Afisi ya Habari
Urusi
H. 15 Jumada II 1441 | Na: 1441/ 02 |
M. Jumatano, 12 Februari 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Miaka 23 ya Kifungo kwa Maneno: “Mola wangu ni Mwenyezi Mungu!”
Mnamo 10 Februari 2020, Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Wilaya ya Yekaterinburg ili muhukumu Eduard Nizamov, kwa kosa la kuandaa amali za Hizb ut Tahrir nchini Urusi, hadi miaka 23 ya kifungo katika ulinzi wa hali ya juu wa adhabu. Ndugu alishitakiwa chini ya vifungu kadhaa vya Kanuni ya Uhalifu nchini Urusi: “kuandaa amali za shirika la kigaidi” (sehemu ya 1 katika kifungu cha 205.5), “kuunga mkono amali za kigaidi” (sehemu ya 1 katika kifungu cha 205.1) na “vurugu la uvamizi wa nguvu” (kifungu cha 278). Pia, vyombo vya habari vya Urusi kwa kujirudiarudia vilimuita Nizamov kama kiongozi wa chama cha Russian Wing. Mnamo 2005 Eduard tayari alikuwa na hatia ya kushiriki katika amali za Hizb ut Tahrir, lakini wakati huo ulinganizi wa Kiislamu haukukandamizwa kwa mpango wa “vita dhidi ya ugaidi,” kwa hivyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili pekee ya majaribio chini ya sehemu ya 2 katika kifungu cha. 282.2 cha sheria ya Kanuni ya Uhalifu nchini Urusi (kushiriki katika amali za shirika lenye msimamo mkali).
Akiongea ‘maneno yake ya mwisho’ katika kesi hiyo Nizamov alizungumza kuhusu Uislamu, mateso ya Waislamu nchini Urusi, siasa za kuupinga Uislamu na sheria za Urusi, vile vile propaganda za kuupinga Uislamu za vyombo vya habari rasmi. Alisema kwamba matokeo ya asili ya sera ya nchi kama hii ni kuonekana kwa chuki dhidi ya Uislamu katika jamii ya Warusi, na serikali kwa umakini na kwa makusudi inaunda picha mbaya ya Uislamu na Waislamu katika jamii kwa ajili ya kuhakikisha sera yake ya kuupinga Uislamu na ukandamizaji dhidi ya Waislamu.
Eduard pia alizungumza kuhusu maisha yake, kuhusu vipi aliutizama kwa uangalifu Uislamu, namna dini ilivyomsaidia katika hali ngumu maishani. Alitoa hoja kuwa Quran ndio chimbuko la sheria pekee ya kweli na thabiti ambayo imebaki bila kutikisika kwa zaidi ya karne 14. Kama mfano wa nyuma wa sheria zinazoweza kubadilika zilizotungwa na mwanadamu alitaja sheria za Urusi, ambazo zinabadilika kwa haraka, ikiwemo kutiliamkazo, ambao huunda hali ya mshangao ambayo Muislamu, hata ajaribu vipi kuzifuata sheria hizi, anabakia kuwa “mhalifu” katika macho ya mashine ya kukandamiza ya Urusi. Eduard alikataa mashtaka yote dhidi yake, akisisitiza kuwa hakuna uhalifu wowote katika vitendo vyake, baada ya ya hapo alileta mashtaka dhidi ya wale wanaouzulia uongo Uislamu na kuwafunga Waislamu kwa imani yao.
Shtaka la ugaidi dhidi ya wabebaji ulinganizi wa Kiislamu sio zaidi ya kukubali kwa udhaifu wa mtu mbele ya ukweli na wale ambao silaha yao pekee ni maneno. Hakuna shaka kuwa Huduma Maalumu za Urusi dhidi ya Wanachama wa Hizb ut Tahrir zitaonekana wazi na wale wote ambao wanahusika katika kuwafunga Waislamu kwa imani yao kwa Mwenyezi Mungu Mtakatifu watalazimika kuhesabiwa kwa uhalifu wao.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
(إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ)
“Hakika, wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa; kisha yatakuwa juu yao majuto; na kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [8:36]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Urusi
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Urusi |
Address & Website Tel: http://www.hizb-russia.info |
E-Mail: mediaoffice.htr@gmail.com |