Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  10 Jumada I 1444 Na: 08 / 1444 H
M.  Jumapili, 04 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkakati wa Kutambaa kwa Mchwa Unasalia Kuthibitishwa hadi Uavyaji wa Mapinduzi ya Ash-Sham... Jihadharini!
(Imetafsiriwa)

Duru rasmi za Kituruki ziliiambia Al-Jazeera kwamba Uturuki iliweka masharti ya kujiondoa kwa kile kinachojulikana kama Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria – ambavyo kimsingi vinajumuisha Vikosi vya Ulinzi vya Watu wa Kikurdi (YPG) - kutoka Manbij, Ayn al-Arab Kobani na Tal Rifaat kaskazini mwa Syria. Duru hizo zimeongeza kuwa, Ankara pia ilitaja kuregea kwa taasisi za utawala wa Syria kama njia badali ya Kikosi cha Kidemokrasia cha Syria (SDF), vikiwemo vikosi vya usalama na walinzi wa mpaka.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham: Sio siri tena kwa mtu yeyote dori ambayo utawala wa Uturuki ulicheza na unacheza dhidi ya mapinduzi yaliyobarikiwa ya Ash-Sham, baada ya kuukabidhi mji wa Aleppo na maeneo makubwa yanayoanzia Morek kaskazini na kaskazini magharibi mwa jiji la Aleppo kwa utawala wa kihalifu. Inaendelea kufanya kazi ya kukabidhi maeneo mengine katika juhudi za kuupa uhai tena, na kusaidia kupanua udhibiti na ushawishi katika eneo lote la Syria.

Pia, utawala wa Uturuki unatafuta, kupitia kuyakabidhi baadhi ya maeneo yanayodhibitiwa na SDF kwa utawala wa Assad, kupata pointi kabla ya uchaguzi wa rais wa Uturuki, ambao unakaribia. Kwa kucheza kwenye safu ya usalama wa taifa kwa upande mmoja, na kuyawasilisha maeneo haya kama zawadi kabla ya kukutana na dhalimu wa Ash-Sham kwa upande mwingine.

Kukaa kimya kuhusu yale ambayo utawala wa Uturuki umeyafanya na unayafanya dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham, kwa kutumia zana zake kutoka kwa viongozi wa mfumo wa makundi unaohusishwa nayo, ni uhalifu dhidi ya mapinduzi, na kujiua kisiasa ambako wahusika wake watajuta sana wakati watakapokutana na hatima yao. Na watajuta kupoteza kila tone la damu ya watoto wao, bila kutaja mateso katika aina zake zote za kuhamishwa, uharibifu, kukamatwa na kuteswa.

Njia ambayo serikali ya Uturuki inafuata inajulikana kwa kila mtu mwenye akili timamu. Kushindwa kwake kuanzisha operesheni za kijeshi dhidi ya kile kinachoitwa Kikosi cha Kidemokrasia cha Syria pasi na idhini kutoka kwa mabwana zake, na matakwa yake ya kuyakabidhi baadhi ya maeneo yanayodhibitiwa na SDF kwa utawala wa kihalifu badala ya kufanya kazi ya kuyaungana na maeneo yaliyokombolewa na kuwarudisha watu wao waliohama maeneo hayo. Na kuzuia mfumo wa makundi, kwa kula njama na uongozi wake, usichukue hatua zozote nzito za kuyakomboa maeneo hayo, kunaonyesha dori halisi ya utawala wa Uturuki na ukubwa wa njama zake dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham.

Hii ina maana kwamba kuregea kwa watu waliokimbia makaazi yao katika nchi yao ni ndoto tu, na kwamba kuupindua utawala huo au kuuwajibisha kwa jinai zake kutokana na madai ya kuunga mkono utawala wa Uturuki au watu wengine limekuwa historia, na kwamba sera ya kichuguu ya maridhiano na utawala wa kihalifu na kuondoa mapinduzi ya Ash-Sham inaendelea kwa kasi kwa mbinu na aina mbalimbali za udanganyifu.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Makazi ya Uislamu: Tulikuwa na bado tungali tunafanya kazi ya kufichua hila na njama zilizosukwa na Magharibi kafiri dhidi ya mapinduzi yaliyobarikiwa ya Ash-Sham, na kuweka njia na mbinu zote za ufanisi kukabiliana nayo, kwa kuanzia na onyo kuhusu fedha chafu za kisiasa ambazo sumu yake bado inazunguka kwenye mishipa ya viongozi wa mfumo wa makundi yanayohusiana, pamoja na mapigano ya chuki yaliyotokea kati ya vipengele vyake, kupitia onyo la mapatano na mazungumzo, na maazimio yaliyotokana na mikutano yote ya kimataifa huko Geneva, Sochi na Astana...

Na sisi hawa hapa katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Syria, tukirudia na kuthibitisha kwamba suluhu pekee ya kutoka nje ya uhalisia tulioufikia ni kutoa mambo ya ushindi na mafanikio, ya kwanza kabisa ni kwamba sote tushikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, baada ya kukata mahusiano yote na mataifa yote, na kuunganisha nguvu za umma na za kimada nyuma ya uongozi wa kisiasa mwaminifu, unaofahamu na wenye ikhlasi ambao unatabanni mradi wazi wa kisiasa unaotokana na Aqida (itikadi) ya Kiislamu, vyenginevyo ni kupoteza tu muda, juhudi na muhanga.

Njama dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham ni kali, na njama hizo ni kubwa, na kukabiliana nazo kunahitaji misimamo ya ikhlasi, na huu ni wajibu wa watoto wote waaminifu wa mapinduzi ya Ash-Sham, kwani katika hilo umo ushindi wetu, wokovu wetu, na maisha yetu.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُون]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu