Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  29 Rabi' I 1444 Na: 1444/04
M.  Jumanne, 25 Oktoba 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ingawa Uwanja wa Kasbah Umegeuzwa kuwa Kambi ya Usalama na Kijeshi

Hizb ut Tahrir Yanakili Msimamo wa Kisiasa Kukataa Kuiuza Tunisia kwa Mfumo wa Fedha wa Kimataifa na Mipangilio yake
(Imetafsiriwa)

Serikali ya rais haikutosheka na kutia saini hati ya mpito kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ili kukaza mshiko wake kwa nchi hii na wananchi, wala haikutosheka na kutoa rushwa kwa Chama Kikuu cha Wafanyakazi cha Tunisia kwa ushiriki wake katika uhalifu wa kujisalimiisha kwa masharti ya IMF na dozi yake hatari, wala haikutosheka na kuzua mashtaka ya kidulma na ya kirongo dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir kuidhoofisha hizb na kuishughulisha ili isifichue njama zake na duara za kikoloni na zan zao za kifedha. Haikutosheka na yote hayo. Kwa hiyo, asubuhi ya leo, tarehe 25/10/2022, iliugeuza Uwanja wa Kasbah kuwa kambi ya kijeshi na ya usalama, na kufunga milango yote ya kuingia na kutoka kwenye Uwanja wa Kasri la Serikali, na kuzuia umati wa watu kuwasili na kukusanyika ili kuzuia maadamano yaliyoitishwa na Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Tunisia kuhutubia sera ya kuiuza Tunisia kwa wakoloni. Licha ya haya, hizb iliweza kufanya maandamano hayo na kutuma ujumbe ufuatao:

1- Kuziba midomo na kutoiruhusu Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia kueleza kukataa kwake makubaliano kati ya serikali na IMF kunathibitisha kuwa dola hii haimiliki uamuzi wake wa kisiasa, na kwamba mabalozi wa nchi za nje hawairuhusu kuwaacha wale wanaoeleza kukataa kwao utawala wa Magharibi na zana zake za kifedha. Magharibi inaruhusu maandamano kwa wale tu wanaokiri utawala wao juu ya nchi hii, kiupole na kinguvu, na hawaruhusu chochote chini ya hayo.

2- Mikopo ya nje ina madhara halisi kwa uhuru wa nchi na uamuzi wa kisiasa. Hapo awali, mikopo ya nje kwa ajili ya kufadhili ilikuwa ndio njia ya ukoloni wa moja kwa moja kwa nchi. Kupitia hilo, Wafaransa walikuja kuitawala Tunisia, na leo hii ndio njia kuu ya kupanua ushawishi na njama dhidi ya nchi hii, na hakuna kitu kizuri kinachotoka humo.

3- Hakuna suluhisho kwetu isipokuwa kwa kukataa mfumo wa kibepari na nidhamu yake ya kiuchumi na kifedha, na kukataa misaada ya kimataifa na mikopo kutoka kwa benki zake, na badala yake kuamsha mradi wa hadhara ya Kiislamu ili kutarajia maisha mapya, salama na amani ulio huru kutokana na migogoro ya kiuchumi au ya kifedha, kwa kuzingatia uadilifu wa nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu.

Maandamano hayo yalijumuisha hotuba na kauli mbiu zilizotolewa dhidi ya sera za serikali zilizoiweka nchi na watu rehani kwa ukoloni. Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia ulielekea kwa serikali ili kuwapa barua ya wazi kutoka kwa hizb yenye kichwa: "Kusaini Mkataba na Mfumo wa Fedha wa Kimataifa ni Ala Nyingine ya Kuikoloni Tunisia."

Kwa kumalizia, tunasema: Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia iliweza kunakili msimamo wa kisiasa wa kukataa kuiweka rehani nchi na watu kwenye duara za Kimagharibi, katika wakati ambapo tabaka la kisiasa (watawala na wapinzani) limeanguka mikononi mwa Magharibi. na kutambua mamlaka yake juu ya nchi hii. Leo, Hizb ut-Tahrir imeamua na imedhamiria zaidi kuangusha utawala wa Kimagharibi na zana zake za ndani, na kuitoa nchi hii kutoka katika majanga yake kupitia kusimamisha utawala muongofu kwa msingi wa Uislamu chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj: 41].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu