Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  22 Muharram 1446 Na: 1446 / 03
M.  Jumapili, 28 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tatizo la Umeme wa Ghali Halitatuliwi kwa Kupunguzwa kwa Malipo ya Nyuzi za Umeme na Majadiliano Mapya ya Mikataba Pekee. Suluhisho ni Kukomeshwa Kabisa kwa Ubinafsishaji katika Sekta ya Kawi, kwa mujibu wa Amri ya Mwenyezi Mungu (swt)
(Imetafsiriwa)

Kutolewa kwa data kuhusu malipo ya nyuzi za umeme kwa mitambo ya kuzalisha umeme na aliyekuwa waziri wa muda wa biashara, Gohar Ejaz, kumewashangaza watu. Muundo wa kandarasi za malipo ya nyuzi za umeme, ambao thamani yake ni zaidi ya rupia bilioni 2,000, umepangwa na mashirika ya wakoloni ya kimataifa, Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Sehemu kubwa ya malipo haya ya nyuzi za umeme ni riba ya mikopo ya riba kwa viwanda hivi. Fedha hizo zinakusanywa kutoka kwa umma na wafanyibiashara, hata kama viwanda hivi havizalishi kiwango hata kimoja cha umeme. Kwa hakika huu ndio uhalisia wa baadhi ya viwanda. Kwa hivyo, wawekezaji hawa wachache na benki wanapora mifuko ya watu, huku wakiwa wamekaa majumbani. Mitambo mingi iliyopo sasa inategemea uwekezaji kutoka kwa mrandi wa Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC). CPEC imeharibu uchumi na watu wetu. Je, CPEC sio “mbadilishaji mchezo” ambao watawala walikuwa wakiucheza?!

Watawala walijua makubaliano ya kawi ya “kuchukua au kulipa” kuanzia siku ya kwanza kabisa. Walifanya makubaliano haya, na wanafanya makubaliano mapya kila wakati. Wale wanaomaliza muda wao wa makubaliano wanaruhusiwa kuendelea kuwapora wananchi, kwa kuwaongezea muda wa leseni zao. Madhumuni ya kufichua maelezo ya sasa ni kuweka shinikizo kwa China kujadili tena mikataba hii. Sekta ya nishati iko ukingoni mwa kuanguka kabisa, na bila mabadiliko yoyote kwa makubaliano haya, kutakuwa na shinikizo kubwa la umma. Kuna hofu ya athari ya domino, kuongezeka kwa shinikizo la kukomesha uporaji, kabla ya kuanguka kabisa. Kwa hiyo, kupitia baadhi ya mageuzi, majaribio yanafanywa kuokoa ubinafsishaji wa ubepari wa kiliberali mamboleo wa kikoloni kwenye sekta ya kawi, ili mfumo huu katili uweze kuendelea. Suluhisho la tatizo hili sio mageuzi machache katika mikataba iliyopo. Suluhisho, kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu (swt), ni kutangaza kawi kama “mali ya umma” na kuiweka chini ya usimamizi wa serikali. Kisha mapato ya sekta hii yanaweza kukusanywa katika hazina ya umma ya Bayt ul Maal, na watu wanaweza kupata kawi kwa bei nafuu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«المسلِمونَ شُركاءُ في ثلاثٍ، في الكَلَإِ، والماءِ، والنَّارِ»

“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu, maji, malisho na moto (kawi).” [Abu Dawud na Ahmad]. Kwa hivyo ubinafsishaji wa sekta ya kawi umeharamishwa waziwazi na Uislamu.

Kutokana na mikataba hii ya kawi, mishahara ya Waislamu inaliwa na bili za umeme, huku watoto wao wakilala njaa. Kwa hivyo kwa nini tunapaswa kunyamaza kuhusu mikataba hii ya kikatili, iliyofanywa kwa jina la dhamana ya ubwana wa mfumo wa kimataifa, ambayo huwakaba watu wetu? Hatupaswi kunyamaza. Ni lazima tudai haki zetu za Uislamu na kuwalinda watu wetu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema;

«المسلمونَ على شروطِهم إلَّا شرطًا حرَّم حلالًا أو أحلَّ حرامًا»

“Waislamu wamejifunga kwa masharti ya mikataba yao, isipokuwa kwa masharti ambayo yanaharamisha halali au yanahalalisha haramu.” [Tirmidhi]. Mikataba hiyo imeharamishwa waziwazi kwa sababu wanageuza mali ya umma kuwa mali ya watu binafsi. Hakuna yeyote duniani mwenye haki ya kupindua amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu (swt) haturuhusu kuwaruhusu makafiri na mamlaka zao za kikafiri kutawala mambo ya Waislamu. Katika mikataba hii, taasisi za kimataifa za kikoloni ndizo zenye mamlaka ya kututoza faini na adhabu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَنۡ يَّجۡعَلَ اللّٰهُ لِلۡكٰفِرِيۡنَ عَلَى الۡمُؤۡمِنِيۡنَ سَبِيۡللًا]

“wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisa 4:141]

Huu ndio uhalisia wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI), ambao kwao watawala wa sasa waliunda Baraza Maalum la Uwezeshaji Uwekezaji (SIFC), na kutangaza ramani mpya ya maendeleo ya nchi. Je, hii si ndiyo ramani ya barabara ambayo matokeo yake tayari yako mbele yetu? Mapato ya dolari kwenye uwekezaji katika mitambo ya kuzalisha umeme yamepunguza akiba yetu ya fedha za kigeni. Zaidi ya hayo, sababu kuu ya kuendelea kuongezeka kwa bei ya umeme ni kutokana na malipo ya dolari, kwani kushuka kwa thamani ya rupia kunafanya ongezeko la bei kutoepukika. Lengo la uwekezaji wa China na Magharibi ni kuhodhi rasilimali muhimu za nchi kwa kubinafsisha rasilimali zinazomilikiwa na umma. Hii inawapa dhamana ya mapato ya dolari, hata kama watu watalazimishwa kuuza figo zao, na sekta ya ndani itaanguka.

Huu ni muundo wa ukoloni wa mfumo wa kimataifa, ambao watawala wetu wamekuwa wakiufikisha kwa wananchi usiku na mchana. Muundo pekee wa maendeleo na ustawi kwa Waislamu ni Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Khilafah Rashida itaunganisha rasilimali za ulimwengu mzima wa Kiislamu kuunda uchumi mkubwa zaidi duniani. Muundo wa kiuchumi wa Uislamu hautaruhusu mabepari na wakoloni wachache kunyonya rasilimali za Umma.

Badala yake, Khalifa Rashid huweka mapato ya rasilimali za mali ya umma kwenye akaunti ya Bayt al-Mal ili kuyatumia katika mambo ya umma, huku akitoa rasilimali hizi kwa watu kwa bei nafuu. Khilafah Rashidah itamaliza mikataba ya “kuchukua au kulipa”, kwa sababu Khilafah imejengwa juu ya kukataa udhalimu wa mfumo huu wa dunia wa kikoloni. Khilafah Rashida itafanya miamala yake ya kimataifa kwa sarafu za dhahabu na fedha badala ya dolari, ili kusiwe na dola yoyote ya ulimwengu yenye uwezo wa kuathiri mambo yetu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[لِمِثۡلِ هٰذَا فَلۡيَعۡمَلِ الۡعٰمِلُوۡنَ] “Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [Surah As-Saffat 37:61].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu