Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
H. 1 Muharram 1446 | Na: BN/S 1446 / 01 |
M. Jumapili, 07 Julai 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji ya Kikatili dhidi ya Watu Wetu mjini Gaza Bila Uwajibikaji! Lini Tutayaona Majeshi ya Waislamu Yakiinuka?!
(Imetafsiriwa)
Wizara ya Afya mjini Gaza imetangaza kuwa mashahidi 79 na majeruhi zaidi ya 289, baadhi yao wakiwa katika hali mahututi, wamewasili katika hospitali ya Nasser Medical Complex kufuatia mashambulizi ya mabomu kwa kambi za watu waliokimbia makaazi yao huko Mawasi Khan Yunis. Mauaji haya yanajiri baada ya uvamizi huo kufanya mauaji ya kutisha katika eneo la viwandani la kitongoji cha Tel al-Hawa, katika vitongoji vya Mji wa Gaza, na katika kambi za eneo la kati, na kusababisha zaidi ya mashahidi 100, na kuongeza kwa kasi idadi ya majeruhi.
Ukatili ambao umbile la Kiyahudi linatenda dhidi ya watu wetu huko Gaza haufichiki tena kwa mtu yeyote. Wanalenga watoto, wanawake na wazee, pamoja na nyumba, shule, hospitali, makao, na mahema ya waliohamishwa, mchana peupe na mbele ya kamera za vyombo vya habari. Miili imetawanyika barabarani na mchangani, na maiti zimelala kwenye barabara na nyumba chini ya vifusi na udongo, kana kwamba ni uwanja wa vita vya kikatili katika vita vya tatu vya dunia, bila huruma, upole, au maadili!
Jamii ya kimataifa yenye jicho moja imesalia kimya kabisa, na inaona kupitia darubini madhara hata madogo ya makafiri wakoloni, na kusababisha ghasia kote duniani. Taasisi, mashirika, marais, na watu mashuhuri hukutana kwa ajili yao, kuunda miungano na mikataba, na kupigana vita kwa ajili ya wachache wao. Hata hivyo, inapokuja kwenye mateso ya Waislamu na watu wa Gaza, inachukuliwa kama tukio la kupita tu, linalohitaji maneno machache ya kulaani au maswali yasiyo na hatia. Hili linadhihirisha kwamba jamii ya kimataifa si chochote ila ni chombo cha madhalimu na kiburi cha firauni duniani, na taasisi zake, sheria na miungano yake iliyoanzishwa kwa ajili ya kuhakikisha maslahi ya ukoloni, kiburi na kuendeleza madhalimu.
Ama kuhusu Marekani na nchi zote za kikafiri zilizokimbilia mwanzoni mwa vita kuunga mkono, kuidhinisha, na kusimama pamoja na umbile la Mayahudi, zimeshuhudia wenyewe kwamba wao ndio chimbuko la uovu duniani na chanzo cha chuki na uhalifu. Uungaji mkono wa Marekani wa wazi na usio na haya kwa umbile la Mayahudi, pamoja na nchi nyingine za kikafiri, kwa kuwapatia silaha, tani nyingi za mabomu, na vilipuzi, umeweka wazi umbile lao halisi kwa Waislamu hasa na ulimwengu kwa jumla. Wamejidhihirisha kuwa ni viongozi na nchi zisizo na akhlaki wala maadili, zisizo na kanuni wala ubinadamu. Wasiwasi wao msingi ni maslahi yao ya kikoloni na faida za kibinafsi, hata ikiwa itamaanisha kuangamiza watu au kuwachoma wanadamu.
Huyu hapa Biden na utawala wake, wakiunganishwa na chuki yao kubwa kwa Uislamu na Waislamu. Hawafanyi chochote isipokuwa kuwatumikia katika vita vya uchaguzi, hata kama barabara za Gaza zimejaa maiti na mabaki, na damu ya watu wa Gaza inatiririka kama mito, iliyosababishwa na mabomu na silaha wanazotuma kwa Mayahudi. Hawana shida na hili, na haliwasababishii kusita hata dakika moja.
Ama Mayahudi ni watu ambao hawafichi tena ndoto zao za Kitalmudi na malengo yao ya kiitikadi, na kutaka kuwaua watu wote wa Palestina ili asibakie yeyote isipokuwa wao katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Hivyo basi, enyi Umma wa Kiislamu hadi lini mutawaacha watoto wenu na ardhi yenu iliyobarikiwa kwa Mayahudi wanyakuzi, na nyuma yao Marekani na makafiri wakoloni, ili kueneza ufisadi na uhalifu, na kuchoma vibichi na vikavu?
Hadi lini, enyi majeshi ya Ummah na maafisa wake huru, mtabaki mkifungiwa ndani ya kambi zenu bila ya ushujaa wa al-Mu'tasim au ari ya al-Faruq?
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [At-Tawba:38].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: |