mkono wa haki, mkiregesha Uislamu mahali pake panapostahiki, Khalifah katika uhalisia wake, na uadilifu katika ardhi ambayo umetoweka.

[إِنَّ اللهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالإِحْسَانِ وَإِيتَاء ذِي الْقُرْبَى وَيَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاء وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani,na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.” [Surat An-Nahl: 90]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu