Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  30 Rajab 1440 Na: 1440/05
M.  Jumamosi, 06 Aprili 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Tanzania Yatuma Ujumbe Katika Ubalozi wa Uchina

Jana, Ijumaa 5 Aprili 2019 / 29 Rajab 1440 Hijri, Hizb ut Tahrir / Tanzania ilituma ujumbe hadi Ubalozi wa Uchina nchini Tanzania ili kufikisha barua maalumu ya kuwasilisha malalamishi juu ya mateso ya dola ya Uchina kwa Waislamu wa Uyghur.

Ujumbe huo, uliongozwa na Masoud Msellem – Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania akiandamana na Said Bitomwa – Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania, waliwasili katika ubalozi huo wa Uchina jijini Dar es Salaam mwendo wa 11:45 am.

Usalama wa ubalozi huo katika lango kuu ulipokea barua hiyo ambayo ilijumuisha nakala nne (lugha) ya Kichina, Kiuyghur, Kiarabu na Kiswahili. Tulipoomba kutaka kuonana na afisa yeyote wa ubalozi huo, walijibu kuwa mpangilio wao ni kupokea barua iliyo na anwani pekee, kisha ubalozi, endapo utaona kuna haja huenda ukafanya maandalizi ya mkutano.

Kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, tunauomba kwa ari Ubalozi wa Uchina nchini Tanzania kuandaa mkutano na Hizb ut Tahrir / Tanzania ili kufikisha ujumbe wetu kwao wenyewe. 

Barua hiyo ilikuwa ni taarifa kwa vyombo vya habari kwa anwani: Khilafah Itakomboa Turkestan Mashariki Na kuwanusuru Uyghur kutoka kwa Ukandamizaji wa Kihalifu wa Uchina.” Ilitolewa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Sehemu ya taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema yafuatayo:Huku utawala wa Uchina ukiendelea kuwahangaisha Waislamu wa Uyghur kwa kutumia kila mbinu ya kidhalimu ikiwa ni pamoja na kuwawekea vikwazo wasitekeleze ibada zao na wasihudhurie misikiti kwa kuifunga, kuwalazimisha wasifunge katika mwezi wa baraka wa Ramadhan, na kupiga marufuku ibada aina yoyote ya Kiislamu mpaka hivi majuzi wamezindua kambi kubwa na kuwafunga Waislamu zaidi ya milioni 1 ndani ya kuta zake eti ni kampeni inayodaiwa kulenga "kupambana na ugaidi" kwa kisingizio cha mwito wa: "mafunzo ya kitaaluma" na huku ikiwashika wasomi, wanasayansi, wanafikra na maprofesa wa vyuo. Yote haya ili kueneza wasiwasi na kutia hofu katika mioyo ya Waislamu ili kujisalimisha kwa udhaifu wa ushikamanaji wa Dini yao ya Kiislamu.”

Kama barua hiyo ilivyo tamatisha, ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itakuja hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ambayo italeta ushindi kwa ndugu zetu wanaodhulumiwa Turkestan Mashariki, na itawahesabu wote wale walio wadhulumu na kusimama dhidi yao. Mtume (saw) asema 

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Kiongozi ni ngao, nyuma yake mnapigana na kujilinda”. Na wakati huo hakuna Uchina wala mwingine yeyote atakaye thubutu kuwadhuru Waislamu, kwa sababu watatambua kwamba lolote walifanyalo sasa litawarudi maradufu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye uwezo.  

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu