Afisi ya Habari
Uholanzi
H. 6 Safar 1444 | Na: 03 / 1444 |
M. Ijumaa, 02 Septemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Waislamu wa Uyghur
(Imetafsiriwa)
Afisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti kuhusu uzito wa "ukiukwaji wa haki za binadamu" dhidi ya Waislamu wa Uyghur unaofanywa na China. Afisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu (OHCHR) inasema kuwa imepata ushahidi wa kutosha wa mateso na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu ambao unaweza kuelezewa kama "jinai dhidi ya binadamu". Ripoti hiyo inaelezea kwa kina jinsi Uyghur na Waislamu wengine wanavyokabiliwa na mateso na unyanyasaji wa kimwili. Dondoo ndogo kutoka kwa orodha hii ndefu ya uhalifu ni kwa mfano matumizi ya viti vya mateso ambamo mtu hufungwa mikono na miguu na baadaye kuteswa, wanawake na wasichana wanabakwa, uavyaji mimba wa kulazimishwa na ufungwaji kizazi hufanyika na kufungwa faragha kwa muda mrefu.
Uchapishaji ripoti hiyo ulichukua si chini ya miaka mitano tu kuhitimisha kile ambacho Wauyghur na mashirika mengine ya haki za binadamu yamekuwa yakisema kwa miaka mingi. Hali karibu isiyo ya kweli ya Waislamu wa Uyghur katika kambi za mateso, kuwalazimisha wanawake Waislamu kuolewa na Wachina wasio Waislamu na kupiga marufuku mila nyingi za Kiislamu, imejulikana kwa miaka mingi. Hii ndio sababu sisi, kama Hizb ut Tahrir / Uholanzi, tuliandaa kampeni ya kitaifa mwanzoni mwa 2019 kuzungumzia dhulma ya serikali ya China na mateso ambayo yamefanywa kwa ndugu na dada zetu Waislamu.
Ripoti hiyo, iliyochapishwa baada ya miaka mingi ya siasa za wazi dhidi ya Uislamu za serikali ya China imechelewa sana. Inaonyesha kuwa kushughulikia jinai zinazofanywa na China dhidi ya Waislamu sio kipaumbele cha moja kwa moja. Wakati huo huo utawala wa China umewadhulumu mamia na maelfu ya Waislamu. Kwa hivyo kulengwa muda wa kuichapisha serikali hivyo basi hauendani na kile ambacho serikali ya China inawafanyia Waislamu. Badala yake, inaendana na maslahi ya Marekani; kimkakati au vyenginevyo. Kutokana na ukweli rahisi kwamba Umoja wa Mataifa ni chombo ambacho kiko mikononi mwa Amerika, kilicholetwa nao baada ya Vita vya Pili vya Dunia ili kudhihirisha ushawishi na utawala wake juu ya ulimwengu wote kupitia "nguvu laini". Muda uliolengwa wa kuchapisha ripoti hiyo unapaswa kuonekana ndani ya muktadha wa mkakati wa Marekani dhidi ya China ijayo. Ripoti hiyo inatumika kama nyongeza pamoja na mipango mingine mingi ndani ya siasa za udhibiti dhidi ya China.
Kuna uwezekano mdogo sana kwamba kupitia nguvu hii, ambayo ni kwa maslahi ya Marekani, shinikizo dhidi ya Waislamu litapunguzwa. Tatizo hata hivyo ni kwamba sera ya China dhidi ya Waislamu imeegemezwa kwenye matamshi yale yale, kile kinachoitwa "vita dhidi ya ugaidi" (vita dhidi ya Uislamu). Amerika, kwa miongo kadhaa, ndiyo iliyoleta uharibifu katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa namna ambayo ingeufanya utawala wa China kuwa na wivu. Je, basi, sio ujinga kutumaini rehema na huruma ya Umoja wa Mataifa na Marekani? Kuweka usalama wa Uislamu na Muislamu mikononi mwa taasisi na dola hizi kutapelekea tu mkwamo. Hakuna kitu kilicho dhahiri zaidi kuliko Waislamu kudhamini usalama wa Uislamu na Waislamu wao wenyewe kupitia kufanya kazi kuelekea katika dola ya Kiislamu itakayowaunganisha na kuwatetea wao na wanadamu wengine wote.
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uholanzi |
Address & Website Tel: 0031 (0) 611860521 www.hizb-ut-tahrir.nl |
Fax: 0031 (0) 611860521 E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl |