Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  18 Safar 1444 Na: 1444 / 03
M.  Jumatano, 14 Septemba 2022

 Rambirambi


(Imetafsiriwa)

Leo, Jumatano, Septemba 14, 2022, mheshimiwa Sheikh Saeed Amin Saeed Amun amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89, naye ni baba wa Numan, ambaye, Mwenyezi Mungu akipenda, ni mmoja wa mabwana wa mashahidi huko Peponi. Mazishi yake yalifanyika saa 2:00 usiku kwa saa za Tashkent.

Kuhusiana na hili, sisi katika Hizb ut Tahrir/Uzbekistan tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa wanafamilia hii iliyobarikiwa.

Lau tutamzungumzia mtu huyu, Mwenyezi Mungu amrehemu, na jinsi alivyowalea watoto wake na wajukuu zake kwa namna bora, na hivyo kuwafanya kuwa watu wenye elimu na akili zaidi katika nchi hii, hatutatimiza haki yake. Kwa ufupi, mtu huyu mtukufu aliishi huku akiota kwamba wanazuoni wakubwa watatoka katika Ummah huu kama zamani. Alipotembelea mji fulani, alileta magazeti na vitabu na kuwapa jamaa zake, akizingatia kwamba vitabu na magazeti hayo ndiyo zawadi bora zaidi ambayo angeweza kuwapa.

Tukimzungumzia mtu huyu mtukufu, haiwezekani kumkumbuka mke wake mtukufu, Umm Numan, Saidaminova Dilbarkhan, aliyezaliwa mwaka 1938 na kufariki dunia, Mwenyezi Mungu amrehemu, mwaka 2012. Kufiwa na mwanawe kipenzi kulimuathiri sana. Na kwa vile Numan alikuwa mwana bora wa familia hii iliyobarikiwa, kifo chake cha kishahidi chini ya mateso ya kinyama aliyofanyiwa na mamlaka za utawala kulizijeruhi sana nyoyo za wanachama wake wote. Ummu Numan (Rahmatullah alaiha) aliheshimu da’wah aliyokuwa amebeba mwanawe, vilevile aliwaheshimu sana wenzake katika da’wah hii tukufu, na hakuacha kuwaombea dua kila alipomuombea.

Numan, aliyelelewa na wazazi hawa wawili wema, aliacha mfano wa ajabu kwa wafanyikazi wenzake wote kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu katika uthabiti wake dhidi ya madhalimu. Numan, aliyezaliwa mwaka 1972, aliteswa mnamo mwaka 2000 wakati wa kuhojiwa kwake. Alikuwa na umri wa miaka 28 na aliuawa shahidi chini ya mateso. Na alichagua bora zaidi ya matendo mema na hakutosheka na yaliyo mepesi au rahisi zaidi, jambo ambalo liliwaghadhibisha madhalimu pale alipozungumza na afisa aliyeshiriki katika kumhoji na kumtesa kwa maneno ya chuki: “Wewe ni nani unihoji na hata nimeze mate yangu juu yako, ili nisikutemee usoni mwako.”

Ndugu Wapendwa: Leo amekwenda kwenye rehma za Mola wake Mlezi, baba aliyemlea kijana huyu shupavu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awabariki wazazi hawa wawili kwa wingi wa rehma na msamaha Wake, na awakutanishe pamoja na mtoto wao kipenzi aliyeuawa kishahidi Numan katika mabustani ya Pepo, na aibariki familia hii iliyobarikiwa na watoto wengi kama Numan. Kwa kumalizia, tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mtukufu:

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu