Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  25 Muharram 1446 Na: BN/S 1446 / 04
M.  Jumatano, 31 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Umbile la Halifu la Mayahudi Kukiuka Nafasi za Ummah na Kuua Watu wake katika Miji Mikuu ni Uhalifu wa Tawala za Kioga mbele ya Umbile la Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Katika shambulizi la kiuhaini na lisilo na aibu, umbile halifu la Kiyahudi lilimuua mkuu wa afisi ya kisiasa ya Hamas jijiniTehran, ambapo Ndugu Ismail Haniyeh aliuawa shahidi alfajiri ya leo na adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Umma. Tunamuomba Mwenyezi Mungu rehema na msamaha wake na amjaalie miongoni mwa mashahidi. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutaregea.

Mkono uliolaaniwa wa umbile hilo lililokasirikiwa umepanuka, ufisadi wake umeenea, na jinai zake zimevuka Ardhi Iliyobarikiwa ambapo unasababisha vifo, mateso, na mauaji kwa watu wake. Uchokozi wake umeenea, huku ndege zake zikizunguka anga za miji mikuu katika nchi za Kiislamu na miji yao, wakiua wapendavyo, wakiharibu na kuchoma wanavyotaka, na kuua kila unapotaka. Hakuna tofauti kati ya Gaza na Yemen, au miji ya kusini na Tehran. Ujumbe wake, kwa kauli na vitendo, ni kwamba nyinyi Waislamu hamna utakatifu katika damu na uhai wenu, ardhi, na anga, na kwamba hamna mipaka iliyolindwa, hamna heshima ya kizuizi, na hamna mstari mwekundu! Hali hii kwa hakika imekuwa uhalisia, ambapo hakuna utakatifu kwa nchi yoyote ya Kiislamu ambayo haijakiukwa na umbile hili, chini ya uongozi wa watawala wasaliti, walaghai, na waoga ambao wameingia katika hali ya unyonge kiasi kwamba hawajali tena kutunza ardhi zilizokiukwa, utu uliotusiwa, au nchi jirani za ndugu katika ardhi ya Uislamu ambao adui yao amevuka mipaka. Hawaguswi na damu safi iliyomwagwa, hata kama ni damu ya mgeni aliyeomba hifadhi kwao au Muislamu aliyewajia akikimbia ukandamizaji wa Mayahudi.

Hali ya watawala wote, ambao wamewapa ujasiri viumbe waoga na wadhalilifu zaidi kutoka kwa umbile la Mayahudi, iwe wametangaza waziwazi usaliti na uhalalishaji mahusiano, au kudai upinzani na ukaidi, haina tofauti na hali ya yule mlaji njama aliye kimya, aliyeridhika, au yule muoga, aliyedhalilishwa ambaye hasubutu kujibu hata akishambuliwa, ambaye ana haki ya kujibu, au yule anayetetemeka kwa uoga na hofu ya jibu kali ingawa anao uwezo wa hilo, akijificha chini ya paa la Marekani huku adui akileta uharibifu, kuua na maangamivu pasi na mipaka!

Kile ambacho umbile la Kiyahudi linafanya leo inathibitisha kwamba hakika ni adui wa Ummah mzima, sio tu kihukmu bali kivitendo vile vile, kwani sasa linatekeleza uchokozi wake dhidi ya kila mtu.Uovu na ubaya haufungiki tena kwa Palestina na watu wake, na kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka isipokuwa ling'olewa. Uchokozi wake utabakia muda wote maadamu lingalipo, na kuthibitisha kwamba hakuna ardhi katika nchi za Kiislamu inayowahifadhi wala anga kuwalinda, iwe ni kutoka kwa watu wa ardhi au wale waliotafuta hifadhi kwa ndugu zao. Hii ni chini ya watawala hawa waoga, na ardhi yao itabaki kukiukwa, heshima na utu wao kuvunjwa, damu yao kumwagwa, na uhai wao kudidimia maadamu watawala hawa wataendelea kubaki kwenye viti vyao vya enzi. Nguvu, uwezo, idadi, mali, majeshi, na uwezo wa Ummah, licha ya wingi na ukubwa wao, havitakuwa na manufaa maadamu tawala hizi za khiyana zitawazima na kuwabana. Wao sio msaada wala uti wa mgongo kwa Ummah!

Suala la kuwaondoa watawala hawa waoga ambao wameufuja Ummah, Dini yake, na damu yake, na wakamfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake, liko katika kila tukio. Hakika ndio msingi wa majanga yote yanayotokea katika nchi za Kiislamu. Suala la kuwa na Imam kwa Waislamu, ambaye atakuwa ngao na ulinzi kwao, kusimamisha Dini na kuhuisha jihad, kuhifadhi ardhi na watu wake, limekuwa ni jambo la lazima, kwani ni wajibu na faradhi. Hapo, ndipo pekee umbile la Kiyahudi na uchokozi wake utakuwa ni madhara ya kuondolewa na athari ya kufutwa, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[كُلَّمَا أَوْقَدُوا نَاراً لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَاداً وَاللهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ]

“Kila mara wanapo washa moto wa vita, Mwenyezi Mungu anauzima. Na wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi waharibifu.” [Al-Ma'ida:64].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu