Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  17 Jumada I 1444 Na: 1444/10
M.  Jumapili, 11 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Licha ya Ujanja wa Duara za Magharibi na Kejeli ya Uchaguzi wa Wabunge, Mapinduzi ya Umma Yanaendelea ili Kusimamisha Khilafah ya Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Maadhimisho ya miaka kumi na mbili ya kuzinduliwa kwa mapinduzi ya Umma yanatuangukia tarehe 17 Disemba hii. Makafiri wa kikoloni wa Magharibi na vibaraka wao walio madarakani wanafanya kazi kwa njia na mbinu zote kuvunja utashi wa watu, kukandamiza ari yao ya kimapinduzi, na kuondoa jaribio lolote la kuleta mabadiliko makubwa kwa msingi wa Uislamu, hasa pale Uislamu na Khilafah ilipokuwa ndio rai jumla katika nchi za Kiislamu, ikiwemo Tunisia.

Magharibi kafiri imejaribu kuyapotoa mapinduzi kutoka kwenye mkondo wake tangu siku ya kwanza ya kuzinduliwa, kwa sababu ya hatari kubwa iliyoletwa na ushawishi wake katika eneo hilo. Matokeo ya Mkutano wa G8 wa Deauville nchini Ufaransa mwezi Mei 2011 yalihitaji kuifunga Tunisia na mikataba ya kimataifa, kuizamisha katika madeni ya nje, na kuweka ramani ya mustakabali wake kulingana na mtazamo wake katika maisha kupitia katiba iliyotungwa na wanadamu inayoutenga Uislamu na utawala na kuhifadhi maslahi yake, na matokeo yake kudhibiti hali ya kisiasa, kuwaleta watu wake wa chaguo lao madarakani. Licha ya ujanja wote huo, nchi za Magharibi na zana zake za duni hazikuweza kuzima moto wa mapinduzi. Vuguvugu la Julai 25, 2021 lilitokea ili kuokoa mfumo wa kisekula unaoporomoka kwa kubadilisha kibaraka mmoja na kuweka mwengine na kubadilisha katiba ya 2014 ya kisekula kwa katiba nyengine ya kisekula, hivyo kuhakikisha kuwa nchi inasalia kuwa chini ya udhibiti wake katika mipango, sheria na utekelezaji baada ya kutengwa kutoka katika dini, mfumo na hukmu zake.

Watu Wetu wa Tunisia: Kejeli ya uchaguzi wa wabunge, pamoja na kuwa ni jinai inayompinga Mwenyezi Mungu katika sheria na chaguo la rais Kais Saied kuufanya wakati wa maadhimisho ya kuanzishwa kwa mapinduzi ya Umma ni sura nyingine ya njama za kufunga faili ya mapinduzi milele na kupandikiza mfumo wa kisekula, sababu ya taabu na kukata tamaa. Aidha, ni jibu kutoka kwake kwa dola za Magharibi kujiondoa katika hali ya kipekee kupitia kuanzisha Bunge jipya, ambalo linamuwezesha kuhifadhi maslahi ya Magharibi na kusonga mbele katika kutekeleza ahadi za Serikali ya Rais kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Kinachotia matumaini ya kweli ni kwamba Ummah umetambua kwamba chaguzi hizi ni chombo cha kuumakinisha mfumo na kwamba unawaleta tu vibaraka kwa duara za Magharibi pekee. Kususia kwa watu kura ya maoni juu ya katiba na kusita kwao kushiriki katika uchaguzi ujao wa bunge kunawakilisha kofi kali kwa ukoloni na vinyago vyake.

Watu Wetu Nchini Tunisia: Leo, mabadiliko ya kimsingi yamekuwa kitu ambacho kinajilazimisha wenyewe juu yetu, na hakuna njia mbadala au chaguo jengine isipokuwa kazi kubwa ya kubadilisha uhalisia ambao watu wote wameshuhudia kuwa wakifisadi. Leo mapinduzi yapo njia panda na yanapita kwenye mtihani mgumu kwani wapo wanaotaka kuyamaliza na kuyafilisi kwa kuzima moto wake na kuzima harakati zake ili yasinyanyuke, na kinyume chake wapo wanaofanya kazi kuhifadhi fikra yake, kushika mizizi yake na kusahihisha mkondo wake kwa mujibu wa mtazamo wa kimkakati na ruwaza iliyoegemezwa kwenye mradi wa kisiasa, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Na sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia tunatoa wito kwa watu wetu wa Tunisia kukamilisha mapinduzi yao kwa Uislamu, na kuzingatia njia mbadala ya kihadhara tunayowapa, ambayo imejengwa juu ya Uislamu mtukufu, kama badali pekee inayoweza kuutoa Ummah kutoka katika misukosuko yake na kufikia malengo na misimamo ya mapinduzi, katika kuipindua serikali katika sura zake, nguzo, na alama zake zote na kufanya kazi ya kusimamisha utawala wa kimantiki kwa msingi wa Uislamu, ambao Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuutabikisha, chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo huweka mizani kwa uadilifu alivyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt).

[الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj 22:41]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu