Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  30 Jumada I 1447 Na: HTS 1447 / 57
M.  Ijumaa, 21 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Watu wa Sudan, Amerika Inaharakisha Kuvuna Matunda ya Vita vyake nchini Sudan, Kwa hivyo Msiiruhusu Itenganishe Darfur
(Imetafsiriwa)

Wakati wa hotuba yake katika Kikao cha Uwekezaji kati ya Marekani na Saudi Arabia, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba Mfalme Mtarajiwa Mohammed bin Salman alikuwa ameomba azimio la mgogoro nchini Sudan, akiongeza kwamba alianza kusoma suala hilo nusu saa tu baada ya maelezo ya Mwanafalme huyo. Trump pia aliandika kwenye tovuti yake ya Kijamii ya Truth kwamba atatumia mamlaka ya urais kusimamisha vita mara moja.

Katika jibu la haraka, kupitia tweet kwenye jukwaa la X, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Burhan, aliandika mnamo Jumatano jioni: “Asante, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, asante, Rais Donald Trump.”

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mnamo Jumatano, 19 Novemba 2025, ambayo ilionekana kuwa imeandaliwa mapema, Baraza la Utawala wa Mpito lilisema: “Serikali inakaribisha juhudi za Ufalme wa Saudi Arabia na Marekani kufikia amani ya haki nchini Sudan. Pia inawashukuru kwa wasiwasi wao na juhudi zinazoendelea za kuzuia umwagaji damu nchini Sudan, na inathibitisha utayari wake wa kushirikiana nao kwa uzito ili kufikia amani ambayo watu wa Sudan wanaisubiri...”

Kwa hivyo nini kilitokea?! Ni nini kilichotokea kilichoifanya Amerika kuingilia kati ili kukomesha vita, na kusababisha msimamo wa serikali kubadilika kutoka mazungumzo ya uhamasishaji wa kijeshi, kuondoa wanamgambo, na kukomboa eneo lote la Sudan, na kuzungumzia amani ambayo watu wa Sudan wanaisubiri?!

Ni wazi kwamba Amerika inataka kuvuna manufaa ya vita ilivyoanzisha, hasa baada ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kunyakua udhibiti wa Darfur yote na bado kudhibiti sehemu kubwa za Kordofan, ikionekana kulinda mipaka ya Darfur. Suluhisho lililopongezwa na Baraza la Utawala, baadhi ya vikosi vya kisiasa, na baadhi ya vyombo vya habari ni lile lile lililopendekezwa na Quartet, ambalo linalinganisha jeshi na RSF. Na kwa msingi huu, suluhisho litatekelezwa! Hakika, mshauri wa Rais Trump wa Marekani, Massad Boulos, alituma ujumbe kwenye Twitter: “Chini ya uongozi wa Rais Trump, tunafanya kazi na washirika wetu kuwezesha makubaliano ya amani ya kibinadamu na kukomesha usaidizi wa kijeshi wa nje kwa pande hizo, ambao unachochea vurugu.”

Kuhusu kwa nini Amerika inaharakisha juhudi zake za kukomesha vita nchini Sudan, ni kuzuia uingiliaji kati wa Ulaya, na hasa Uingereza, nchini Sudan. Mojawapo ya sababu za vita hivi vikali ilikuwa ni kuiondoa Uingereza na washirika wake kutoka eneo la tukio. Hili lilifikiwa kwa kuvunja kile kinachoitwa Muundo wa Makubaliano, ambao tayari umefanyika. Sasa, Ulaya imechukua ukatili uliofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka huko El Fasher kama fursa. Chanzo kimoja cha kidiplomasia cha Ulaya kilithibitisha kwa Al-Araby TV mnamo Jumanne, 18 Novemba 2025, kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa EU watashinikiza kupanuliwa kwa vikwazo vya silaha ili kujumuisha Sudan yote. Zaidi ya hayo, Mratibu wa Msaada wa Dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, alielezea hali huko Darfur, haswa huko El Fasher, baada ya ziara yake, kama eneo la kutisha na eneo la uhalifu.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tumekuwa tukionya kila wakati, na tunaendelea kuonya, kuhusu hatari za kuingiliwa na Marekani katika nchi yetu na utekelezaji wa mpango wake wa kuigawanya Sudan. Amerika ndiyo iliyoitenganisha Sudan Kusini kwa jina la kinachoitwa amani, na leo inatafuta, kwa kutumia mbinu ile ile ya kukomesha vita na kufikia amani, kutenganisha Darfur baada ya kumpa nguvu kibaraka wake, Hemedti, huko na kufumbia macho uundaji wa serikali sambamba. Mjumbe wake maalum, Musaad Boulos, bado anazungumzia pande mbili, akilinganisha jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka, kama vile Amerika hapo awali ilivyolinganisha serikali ya Sudan na wanamgambo wa kiongozi wa waasi aliyekufa, John Garang!

Enyi watu wa Sudan, msing’atwe mara mbili na nyoka wa Amerika! Amkeni haraka na mzuie mpango wake wa kutenganisha Darfur kwa kurudi kwenye hukmu za Uislamu, kama Mola wenu Mlezi, Aliyetukuka, alivyowaamuru. Amesema Mwenyezi Mungu:

[فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ]

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” [An-Nisa 4:59], na wazuieni wale wanaotekeleza mipango ya Marekani na kuwahimiza kushikamana kwa uthabiti na haki. Na fanyeni kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itawakata mikono wale wanaoharibu umoja wa nchi yetu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb Ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu