Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  10 Rajab 1445 Na: 1445 / 30
M.  Jumatatu, 22 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hata kama Serikali zote za Magharibi na Mawakala wao katika Ulimwengu wa Kiislamu Wataipiga Marufuku Hizb ut Tahrir, Hizb ut Tahrir Itasimamisha Tena Khilafah na Kung'oa Mfumo wa Kilimwengu wa Magharibi, Kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu (swt)

(Imetafsiriwa)

Gazeti mashuhuri zaidi la lugha ya Kiingereza nchini Pakistan, Gazeti la ‘The Dawn’ liliripoti kupigwa marufuku kwa Hizb ut Tahrir nchini Uingereza, likiwa na kichwa, “Uingereza yapiga marufuku Hizb ut Tahrir kama kundi la kigaidi.” Imezua mdahalo na mjadala ndani ya mitandao ya kijamii na duru zenye ushawishi. Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan hivyo inawasilisha nukta zifuatazo kwa watu wenye nguvu na ushawishi nchini Pakistan kwa ajili ya mazingatio,

1. Ni “mama” wa demokrasia na kitovu cha “huria,” Uingereza ambayo imepiga marufuku chama cha kisiasa cha kimataifa cha Kiislamu Hizb ut Tahrir. Kwa hivyo, Uingereza imezika madai yake yote ya uhuru wa kujieleza katika 10 Downing Street, London. Uamuzi huu ulikuja kama mshtuko kwa wasomi wa Kimagharibi na waangalizi wa kisiasa. Hizb ut Tahrir inajulikana kwa mapambano yake yasiyo ya kijeshi, ya kifikra na ya kisiasa kwa zaidi ya miaka sabiini. Idadi kubwa ya wanafikra mashuhuri zaidi duniani, serikali, mashirika ya haki za binadamu, mahakama na vyombo vya habari, vyote vimeshuhudia ukweli huu mamia ya mara. Hata uchunguzi wa serikali yenyewe ya Uingereza zaidi ya nusu dazeni unashuhudia hili. Kupiga marufuku huku kuna nia iliyopotoka ya kisiasa, kwa mtindo wa ujanja wa wanasiasa wa Uingereza, badala ya sababu nzuri za kisheria au uhalali wa wazi wa kimaadili.

2. Kwa kupigwa marufuku huku, ni wazi kwamba Hizb ut Tahrir imeilazimisha hadhara ya Kimagharibi, kukubali kushindwa ndani ya himaya ya kifikra na kisiasa. Marufuku hiyo imeweka wazi kuwa uhuru wa kujieleza unakubalika maadamu Waislamu hawaupingi mfumo dhalimu Kimagharibi. Pia ni tangazo la kushindwa kwa ukuu wa kifikra wa hadhara ya Kimagharibi. Hapo awali ilitoa uhuru wa kujieleza kwa vyama vyenye fikra nyengine zote, ziwe za kikomunisti au za kisoshalisti, kwa sababu waliamini kwamba hadhara ya Kimagharibi, kwa sababu ya “ukuu” wake ingeshinda fikra nyingine zote. Waliamini hadhara ya Kimagharibi italazimisha vyama vyote kushindwa kifikra na kusalimu amri. Hata hivyo, mbele ya fikra za kweli, zenye nguvu, zenye kukinaisha za Uislamu, Uingereza haikuona njia nyingine isipokuwa kupiga marufuku, kudhibiti na kukandamiza. Vyovyote iwavyo hivi karibuni, serikali ya Uingereza iliyofanya kazi pamoja na washirika wa Kiarabu na Kituruki, kuiangamiza Khilafah mnamo Rajab 1342 H sawia na Machi 1924 M, itaona kurudi kwa Khilafah, ambayo itaipa Uingereza jibu inalostahiki mno na lililopita muda wake, kwa upotovu wake.

3. Hizb ut Tahrir inachukulia kuwa ni heshima kwamba imesimama imara katika kutoa wito wa kuhamasishwa majeshi kwa ajili ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Hakuna vikwazo au marufuku zinazoweza kusimama katika njia ya wajibu wake wa Kiislamu. Hizb ut Tahrir itaendeleza mapambano yake kwa nguvu ile ile. Marufuku ya kwanza ya Hizb ut Tahrir ya John Bagot Glubb, pia iliwekwa na Uingereza. Luteni Jenerali John Bagot Glubb wa Uingereza, (“Glubb Pasha”), Mkuu wa Majeshi ya Jordan alihakikisha kupigwa marufuku kwa shughuli za Hizb ut Tahrir nchini Jordan. Hata hivyo, licha ya marufuku hii ya mapema, na kupigwa marufuku kulikofuata na mawakala wa Magharibi katika Ulimwengu wa Kiislamu, Hizb ut Tahrir imefikia zaidi ya nchi arubaini za Kiislamu. Ni chama kikubwa zaidi cha kisiasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana kuhamasisha majeshi ya Waislamu, wakiwemo wale wa Pakistan, Uturuki, Jordan na Misri, kuinusuru Gaza na Palestina. Hii ni licha ya ukweli kwamba shughuli za Hizb ut Tahrir tayari zimepigwa marufuku na wengi wa vibaraka wa nchi za Magharibi katika Ulimwengu wa Kiislamu. Kwa hivyo marufuku mpya haitaleta tofauti yoyote kwa shughuli zetu. Baada ya miongo kadhaa ya kazi, katika makumi ya nchi, Mashababu wa Hizb ut Tahrir wanajua vyema kwamba Mwenyezi Mungu (swt) daima hufungua milango mipya na bora kwa Dawah, wakati wowote milango inapofungwa katika njia ya Dawah.

4. Fikra ya uhuru wa kuzungumza ni fikra dhaifu, ya uongo na batili. Inatokana na mvutano wa kisekula wa uhuru kutoka kwa dini. Fikra hii ndiyo silaha ya Magharibi ya kukufuru, na kukashifu maadili ya kidini. Imethibitisha kutofaulu katika kuwahisabu watawala, pamoja na kuilinda jamii dhidi ya mawazo ya kirongo, yenye kudhuru. Hilo pia liko wazi kutokana na kupigwa marufuku juu ya Hizb. Msingi wa mapambano ya kisiasa na kifikra katika Uislamu ni jukumu tukufu la kuamrisha mema na kukataza maovu. Huu ndio msingi wa Shariah wa mapambano ya Hizb. Msingi huu unaweka wajibu wa kidini wa kusema dhidi ya ukafiri, ukandamizaji na batili. Hakuna vikwazo au udhibiti unaodhibiti au kubatilisha wajibu huu. Wajibu huu hauwezi kupuuzwa kwa msingi wa kuogopa madhara kutoka kwa madhalimu. Hakika mapambano katika njia ya wajibu huu yana thawabu kubwa, pale neno la haki linapoinuliwa mbele ya watawala madhalimu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةَ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad bora ni kusema neno la haki mbele ya mtawala dhalimu.” (Abu Daawuud). Kwa hiyo, mapambano ya Hizb yanazidi kusonga mbele, kiasi kwamba viti vya vibaraka wa Magharibi katika Ulimwengu wa Kiislamu vinatikisika kabla ya kuporomoka, kikiwemo kiti cha enzi cha mwana mcheza kamari wa mwanamke Muingereza, Mfalme wa Jordan.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Magharibi imeonyesha wazi chuki yake dhidi ya Uislamu, Khilafah na Jihad. Hizb ut Tahrir ndicho chama pekee cha Kiislamu ambacho kimejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya kutabikisha njia badali ya Kiislamu ya mfumo dhalimu wa kilimwengu wa Kimagharibi. Hivi sasa, kuna pambano moja tu kali la kimfumo linaloendelea duniani, vita baina ya Uislamu na ukafiri. Hata hivyo, uongozi wenu ni mtiifu kwa makafiri, kwa kushirikiana na mfumo wa kisiasa wa Kimagharibi katika vita hivi. Tunaweza kushinda vita hivi iwapo tu mutauondoa uongozi huu na kutoa Nusrah (msaada) kwa Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Hapo pekee ndipo munapoweza kuwakomboa Waislamu wa Gaza kutoka kwenye makucha ya Mayahudi. Kusimama Khilafah ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wetu (saw). Ima mutekeleze wajibu wenu, au wengine mithili yenu watafanya, leo au siku inayofuata, au punde tu baada ya hapo. Kwa hivyo, ni nini kinakuzuieni kufikia heshima hii kubwa? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [Surah Al-Noor 24:55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu