Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 14 Rabi' II 1446 | Na: 1446 / 14 |
M. Alhamisi, 17 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir ni Chama cha Kisiasa Ambacho Mfumo Wake ni Uislamu. Kamwe Hakina Uhusiano wowote na Uanamgambo
(Imetafsiriwa)
Kwa hili tunaiandikia Timu ya Wahariri ya gazeti la ‘Dawn’, kuhusu uchafuzi wa jina la Hizb ut Tahrir kwenye safu yenye kichwa, “Ratiba ya Nne: Kupambana na ugaidi au kunyamazisha upinzani?” Makala hayo yalichapishwa mnamo 16 Oktoba 2024, na yaliandikwa na Zia Ur Rehman, ambaye pia ni mwandishi katika gazeti la ‘New York Times’. Aliandika, “Kihistoria, Ratiba ya Nne imelenga wanamgambo sugu, wakiwemo wanachama wa vyama vilivyopigwa marufuku kama vile Tehreek-i-Taliban Pakistan (TTP) na Hizb ut Tahrir.”
Madai kwamba Hizb ut Tahrir ni shirika la wanamgambo sio sahihi na ni uchafuzi wa jina. Hizb ut Tahrir haibebi silaha, kwa sababu hiyo inagongana njia ya Mtume (saw) katika kusimamisha dola ya Kiislamu, kwani yeye (saw) alitegemea kazi ya kisiasa na hakutumia silaha. Wakati watu wa Ahadi ya Pili ya Aqaba (Ahadi ya Nusrah) walipomwomba ruhusa ya kupigana na watu wa Mina, yeye (saw) aliwajibu kwa kusema, «لم نؤمر بذلك» “Hatujaamrishwa kupigana bado.”
Hizb ut Tahrir haina uhusiano wowote na uanamgambo. Hata hivyo, watawala wa Waislamu wanaogopa kazi ya Hizb ut Tahrir kwa sababu mradi wa Khilafah ni badali ya kimfumo na ya kisiasa kwa mfumo wa sasa wa dunia. Watawala wa Waislamu hawawezi kupambana kifikra na misimamo ya kifikra ya Hizb ut Tahrir. Wao, kwa hivyo hukimbilia uongo ili kuichafua kazi ya kisiasa na kifikra ya Hizb. Wanaunda uhalali wa kuwanyima wanachama wa Hizb haki zao za kisiasa.
Wanachama kadhaa wa Hizb ut Tahrir, wakiwemo wanaharakati wa kisiasa walio na elimu ya hali ya juu, wamekuwa katika Ratiba ya Nne ya serikali kwa karibu muongo mmoja sasa. Hii imeruhusu utawala kuwatesa watu hawa kwa sababu tu wanataka kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume nchini Pakistan. Watawala wanawanyima haki yao ya kutembea, na haki yao ya kufanya miamala ya kifedha. Taswira isiyo sahihi ya Gazeti la ‘Dawn’ ya wanaharakati wa kisiasa kama wanamgambo, inaisaidia serikali katika kuwatesa wanaharakati wa kisiasa, na kuzuia uelezaji wa kisiasa za Kiislamu.
Iwapo Gazeti la ‘Dawn’ linataka kurekebisha mazingira ya kifikra na kisiasa ya Pakistan, je, inafaa katika uadilifu wake kuchapisha habari ghushi? Tunaomba kwamba Timu ya Wahariri wa ‘Dawn’ isahihishe maoni ya makosa ambayo kuripoti kwake kusiko sahihi kumeunda kuhusu Hizb ut Tahrir. Tunaomba ichapishe ufafanuzi ufuatao, “Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu. Inafanya kazi ya kisiasa na kifikra ili kusimamisha Khilafah Rashida. Kamwe haina uhusiano wowote na uanamgambo.” Tuna haki ya kuwakilishwa kwa usahihi katika gazeti la kila siku la kitaifa, ambalo linafakhiri kwa uadilifu wake na kuripoti kwake sahihi.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |