Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  11 Ramadan 1445 Na: 1445 / 40
M.  Alhamisi, 21 Machi 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhuisha Udugu wa Kiislamu, Khilafah Rashida Itawahamasisha Waislamu wa Jeshi la Pakistan na Maeneo ya Kikabila kwa ajili ya Ushindi dhidi ya Makafiri

(Imetafsiriwa)

Damu takatifu ya Waislamu ilimwagwa katika mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan wakati wa mapigano makali kati ya Waislamu wa Jeshi la Pakistan na Waislamu wa maeneo ya makabila. Mnamo tarehe 17 Machi, tulipoteza vikosi saba vya Jeshi la Pakistani. Kisha mnamo tarehe 18 Machi, tulipoteza Waislamu zaidi, wakati Jeshi la Anga la Pakistan lilipopiga mabomu ndani ya Afghanistan. Kisha tukapoteza Waislamu zaidi wakati Taliban wa Afghanistan walipopiga makombora ndani ya Pakistan. Tulipoteza makumi ya Waislamu katika siku hizi za Ramadhan, huku tukipoteza maelfu katika miaka mingi ya mzozo huu kati yetu. Hakuna upande unaorudi nyuma na pande zote mbili zinapoteza waumini. Hii ni huku Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye anapendwa na pande zote mbili, akisema:

«قَتْلُ الْمُؤْمِنِ أَعْظَمُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ زَوَالِ الدُّنْيَا» “Kumuuwa Muumini ni jambo kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kuangamia kwa dunia nzima.” [An-Nasa’i]. Hii, enyi Waislamu, haijalishi Muumini amezaliwa wapi, au ni wa kabila gani. Hivi ndivyo ilivyo na jinsi inavyopaswa kuwa. Sio kama mkuu wa jeshi la Pakistan alivyosema, aliposema, mnamo tarehe 24 Januari, "Pindi usalama wa kila Mpakistani unapokuwa uko hatarini, Afghanistan inaweza kushitumiwa na kulaaniwa kwa ujumla.” Hakika sivyo!

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistani na Maeneo ya Kikabila! Vunjeni upanga wowote unaoelekeza kwa Muislamu. Elekezeni upya silaha zenu kwa maadui zetu halisi, dola zenye chuki za makafiri, ambao wanapigana nasi wote, na kumiliki ardhi zetu. Ni dola hizi za kikafiri ndio ambazo zinataka mzozo wetu uendelee. Zinasimama nasi, tunapopigana wenyewe kwa wenyewe. Tazama, jinsi balozi wa Marekani alivyokutana na Rais Zardari, kueleza kuunga mkono vita. Mnamo tarehe 18 Machi, taarifa kwa vyombo vya habari ya ubalozi wa Marekani ilisema, “Balozi aliwasilisha rambirambi zake kwa kupoteza wanajeshi wa Pakistan katika shambulizi la kigaidi la hivi majuzi huko Waziristan na kumhakikishia Rais, Marekani itasimama pamoja na Pakistan katika mapambano yake dhidi ya ugaidi.” Makafiri wanashajiisha mapigano yetu sisi kwa sisi kote katika Ulimwengu wa Kiislamu, kutoka Sudan hadi Pakistan, huku mabalozi wa Marekani wakichochea na kuchochora, kama vile mnong'ono wa Mashetani. Nguvu na uwezo wetu haziko nje yetu sisi wenyewe. Zipo ndani yetu, kama udugu wa waumini. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah an-Nisa'a 4:139].

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan na Maeneo ya Kikabila! Vita kati yetu, ni kwa mujibu wa mahitaji ya Marekani, katika suala la mizani ya usalama wa kikanda. Wakati tunapigana sisi kwa sisi, mshirika wa Marekani, adui yetu, India, anamakinisha utawala wake juu yetu sote. Wakati mpaka kati ya Waislamu wa Pakistan na Waislam wa Afghanistan ukiwaka moto, mipaka na Dola ya Kibanian inahifadhiwa kwa utulivu. Wakati Jeshi la Pakistan na wapiganaji wa kikabila wamenaswa ndani ya vita visivyo na mwisho, Jeshi la India liko huru kuelekeza uadui wake dhidi ya Waislamu wote wa kanda hii. Je, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa, enyi Waislamu? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ]

“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao.” [Surah Al-Fath 48:29]. Je, Waislamu wanapaswa kuwa wakali, wenye kulipiza kisasi na kuwachukia waumini, kuwashambulia na kujibu mashambulizi, kuua na kuuwawa? Je, Waislamu wanastahiki tu, kukubali usawazishaji mahusiano na kuwa ni wenye kujizidhibiti pamoja na Makafiri? Vipi, enyi Waislamu, vipi?!

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan na Maeneo ya Kikabila! Vipi leo mnapigana wenyewe kwa wenyewe? Je! sio nyinyi mliofanya kazi pamoja dhidi ya maadui makafiri, muda usio mrefu uliopita? Sio nyinyi, mliofanya kazi pamoja kuvifukuza vikosi vya uvamizi vya Urusi ya Kisovieti? Je! sio nyinyi mlioshirikiana katika kudumisha usalama wa kieneo kwa Waislamu? Je! Sio nyinyi, ambao kwa pamoja mliufanya Msitari wa Durand kuwa tulivu na salama, huku mkihakikisha Jeshi la India linakesha usiku, kwenye Mstari wa Udhibiti, kwa miaka mingi? Kisha, hapakuwa na vita baina yenu, kwa sababu ya Uislamu wenu. Ama kwa sasa, vita vyenu vya leo vinaweza kuisha, kupitia Uislamu wenu. Kumbukeni enyi ndugu wapenzi, kwamba makabila ya Madina yalikuwa yanapigana wao kwa wao kabla ya Uislamu. Hata hivyo, baada ya Uislamu, walisimama safu moja, kama jeshi moja, dhidi ya maadui makafiri. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu.” [Surah Aali Imran 3:103].

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan na Maeneo ya Kikabila! Geuzeni meza dhidi ya ukafiri na dola zake. Geuzeni wimbi la historia kwa kuupendelea Uislamu na Ummah wake. Fanyeni uadui baina ya Waislamu kuwa msiba wa zamani, kwa kuregesha hukmu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume (saw). Nyinyi ni wa ndugu moja. Mtume (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ قَدْ أَذْهَبَ عَنْكُمْ عُبِّيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ وَفَخْرَهَا بِالآبَاءِ مُؤْمِنٌ تَقِيٌّ وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ أَنْتُمْ بَنُو آدَمَ وَآدَمُ مِنْ تُرَابٍ لَيَدَعَنَّ رِجَالٌ فَخْرَهُمْ بِأَقْوَامٍ إِنَّمَا هُمْ فَحْمٌ مِنْ فَحْمِ جَهَنَّمَ أَوْ لَيَكُونُنَّ أَهْوَنَ عَلَى اللَّهِ مِنَ الْجِعْلاَنِ الَّتِي تَدْفَعُ بِأَنْفِهَا النَّتْنَ»

Mwenyezi Mungu (swt) amekuondoleeni kiburi cha zama za ujahilia, na kujifakhirisha kwake kwa mababu. Muumini ima ni mchamungu au mtenda dhambi muovu. Nyinyi nyote ni wana wa Adam (as), na Adam (as) anatokana na udongo. Watu waache kujifakhiri kwa mababu zao. Hao ni kuni tu katika Jahannam, au bila ya shaka watakuwa duni mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) kuliko mbawakawa anayeviringisha kinyesi kwa pua yake.” [Abu Daud]. Fanyeni kazi kama ndugu ili kusimamisha tena Khilafah Rashida. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume ndiyo itakayotukusanya sisi sote kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na Gaza zinazokaliwa kwa mabavu, na kuwalazimisha maadui zetu kurudi nyuma.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu