Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hotuba ya Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Rashtah, Amir wa Hizb ut Tahrir kuhusu kuanza kwa mwezi wa Dhul Hijjah 1438 Hijria

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwenye Kurehemu

(Imetafsiriwa)

 « وَالْفَجْرِ*وَلَيَالٍ عَشْرٍ »

“Naapa kwa al-Fajiri; na Masiku Kumi”  [Al-Fajr: 1-2]

Kwa wabebaji ulinganizi waaminifu, wasafi, wazuri na wema, ingawa hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Kwa wenye kuzuru tovuti waliojizatiti katika haki inayo tangazwa kwayo, na kheri inayo bebwa nayo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…

Kwa Waislamu wote wanaompenda Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw).

Kwa wote hawa, nawaamkua kwa maamkuzi ya Kiislamu, Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Kama mujuavyo, imekuwa ada kwetu sisi kuwapongeza asubuhi ya siku ya Idd, lakini kwa kuwa imam amesoma katika swala ya al-Fajiri aya hii tukufu:

 « وَالْفَجْرِ*وَلَيَالٍ عَشْرٍ »

“Naapa kwa al-Fajiri; na Masiku Kumi”  [Al-Fajr: 1-2]

Nimeamua kuzungumza nanyi kuhusu masiku haya kumi tukufu ambayo Mwenyezi Mungu amechukua kiapo kwayo, na ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) imeifanya amali njema ndani yake kupendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko siku nyengine zozote. Amepokea Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Sa’eed bin Jubayr kutoka kwa Ibn Abbas aliye sema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

ما من أيام العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام – يعني أيام العشر – قالوا: يا رسول الله، ولا الجهاد في سبيل الله؟ قال: ولا الجهاد في سبيل الله، إلاّ رجل خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع من ذلك بشيء

“Hakuna siku ambazo amali njema ina pendeza zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi – yaani siku kumi za Dhul-Hijjah – (Maswahaba) wakamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata kupigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu? (Mtume) akasema: Hata kupigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa mtu ambaye atatoka kwenda kupigana kwa nafsi yake na mali yake kisha kusirudi chochote katika hivyo (yaani afe shahidi).”

Hizi ndizo siku bora kuanzia tarehe mosi ya mwezi mtukufu wa Dhul-Hijjah mpaka kumalizika kwa siku ya kuchinja ya Idd al-Adha, namuomba Mwenyezi Mungu Ta’ala kuujaalia kuwa na kheri na baraka kwa Uislamu na Waislamu. Na Mwenyezi Mungu azikubali ibada zetu, na kwamba masiku kumi haya yawe na kheri kwa yule atakaye yashuhudia kwa mema na kuyapa haki yake. Masiku haya ni masiku ya ukweli, ikhlasi na kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia amali njema na dua zenye kutakabaliwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Kaka na Dada zangu:

Baadhi ya Mashabab wanasema kuwa usumbufu umezidi dhidi yetu kimataifa, kieneo na sehemu tunazoishi. Ndio hii ni kweli, lakini sio sababu ya kukata tamaa au kuhuzunika, bali ni kivuli cha faraja mbeleni, kwani ongezeko la janga huwa ni ishara ya faraja yake, na ongezeko la giza la usiku ni uashirio wa macheo ya kweli. Na hivi ndivyo ilivyo kuwa kwa makafiri wa Kiqureshi baada ya kuipiga vita Da’wah ya Mtume (saw) na kusimama dhidi yake (saw) kwa kila njia, huku wakiongeza na kuzidisha usumbufu wao. Wakamtenga Mtume (saw) na Maswahaba zake (ra), katika bonde na kuwatesa mpaka kusababisha miguu ya Mtume kumwagika damu. Wakamzulia urongo Mtume (saw) wakimtuhumu uchawi, wazimu na urongo.

 « كَبُرَت كَلِمَةً تَخرُجُ مِن أَفوٰهِهِم ۚ إِن يَقولونَ إِلّا كَذِبًا »

“Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao* Hawasemi isipokuwa urongo tu.”  [Al-Kahf: 5]

Hatimaye janga likaongezeka kwa kukubaliana kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Wakamkimbiza (saw) mpaka katika pango la Thawr, ambamo yeye (saw) na Swahaba wake wa karibu Abubakar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, walijificha, na makafiri walisimama mlangoni mwa pango umbali wa dhiraa moja tu baina yao na Mtume (saw). Tukio hili lilitokea mkesha wa kuamkia siku ya hijra, na baada ya siku moja au mbili, Mtume (saw) akasimamisha serikali mjini Madina al-Munawwarah na kurefusha jengo lake ili kuang’aza Dini hii na kutangaza haki.

  « إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ »

“Bila shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye akili.”  [Az-Zumar: 21]

Na hivyo hivyo katika ulinganizi wetu tunaoubeba, kwa kufuata mfano wa Rasulullah (saw). Hizb ut Tahrir inayoongoza katika ulinganizi huu, mashabab wake na uongozi wake wamekabiliwa na kila aina ya usumbufu na mateso kufikia mpaka daraja ya kupata shahada, kutokana na njama za makhaini, dhulma za majasusi na uovu wa wenye chuki:

Ama kwa Hizb, imepigwa marufuku na kuzuiwa ndani ya nchi kadhaa za Ulimwengu wa Waislamu. Hata katika zile nchi zilizo ruhusu kuwepo na miundo ya vyama vya kila aina kama Indonesia, wameipiga marufuku harakati. Na nchi ambazo zimefungua milango kwa vyama vya kila aina, hata vilivyo potoka pia, kama Tunisia, wameipiga marufuku Hizb… Ama kuhusu ni kwa nini wamefanya hivyo? Jawabu ni kutokana na neno la haki ambalo Hizb inalitangaza.

Ama kwa Mashabab wa Hizb, jela za viongozi katili zinaelezea hadhi yao, kwani wamo ndani ya jela hizo za dhiki huku wakiteswa, na katika jela zao pana (nje) wanaandamwa. Kwa yakini, sisi tunatoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutaregea.

Ama kwa uongozi wa harakati, Amiri wa kwanza alizuliwa urongo wazi wazi, na wenye chuki na majasusi, wakasema na kusema… Amiri wa pili hawakumzulia urongo tu, bali walidai kuwa alihujumu fikra na njia yake… ama mja dhaifu, Amiri wa tatu, hawakujifunga na uzushi pekee au kudai kuwa anahujumu fikra yake, bali walieneza uvumi wa kufariki kwake, wakidhani kuwa watapoza hasira zao! Hakika wao ni wajinga, kwa kuwa wana nyoyo lakini hawazingatii, kama kweli wanazingatia wangejua kuwa kifo cha Amiri wa Hizb hakimaanishi kufa kwa Hizb. Bali, Ata atapokezwa na mtu aliye na nguvu na imara zaidi atakaye wahutubia kwa maneno yake Ta’ala:

 « وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ »

“Na wanapokuwa peke yao wanakuumieni vidole kutokana na chuki. Sema: kufeni kwa chuki zenu! Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.”  [Ali-Imran: 119]

Da’wah hii mwenyewe ni Mwenyezi Mungu, na katu haitadhuriwa na njama za makhaini, dhulma za majasusi na uovu wa wenye chuki, na uzushi wa wazushi, bali itainuka juu juu zaidi na kueneza nuru yake mpaka mbinguni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu Ta’ala na bishara njema za Rasulullah (saw) zitatimizwa katika vigawanyo vyake vitatu:

Utawala huu wa kutenza nguvu utaanguka katika shimo na hatimaye Khilafah katika njia ya Utume itasimama. Mtume (saw) asema:

ثم تكون ملكًا جبرية فتكون ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها الله إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج النبوة، ثم سكت

“Kisha kutakuwepo na utawala wa utenzaji nguvu, utakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu atataka uwepo kisha Mwenyezi Mungu atauondoa wakati anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah katika njia ya Utume, Kisha akanyamaza.”

(Imepokewa na Ahmad kutoka kwa Hudhayfah ibn al-Yaman) Ulimwengu utang’aa na Mwenyezi Mungu itaisimamisha haki na kuziondoa pango za makafiri…

Na tutaking’oa kidola cha kiyahudi. Muslim asema katika Sahih yake kutoka kwa riwaya ya Abu Hurayrah: Mtume (saw) asema:

لا تقوم الساعة حتى يقاتل المسلمون اليهود فيقتلهم المسلمون

“Hakitasimama Kiyama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu watawaua…”

Katika riwaya nyengine, asema (saw):

يقاتلكم اليهود وتنصرون عليهم

“Mayahudi watawapiga vita nyinyi na mutanusuriwa juu yao.”

Na tutaingia katika ardhi iliyo barikiwa tukiwa kama wakombozi, na kuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa adhan ya mwenzetu aliyeko Iraq, aliye tuma ujumbe ndani yake akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu kumjaaliya kuwa Muadhini wa kwanza ndani ya Al-Aqsa baada ya kukombolewa kwake.

Pamoja na kuukomboa mji wa Roma, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Amepokea Ahmad katika Musnad yake na     Al-Haakim na kusahihishwa na Adh-Dhahabi kutoka katika riwaya ya Abu Qaabeel aliye sema:

كنا عند عبد الله بن عمرو بن العاص، وسئل: أي المدينتين تفتح أولاً القسطنطينية أو رومية؟ فدعا عبد الله بصندوق له حلق، قال: فأخرج منه كتاباً، قال: فقال عبد الله: بينما نحن حول رسول الله صلى الله عليه وسلم نكتب إذ سئل رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي المدينتين تفتح أولاً قسطنطينية أو رومية؟ فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: مدينة هرقل تفتح أولاً يعني قسطنطينية.

“Tulikuwa na‘Abdullaah ibn ‘Amr ibn al-‘Aas ilipo ulizwa ni mji gani utakao fungliwa mwanzo, Kostantinopoli (leo Istanbul) au Roma? ‘Abdullaah akasema, “Tulipo kuwa pambizoni mwa Mtume (saw) tunaandika, aliulizwa Mtume (saw): kati ya Miji miwili, ni upi utakao funguliwa mwanzo Kostantiniyya au Roma? Mtume (saw) akajibu: Mji wa mfalme Kisra yaani Kostantinopoli.”

Kostantiniya ushafunguliwa bado kufunguliwa Roma, InshaMwenyezi Mungu, na matarajio ya mwenzetu wa Falastin aliye tuma barua akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu kumruzuku kipande cha ardhi ndani ya mabonde ya Roma kama mfano wa Tamim al-Dari, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, yatatimia.

Hivyo basi, hakutakuwa na nyumba yoyote iliyo jengwa kwa udongo wala sufi ambayo utukufu wa mwenye nguvu au idhlali ya mwenye kudhalilika haitaingia ndani yake. Utukufu ambao Mwenyezi Mungu ataupatia Uislamu, na idhlali ambayo (swt) ataipatia ukafiri.

Amesema Mtume (saw) katika hadith iliyo pokewa katika Musnab ya Ahmad kutoka kwa riwaya ya Tamim al-Dari asema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:

ليبلغن هذا الأمر ما بلغ الليل و النهار ، و لا يترك الله بيت مدر و لا وبر إلا أدخله الله هذا الدين بعز عزيز أو بذل ذليل عزا يعز الله به الإسلام و ذلا يذل به الكفر.

“Mwenyezi Mungu atalifikisha jambo hili (Uislamu) kila panapo fikiwa na usiku na mchana, wala hataiwacha hata nyumba moja iliyo jengwa kwa udongo wala kwa sufi isipokuwa ataiingiza ndani yake dini hii kwa izza ya mwenye izza na idhlali ya wenye kudhalilika, Mwenyezi Mungu ataupa izza Uislamu na kuudhalilisha ukafiri…”

Baihaqi amepokea hadith sawa na hii katika As-Sunan Al-Kubra pia katika Mustadrak ya Hakim.

Waovu na wazushi, wale ambao nyoyo zao zina maradhi ya ufisadi katika ardhi, watasema kuwa tunaota, au ni waotaji… wanaofanana nao washatangulia kusema haya. Walisema kuhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na Maswahaba zake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao: dini yao imewadanganya, wataweza vipi kuzifikia hazina za Kisra na Kaisari?! Hatimaye ahadi ya Mwenyezi Mungu ikatimia licha ya uovu wa wale walio angamia. Kwa hivyo, Kisra na Kaisari walianguka na dola ya Kiislamu na bendera yake ikasimama, hili pia litajirudia tena kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na wenye chuki watakufa na chuki zao na kufuatiwa na dhulma za majasusi na makhaini na kila anaye zungumza batili.

 « وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ »

“Na ndipo watakapo jua wale wanao dhulumu ni mgeuko gani watakao geuka.”  [Ash-Shu’ara: 227]

Kaka na Dada zangu:

Hatufanyi kazi tu kwa ajili ya kujipumbaza, bali tunafanya kazi tukiwa na imani na ahadi ya Mwenyezi Mungu, ambayo sio tu kwa Mitume, na sio ya Akhera pekee, bali pia ni kwa Waumini hapa duniani na kesho Akhera.

  « إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ »

“Hakika sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watakapo simama Mashahidi (kutoa ushahidi wao) …”  [Ghafir: 51]

Nawaahidi kaka na dada zangu, kwamba Hizb tangu kubuniwa kwake mpaka leo, mara nyingi imekaribia kufikia malengo yake, lakini

« لِكُلِّ أَجَلٍ كِتَابٌ »

“Kila kipindi kina hukmu yake.”  [Ar-Ra’d: 38]

Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye na hikma pana… ikiwa Al-Qaweey Al-Aziz amepitisha jambo, hulipatia sababu nyepesi za kulifikia na wala halita cheleweshwa

  « إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا »

“Hakika Mwenyezi Mungu atatimiza amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu amejaalia kila kitu na kipimo chake.”  [At-Talaq: 3]

Kutamatisha, narudia tena yale niliyo anza nayo, nazungumza nanyi katika siku ya mwanzo ya siku hizi kumi zilizo barikiwa, ambazo Mwenyezi Mungu aliapa kwazo, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuzungumza kuzihusu:

ما من أيام العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام – يعني أيام العشر (من ذي الحجة

“Hakuna siku ambazo amali njema ina pendeza zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi – yaani siku kumi za Dhul-Hijjah.”

Hizi ni siku bora, kuanzia tarehe mosi ya mwezi mtukufu wa Dhul-Hijjah mpaka kumalizika kwa siku ya kuchinja ya Idd al-Adha, namuomba Mwenyezi Mungu Ta’ala kuujaalia kuwa na kheri na baraka kwa Uislamu na Waislamu. Na Mwenyezi Mungu azikubali ibada zetu, na kwamba masiku kumi haya yawe na kheri kwa yule atakaye yashuhudia kwa mema na kuyapa haki yake. Masiku haya ni masiku ya ukweli, ikhlasi na kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu kupitia amali njema na dua zenye kutakabaliwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu… Namuomba Mwenyezi Mungu azirudishe tena siku zile tuwe chini ya kivuli cha bendera ya Uqab tumiliki kheri kubwa mikononi mwetu, na ndimi zetu kuitamka, nyoyo zitulizane, na vifua kupanuka kwa ajili yake:

  « وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ* بِنَصْرِ اللَّهِ ۚ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ »

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye na ndiye mwenye nguvu mwenye kurehemu.”  [Ar-Rum: 4-5]

Kutamatisha pia, nakariri tena kuwa Da’wah hii mwenyewe ni Mwenyezi Mungu, na kamwe haitadhuriwa na njama za makhaini, dhulma za majasusi, au uovu wa wenye chuki, wala uzushi wa wazushi, bali ulinganizi wa Mwenyezi Mungu utainuka, na nuru yake itawavutia watazamaji mukhlisina na muangaza wake utaziweka mbali nyoyo za wenye chuki na hasadi.

 « وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ »

“Na bila ya shaka mutajua habari zake baada ya muda.”  [Sad: 88]

 

Wassalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Ndugu Yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Amir wa Hizb ut Tahrir

 

1 Dhul Hijjah 1438 H

23/08/2017 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 28 Januari 2020 12:09

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu