Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  5 Rabi' II 1442 Na: HTY- 1442 / 08
M.  Ijumaa, 20 Novemba 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Abdul Malik Al-Houthi Hatawapatia Watu wa Yemen Usalama wa Chakula
Kama ambavyo Hakuwapatia Ustawi wa Kiuchumi kwa Mapinduzi Yake

(Imetafisiriwa)

Gazeti la Al-Thawra liliripoti mnamo terehe 15/11/2020 M, habari za uzinduzi wa Shirika la Jumla la Kueneza Mbegu Zilizoboreshwa katika Gatuzi la Dhamar, mavuno ya mbegu bora kutoka kwa ngano. Gazeti hilo lilionyesha sehemu za hotuba za Abdul-Malik Al-Houthi juu ya kujitosheleza kwa chakula, kama vile "Yemen ni nchi ya kilimo cha mazao anuwai na ina mazingira anuwai ambayo husaidia kujumuisha na kutoa kile watu wanachokihitaji kwa suala la lishe na chakula", na uthibitisho juu ya "umuhimu wa kuhifadhi maeneo yanayostahili ukulima katika magatuzi anuwai ya Jamhuri ili kufanikisha usalama wa chakula kwa watu wa Yemen ..."

Lakini, kinachozingatiwa kutoka kwa dondoo za Abdul-Malik kufikia usalama wa chakula kwa Yemen ni kukosa kwake mipango yoyote anayoielekeza kwa Baraza la Kisiasa na Wizara ya Kilimo ili kutekeleza kiuhalisia juu ya jinsi ya kupanua kilimo cha nafaka kufikia usalama wa chakula, kama inavyothibitishwa na ukweli kwamba wazo la kuanzisha taasisi ya kuzidisha mbegu bora lilipangwa na kufadhiliwa kutoka nje ya nchi. Ili kuibakisha Yemen kuwa na mafungamano na ng'ambo katika chakula chake, na kwamba taasisi hiyo haitafanikiwa uzalishaji maradufu kama inavyodhaniwa katika upanuzi katika magatuzi mengi, na itabakia mikononi mwa taasisi hiyo ya kigeni, na itafikia idadi fulani ambayo ni ndogo mno katika kujitosheleza kidhati na itaishia hapo.

Mazungumzo ya Abd al-Malik, baraza lake la kisiasa na Wizara ya Kilimo juu ya kujitosheleza kidhati kwa nafaka ni mazungumzo ya viziwi, bila ya mipango ya hatua ambayo inashughulikia kuamua ukubwa wa eneo la ardhi ambalo litapandwa na nafaka, jinsi ya kutoa ardhi hizo, na kisha kupanga mchakato wa umwagiliaji na visima vya kutosha bila mvua na jinsi ya kushughulikia utoaji wa dizeli kwa sababu ya uhaba wake na gharama yake kubwa. Halafu, shida kuu ni kwamba wakulima hawapendi kupanda nafaka, kwa sababu ya bei zake za chini sokoni, ikilinganishwa na mazao mengine ya kilimo.

Imebainika wazi kuwa Abdul-Malik Al-Houthi na baraza lake la kisiasa hawajui chochote juu ya nidhamu ya kiuchumi katika Uislamu wala juu ya hukmu za Sharia zinazohusiana na uchumi, na wanakwenda, kama walivyo kwenda watangulizi wao, kuifanya nidhamu ya kiuchumi wa kirasilimali kuwa ndio kiigizo chao katika kutatua shida za kiuchumi, kama inavyothibitishwa na kuuchelewesha kwa miaka sita iliyopita, usalama wao wa chakula ambapo wakati huo walitegemea Mpango wa Chakula Dunia, ambao pia haukuja kwa sadfa. Zaidi ya hayo, kutatua shida za kiuchumi za Yemen kwa kuendelea kupata mikopo kutoka Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha Duniani, "mikono ya Amerika ya kudhibiti uchumi wa ulimwengu.", kwa kiapo cha Mola wako Mlezi, utapataje utoshelevu wa kidhati katika kilimo cha nafaka?! Kama ambavyo hukushusha bei ya mafuta, ambayo uliifanya kuwa kauli mbiu inayoangaza ya kuingia kwako Sana'a "kabla, wakati na hata baada ya vita," hakika vilevile hutawapa kile unacho kinadi leo katika miito ya kujitosheleza kidhati kwa nafaka! Jambo hilo si lolote ila ni maneno ya ndani tu ya kuwapumbaza wafuasi.

Hakika watu nchini Yemen wanahitaji sana mtu wa kuwaokoa kutokana na udhibiti wa dola za kikoloni juu yao, na aliye na uwezo wa kuutabikisha Uislamu, ikiwemo ndani yake nidhamu ya kiuchumi, na aliye na mipango ya ainisha upya tatizo la kiuchumi na suluhisho zake za kina kutoka kwa nidhamu ya kiuchumi katika Uislamu, na kukanusha nidhamu ya sasa ya kiuchumi wa kirasilimali inayotawala juu ya Yemen. Hakika Hizb ut-Tahrir ina nidhamu ya kiuchumi katika Uislamu, na haipatikani kwa vyama vingine isipokuwa viraka vya nidhamu ya kiuchumi wa kirasilimali na kuiita ya Kiislamu.

Usalama wa chakula nchini Yemen hautapatikana isipokuwa kwa kutabikishwa Uislamu chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah Rashida ya pili, kwa njia ya utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu