Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  9 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 28/1445
M.  Jumamosi, 15 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Pongezi kwa Mnasaba wa Idd al-Adha al-Mubarak

Kutoka Ardhi ya Zaitouna, Tunisia, hadi Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina
(Imetafsiriwa)

Labbaika, Allahumma Labbaik! Labbaika La Sharika Laka Labbaik! Innal-Hamda wan-ne’mata Laka wal-Mulk La Sharika Lak.

Huku sauti za mahujaji kwenye nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu zikipaa kwa mwito wa Mwenyezi Mungu, sauti za watu wa Gaza zimepaa tangu Kimbunga cha Aqsa katika kumwita Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, vikosi vyote vya ukafiri na dola za kihalifu kutoka Magharibi, ambazo zina chuki dhidi ya Uislamu na watu wake, zinakula njama dhidi yao ili kuliokoa umbile katili la Mayahudi na kuupiga vita mradi mtukufu wa Kiislamu unaotokana na itikadi yetu, na kumaliza matamanio yetu ya utu na wokovu kupitia kutabikisha sheria ya Mola wetu.

Kwa mnasaba wa ujio wa Idd al-Adha, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah Tunisia tunatoa salamu zetu kwa watu wetu wenye subira katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina:

Idi hii inatujia huku udanganyifu wa Marekani na washirika wake, na zile walizozikusanya katika dola za kinafiki na zenye mifarakano, zikizidi kuzuia kuanguka kwa umbile la Kiyahudi, umbile la chuki na uhalifu. Udanganyifu huu unaongezeka siku baada ya siku, na mauaji mjini Gaza, Rafah, kaskazini, na kwengineko hayatakuwa ya kwanza wala ya mwisho ya udanganyifu huu.

[قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ]

“Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surat Al-Munafiqun:4]

Idd al-Adha inafika, na kujitolea muhanga ni kwingi, na mateso ni makubwa; nyumba na miji imeharibiwa, mamilioni ya watu wamekimbia makaazi yao, watoto wamekuwa mayatima, na heshima imekiukwa... Thamani pekee ya haya yote ni mwamko wa Ummah na juhudi zake za kukomboa na kuyakusanya majeshi yake ili kuling'oa umbile la wale waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu na ili kusimamisha dola ya Uislamu ambayo italipa kisasi cha Dini, ardhi, na heshima, kwa ridhaa kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Enyi Waislamu wenye subira katika Gaza hasa, na enyi Waislamu wa Tunisia, nchi ya Zaitouna na vizazi vya washindi, na enyi Waislamu popote pale:

Sisi, ndugu zenu katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, tunapokupongezeni kwa Idd yenu na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie afueni, ushindi, na tamkini, tunathibitisha kwamba wokovu wetu upo katika kukata mafungamano ya dola hizi hadaifu zinazohifadhi chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na kukataa masuluhisho yao machafu ya kisiasa ambayo yametufunga minyororo kwa miongo mingi na kuyaweka rehani maamuzi yetu, na kwa kushikamana imara na kamba yenye nguvu ya Mwenyezi Mungu pekee, kwani ushindi wetu uko mikononi mwake. Tukijadidisha upya ahadi yetu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, pale sauti zetu zilipopiga kelele, “Niko hapa, ewe Mwenyezi Mungu, niko hapa,” tunakuleteeni bishara kwamba njama za makafiri zitafeli, na ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kupeana ushindi kwa Dini yake na kuwakirimu waja wake wanyoofu iko karibu, karibu sana. Hapo, ndipo Idd yetu na furaha yetu kuu itakuja. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آَمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Surat Ghafir:51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu