Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tanzia na Rambirambi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir na Mkuu wa Diwan ya Madhalim kwa Kifo cha Dkt. Abdul Halim Muhammad Al-Ramahi (Abu Imad)
(Imetafsiriwa)

[وَمَن يُطِعِ اللّهَ وَالرَّسُولَ فَأُوْلَـئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاء وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَـئِكَ رَفِيقًا]

“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!” [Surah An-Nisaa 4:69]

Amiri wa Hizb ut Tahrir na Mkuu wa Diwan ya Madhalim wanamuomboleza, huku wakiamini Qadhaa wa Qadar ya Mwenyezi Mungu:

Dkt. Abdul Halim Muhammad Al-Ramahi (Abu Imad)

ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 84. Alikuwa mmoja wa watu mashuhuri na wachaMungu wa Diwan hii, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Aliuacha ulimwengu huu wa mapito, na kuhamia kwenye makao ya Akhera ya milele, usiku wa kuamkia Jumapili, tarehe 11 ya Ramadhan iliyobarikiwa 1444 H, sawia na tarehe 2 Aprili 2023 M.

Alikuwa, Mwenyezi Mungu amrehemu, mwongofu juu ya haki na kamwe hakuiacha, bila ya kuogopa lawama ya mwenye kulaumu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hatumsifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Alikuwa na uzoefu mkubwa katika kuchunguza undani wa kesi yoyote, ambayo iliwasilishwa kwa Diwan. Yeye na ndugu zake wangesimama juu ya uhalisia wa jambo hilo. Wangeweka jambo hilo mahali pake. Alihukumu juu yake, pamoja na ndugu zake, akiweka hukumu sahihi ya kimahakama. Macho yake yangeelekezwa kwenye Pepo ambayo upana wake ni kama mbingu na ardhi, iliyotayarishwa kwa ajili ya wachamungu.

Macho yanabubujika machozi na moyo unahuzunika, na hatusemi isipokuwa yale yanayomridhisha Mola wetu, na ninahuzunishwa na kuondoka kwako ewe kipenzi.

Sisi katika Hizb, uongozi pamoja na Mashababu, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) subira na faraja kwa ajili yetu na jamaa zake watukufu, na tuwe kama alivyosema (swt),

[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surah Al-Baqarah 2:156]

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) akurehemu, na akupokee kwenye Mabustani Yake Mapana

[فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيكٍ مُقْتَدِرٍ]

“Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.” [Surah Al-Qamar 54:55].

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”

Ndugu Yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Amiri wa Hizb ut Tahrir

11 Ramadan 1444 H  

Sawia na 2/4/2023 M 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu