Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  12 Sha'aban 1443 Na: 07/1443 H
M.  Jumanne, 15 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katika Kumbukumbu ya Kumi na Moja Tangu Kuanza kwa Mapinduzi Matukufu ya Ash-Sham Hakuna Mbadala wa Kuipindua Serikali na Kusimamisha Utawala wa Uislamu Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.
(Imetafsiriwa)

Kumbukumbu ya kumi na moja ya tangu kuanza kwa mapinduzi yaliyobarikiwa ya Ash-Sham yapo juu yetu, na tuna yakini kwamba Mwenyezi Mungu (swt) hatayafelisha mapinduzi ambayo yalitoa thamani kubwa katika njia Yake, mapinduzi yaliyotoka nje ya misikiti yake, na kulingania kwa sauti ya juu kabisa “Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,” na ikamfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuwa ndiye kiongozi wake.

Kafiri Magharibi imejaribu kuyadhibiti mapinduzi haya yatima, kuyazuia, na kuyageuza kutoka kwenye mkondo wake tangu siku ya kwanza ya kuzinduliwa kwake; kwa sababu ya hatari kubwa yaliyomletea kibaraka wake, dhalimu wa Ash-Sham. Haya yalikuwa ni matayarisho ya kuyaavya na kuyaondoa katika maudhui yake, hivyo ikaitega mitego katika makongamano yake, ikayajaza hadi pomoni kwa fedha chafu za kisiasa, na ikayafunga minyororo ya makubaliano, mapatano na mazungumzo, na ikaanza kujiandaa kutayarisha mustakabali wake kwa mujibu wa mtazamo wake wa kutenganisha Uislamu na maisha, kupitia katiba iliyoandaliwa kwa ajili yake; kwa kuutoa Uislamu katika utawala, kuhifadhi maslahi yake, kudhamini ukoloni wake wa ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham, na kuhakikisha ndani yake kuwasili kwa watu wake madarakani, hivyo imebadilisha kibaraka kwa kibaraka mwengine; na katiba ya kisekula iliyotungwa na binadamu kwa katiba nyengine ya kisekula iliyotungwa na mwanadamu, hivyo kuhakikisha masaibu ya Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham, na ugumu wa maisha yao, baada ya kuwaweka mbali na dini yao, mfumo wake na hukmu zake.

Enyi Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Kafiri Magharibi ndiye aliyeiangusha Dola ya Kiislamu ambayo misingi yake iliwekwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Ni wao ndio waliozikoloni nchi za Kiislamu na kuzigawanya katika vijidola vidogo vidogo. Wanawafanya watu wake kuwa watumwa, na wanawatesa kwa adhabu kali. Je, Azimio nambari 2254 la Baraza la Usalama linataka kutuokoa na kutupa maisha ya staha?

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Nyumba ya Uislamu:

Hautatengea mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale yaliyotengea kwayo  mwanzo wake, kwani hakuna wokovu kwetu isipokuwa kwa kushikamana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), na kutabanni mradi wa Khilafah kwa njia ya Utume unaotokamana na imani yetu, na hiyo ni kwa kufanya kazi kwa bidii na ikhlasi pamoja na wafanyaokazi ili kuusimamisha, ndiyo njia pekee ya wokovu, na ndiyo njia pekee ya wokovu wetu. Ndio pekee inayosuluhisha matatizo ya Waislamu, kuregesha haki zao na kurudisha heshima yao, na kwa njia hiyo pekee Uislamu hutekelezwa katika medani ya vita vya maisha, na kila kitu chengine chochote kisokuwa hiki ni kupoteza muda na juhudi, kupoteza nguvu, na kuzama kwenye kinamasi cha mfumo mbovu wa kirasilimali uliowatesa watu na kuharibu nchi. Mwenyezi Mungu (swt):

 [فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika * Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Taha:123-124].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu